Mchezaji wa klabu ya Azam FC na Taifa Stars, Kiungo Himid Mao amekwea
pipa jana jioni akielekea nchini Denmark, kwa ajili ya majaribio ya
kutafuta kucheza soka la kulipwa katika bara la Ulaya.
Kiungo huyo machachari anakwenda kufanya majaribio yake ya soka la
kulipwa katika klabu ya Randers FC ambayo iko katika ligi kuu nchini
Denmark maarufu kwa jina la Superliga.
Mao amekuwa katika kiwango cha juu katika ligi ya msimu huu pamoja na michuano mingine ambayo kiungo huyo amekua akicheza.
Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Saad Kawemba, amethibitisha kuondoka kwa
mchezaji huyo akisema, “Tuna wachezaji zaidi ya sita wameenda ulaya kwa
majaribio, na Mao ni mmoja wao. Taarifa zingine tutatoa kama klabu ila
Mao ana baraka zote za klabu kuondoka.
Amepata nafasi ya kuondoka, na hakuna atakaemzuia, wote wataondoka na
kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu wote tunaamini watafanikiwa na wataweza
kuanza maisha mapya katika nchi moja wapo,”
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment