MAKAMU wa Rais wa Klabu ya Simba, Geofrey Nyange ‘Kaburu’ amewapongeza
mahasimu wao Yanga, kwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, na
kusema wanajipanga kwa msimu ujao.
Simba imeshindwa kumaliza vizuri ligi ya msimu huu, baada ya kuongoza
kwa tofauti ya pointi nane kwa muda mrefu hadi ilipokuja kuenguliwa
kileleni kufuatia kipigo cha mabao 2-1, kutoka kwa Kagera Sugar.
Akizungumza jana, Kaburu alisema wanajisikia vibaya kuukosa ubingwa wa
msimu huu, lakini hawana budi kuwapongeza Yanga kutokana na kufanikiwa
kutetea taji hilo kwa bahati dakika za mwisho.
“Yanga ni wapinzani wetu kwenye ligi ya Tanzania, tunawapongeza kwa taji
hilo lakini ni bahati ndiyo imewabeba kwa sababu karibu msimu mzima
sisi ndiyo tumeongoza ligi lakini mwishoni tuliharibu na wenzetu kupata
nafasi,” alisema Kaburu.
Kiongozi huyo alisema baada ya kupoteza taji hilo nguvu zao kwa sasa
wamezielekeza kwenye mchezo wa fainali ya Kombe la FA, dhidi ya Mbao FC
utakaopigwa kwenye Uwanja wa Jamhuri Dodoma Mei 28 mwaka huu.
Yanga inaongoza msimamo ikiwa na pointi 63 na Simba ina pointi 65 huku
kila mmoja akibakiwa na mechi moja. Ili Simba itwae ubingwa inahitaji
kuomba Mbao iifunge Yanga mabao 5-0 katika mechi ya mwisho huku yenyewe
ikiifunga Mwadui mabao 8-0 jambo ambalo kwa mwenendo wa ligi ulivyo
halitawezekana.
Kaburu alisema wamepanga timu yao kuipeleka Zanzibar kupiga kambi ya
wiki moja kujiandaa na mchezo huo wa fainali lengo ni kuhakikisha
wanashinda ili kushiriki na michuano ya kimataifa.
Alisema, baada ya mchezo wao wa mwisho wa ligi dhidi ya Mwadui
keshokutwa, kikosi chao kitaondoka Dar es Salaam Jumapili kwa ajili ya
kambi hiyo ambayo wanaamini itakuwa na mafanikio kutokana na ari
waliyokuwa nayo wachezaji na viongozi.
Huu ni msimu wa nne mfululizo Simba inalikosa taji hilo, na kuwaachia
wapinzani wao Yanga wakilitwaa moja kwa moja baada ya kulichukua mara
tatu mfululizo
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment