Maisha ya mapenzi ya kweli ni yale yaliyo na furaha pande zote mbili na
kwamba kila mmoja anaridhika na mwenzi wake kwa hali na mali.
Mapenzi kama yanavyosemwa na watu ni sanaa kama sanaa zingine zilivyo.
Kama ni mchezo, basi una sheria zake. Leo nakuonyesha mbinu ambazo
ukizingatia ndoa yako haitokuwa na matatani.
Ni maoni tofauti tofauti kutoka kwa wadau pamoja na wazoefu wa masuala haya ya mahusiano.
Upendo
Kila mwanaume anataka kujisikia anapendwa. Anataka kuona kuwa mwenza wake anampenda kiuhalisia na anamjali wakati wowote.
Heshima
Hata pale anapokuwa hayupo, anataka mwenzake wake awe nyuma yake, kumuongelea na kumheshimu.
Kukubalika
Kila mwanaume anataka kujisikia mwenza wake anamkubali na kumthamini kwa
mambo mbalimbali kama vile penzi lake, muda, jitihada, anavyojituma na
kila anachokifanya kwa mwenza wake.
Yeye ni bora zaidi
Anataka mwenza wake kujisikia kuwa yeye ni bora zaidi. Kila mwanaume
anataka ajisikie kuwa yeye ni mwanaume bora zaidi kuliko wote aliowahi
kuwa nao, na wengine wanataka kujisikia kuwa ni mwanaume pekee ambaye
umewahi kuwa naye hata kama anajua si kweli.
Uaminifu
Mwanaume anahitaji mwenza wake awe mwaminifu. Uaminifu husaidia kujenga
mapenzi zaidi, kila kitu kwa mwanaume na kadiri mwenzake anavyokuwa
mwaminifu, ndivyo hawezi kuwa na wivu kwani anakuwa ameshajiaminisha.
Ukweli
Kila mwanaume anahitaji kujua kuwa anaweza kumwamini mwenza wake na
kwamba naye anamwamini, ukiwa mkweli ni rahisi mume kukujengea imani,
kuwa mkweli kwa kila jambo.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment