ILI kudumisha muonekano wa ujana kwa mwili wako unahitaji kuupa mahitaji
yake yaliyobadilika. Kuzuia kuzeeka haraka unahitaji chakula chenye
calcium ya kutosha kuipa mifupa yako nguvu na kupata chakula chenye
collagen kwa wingi ili kuifanya ngozi yako isiwe na makunyanzi mwilini,
kiashiria cha uzee.
Katika miaka ya 1950 Mmarekani mwanasayansi mtafiti, Denham Harman
aligundua kuwepo uhusiano mkubwa kati ya mwili kuzeeka na uwepo wa
kemikali ambazo hutengenezwa na mwili katika ufanyaji wake kazi wa
kawaida katika mwili wa mtu, kitaalamu huitwa free radicals.
Mwili una uwezo wa kudhibiti madhara yanayotokana na uwepo wa free
radicals kwa kiasi fulani, lakini idadi ikizidi mwili huzidiwa na
madhara mengi hutokea, yakiwepo kuzeeka kwa mwili na magonjwa mengi kama
kansa, magonjwa ya moyo, mifupa (arthritis), usahaulifu (Alzheimer’s),
ugonjwa wa parkinson’s na kisukari.
Free radicals katika mwili huweza kuongezeka kwa kutumia vitu kutoka nje
ya mwili. Sumu kutoka nje zinazozalisha free radicals katika mwili ni
pamoja na hewa chafu hasa inayotoka kwenye viwanda, moshi wa sigara, na
chakula chenye dawa za kuulia wadudu na utumiaji wa pombe kwa kiwango
cha kuzidi kiwango.
Kiwango kidogo cha free radicals kinachozalishwa na mwili wenyewe
kinaweza kikadhibitiwa vizuri na kemikali nyingine zinazoitwa
antioxidants ambazo nazo pia huzalishwa na mwili.
Free radicals za ziada zinazozalishwa na vitu kutoka nje ya mwili
zisipodhibitiwa kikamilifu husababisha madhara mengi pamoja na magonjwa
yaliyotajwa hapo juu.
Hivyo basi tunahitaji kupata chakula chenye antioxidants kwa wingi ili
kuisaidia miili yetu kupambana na kemikali hizi za ziada. Kuna aina
nyingi za antioxidants zikiwemo vitamini C, vitamini E, flavonoids na
polyphenols kwa kutaja tu bila kuingia kwa undani zaidi.
Baada ya utangulizi huo, sasa ni wakati wa kupitia chakula ambacho
kikitumiwa kitakupa vitu tulivyovitaja hapo juu na kuufanya mwili wako
kuwa na mwonekano wa ujana daima.
Vitamini C
Katika utafiti wa Mtafiti Herman uliofanywa kwenye kikundi cha wanawake
wenye umri wa miaka zaidi ya 40 ulionyesha kwamba wanawake wanaotumia
chakula chenye vitamini C zaidi walikuwa na makunyanzi zaidi na ngozi
zao hazikuwa kavu ukilinganisha na wale ambao walitumia vitamini hiyo
kidogo.
Hii ni kwa sababu vitamini C ni antioxidant yenye nguvu inayozuia
uharibifu wa seli na DNA za seli hivyo kulinda uzalishaji wa collagen
ambayo ndiyo nguzo muhimu ya kulinda ngozi yako.Unashauriwa basi upate
angalau miligram 75 za vitamini hii kwa siku.
Kwa mfano unaweza kupata chungwa moja wakati wa kifungua kinywa na
pilipili tano za njano ndani ya saladi kwenye mlo wako wa mchana.
Chakula chenye vitamini C kwa wingi ni broccoli, strawberries, pilipili
nyekundu, nyanya, tikitimaji n.k.
Chakula chenye protini
Tafiti zilionyesha kuwa wanawake waliotumia protini zaidi walikuwa na
makunyanzi machache zaidi kwenye ngozi zao kuliko wale ambao walitumia
protini kidogo, hii kwa sababu protini hutoa viungo muhimu katika ujenzi
wa collagen.
Ili upate protini unashauriwa kula nyama ya kuku isiyo na ngozi, sehemu
nyeupe ya mayai na samaki. Unapochagua kula nyama ya ng’ombe au mbuzi,
pendelea kutumia ile isiyo na mafuta. Matumizi ya soya yameonyesha
kusaidia kuondoa ile mistari myembamba kweye macho.
Samaki
Samaki wa baharini wenye mafuta wamebainika kuwa na kiwango kikubwa cha
‘omega-3 fatty acids’, kitu ambacho husaidia kuilinda ngozi yako
kutokana na mionzi mibaya ya jua ambayo hudhoofisha collagen.
Nafaka
Utumiaji wa nafaka zisizokobolewa badala ya wali mweupe, mikate
inayotokana na ngano isiyokobolewa (brown bread) na nafaka nyingine una
faida nyingi. Moja ni kuzuia mwongezeko wa insulin katika mwili ambayo
ina madhara ya kuharibu ngozi. Pia nafaka nzima ni chanzo cha madini ya
selenium ambayo husaidia kuikinga ngozi yako kutokana na mionzi ya jua.
Unashauriwa kutumia mchele usiokobolewa (brown rice), shayiri na ngano
isiyokobolewa ili uweze kupata madini haya yatakayokusaidia kulinda
ngozi yako.
Green Tea
Green tea ni kinywaji chenye antioxidants nyingi. Unywaji wa vikombe
viwili au vitatu kwa siku vya chai hii utaifanya ngozi yako kuwa nyororo
na kutopata makunyanzi.
Hatuwezi kuorodhesha vyakula vyote ambavyo vinafaa katika kuzuia kuzeeka
haraka katika nafasi hii, hivyo makala yetu inatoa mwongozo tu wa kula.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment