Mwanzilishi wa Facebook na CEO Mark Zuckerberg amefanikiwa kupata
shahada ya heshima kutoka katika chuo kikuu cha Havard, Marekani.
Bosi huyo ambaye ni miongoni mwa matajiri wakubwa duniani kwa mujibu wa
Forbes, aliwahi kusoma katika chuo hicho miaka 12 iliyopita. Baada ya
Zuck kupatiwa heshima hiyo, kupitia mtandao wake wa Facebook
alimuandikia ujumbe mama yake unaosomeka, “Mom, I always told you I’d
come back and get my degree.”
Miaka kadhaa iliyopita, bosi huyo aliwahi kukaririwa na gazeti la chuo
hicho lijulikanalo kama “The Harvard Crimson” akisema hataweza kurudi
tena chuoni hapo kusoma na badala yake atawekeza nguvu nyingi katika
mtandao wake wa Facebook ambao ulikuwa unakuwa kwa kasi katika kipindi
hicho.
Kwa sasa Mark mbali na kumiliki Facebook ambayo inautajiri wa $61.5
lakini pia anamiliki mitandao mingine kama Instagram na Whatsapp.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment