Kiungo wa Klabu ya Azam FC, Himid Mao ambaye mwanzoni mwa mwezi huu
alienda nchini Denmark kufanya majaribio na Klabu ya Randers FC, ndoto
ya kiungo huyo ya kucheza soka la kulipwa ipo karibu kutimia kwani
mabosi wa Klabu hiyo na wa Azam FC wamekutana kufanya mazungumzo ya
mwisho kuhusu usajili wake.
Hatua hiyo imekuja baada ya Himid kufuzu majaribio ya
siku 10 aliyoenda kufanya katika timu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu ya
Denmark, mapema mwezi huu.
Ofisa Habari wa Klabu ya Azam FC, Jaffar Idd
amesema kuwa kwa sasa wapo kwenye mazungumzo na mabosi hao wa Randers
baada ya kuwapa habari kwamba kiungo wao amefuzu majaribio yake.
“Tupo kwenye majadiliano na wao, tunasubiri
kusikia ofa yao na kama tukikubaliana basi Himid ataenda kujiunga nao
kwa sababu wametuambia tayari amefuzu, hivyo mazungumzo yaliyopo sasa ni
baina yao na sisi”, alisema Jaffar Idd kwenye mahojiano yake na Gazeti la Championi.
Kwa upande mwingine Kocha wa Azam FC, Aristica Cioaba
amesema kuwa kama dili hilo litafanikiwa, basi anamtakia kila la heri
kiungo huyo.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza HapaFollow me instagram>>>Bonyeza Hapa
Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment