RAIS John Magufuli amesema serikali inawachunguza watumishi wa umma
waliogushi umri ili wasibaki kwenye utumishi wa umma kwa muda ambao
hawakustahili kuwa kazini.
Kadhalika, amesema kuna watumishi wenye miaka 60 na zaidi ambao hawataki
kustaafu huku waking’ang’ania ajira na madaraka, na wengine
wakijipachika vyeo vya ukurugenzi.
Akizungumza katika sherehe za maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani
(Mei Mosi) ambazo kitaifa zilifanyika jana katika Viwanja vya Chuo
Kikuu cha Ushirika Moshi, Rais Magufuli alisema uchunguzi huo wa umri
umeshaanza.
“Wako watumishi ambao wamebadilisha umri wao," alisema Rais Magufuli.
"Wamebadilisha miaka yao na unakuta ni mzee kabisa, lakini kabadilisha
umri."
"Kuna watu ambao ni wazee tena kuliko mimi. Wanasema hawaondoki eti ndio wakati umefika, hao nao tunawachunguza.”
Katika hotuba yake, Rais Magufuli alisisitiza kuwa wapo watumishi wa
umma ambao bado wanafanya kazi wakiwa wameshatimiza umri wa kustaafu kwa
lazima wa miaka 60 lakini hawataki kustaafu ili kuachia nafasi wegine
waajiriwe.
Uchunguzi huo unakuja siku chache baada ya serikali kufanya uhakiki wa
vyeti vya elimu vya wafanyakazi wake na kugundua takriban watumishi
10,000 wana vyeti vya kughushi. Wamefukuzwa kazi mara moja.
Akionyesha kukerwa na hali hiyo Rais Magufuli alisema:
“Sheria za nchi yetu hazijasema mtu anayetakiwa kufanya kazi lazima awe na digrii, kila kazi ina qualification (sifa) zake.
"Haiwezekani Watanzania wote wakawa na digrii, darasa la saba
wanaajiriwa, form four (kidato cha nne) wanaajiriwa na wenye certificate
(cheti) wanaajiriwa.
"Na kila mmoja ana wajibu wa kuajiriwa.
”Tunachosisitiza hapa kama wewe ni darasa la saba na unataka kuajiriwa
kaombe kazi ya darasa la saba, kama wewe ni form four kaombe kazi ya
form four, kama una certificate nenda ukaombe kazi ya certificate.
Usiende ukatafute mavyeti ya kufoji ukajiita daktari kumbe hata unesi
haujafikia,”alisema
Aidha, Rais Magufuli alisema wako watumishi ambao wamekuwa wakijiita
wakurugenzi, "watu wakubwa wakubwa tu, wana mavyeti ya kufoji, halafu
wanawanyanyasa hawa watu wa chini ambao wana vyeti halali."
Alisema kundi hilo nalo ni miongoni mwa watumishi wa umma ambao serikali
imekuwa ikiwaamini lakini imegundua kumbe hawastahili nafasi hiyo.
Mbali na kuahidi kushughulikia watumishi walioghushi umri ili kufanya
kazi nje ya miaka ya kustaafu, Rais Magufuli alistahili kurejesha
nyongeza ya kila mwaka ya mishahara na upadishaji watumishi madaraja.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment