Tuesday, 2 May 2017

FAHAMU Njia za Mkato Zinavyoweza Kukupa Mafanikio Yenye Uchungu.

NDUGU zangu, linapokuja suala la kutafuta maisha mazuri na yenye mafanikio, wapo watu ambao wanadiriki kujiingiza katika shughuli zisizo halali ambazo mwisho wa siku zinaweza kuyahatarisha maisha yao.
Lakini niwakumbushe tu kwamba, zipo kazi nyingi tu ambazo ukizifanya kwa nguvu zote na kwa malengo unaweza kuwa na mafanikio makubwa na ukaishi maisha ya furaha na amani. Hapa nazungumzia zile kazi ambazo ni halali.
Lakini huwa najiuliza, hawa wanaofanya kazi zisizo halali walishawahi kujiuliza hatima ya maisha yao itakuwaje?
Kwa nini ufi kie hatua ya kufanya kazi ambayo itafanya maisha yako yawe hatarini? Wapo wanaosema eti wanafanya hivyo kwa sababu maisha ya sasa ni magumu na hivyo ugumu huo wa maisha unaweza kuukabili kwa kufanya kazi hizo.
Hii ni hatari sana na hata hao wanaojipatia mapesa kwa kufanya kazi kama vile za kuuza madawa ya kulevya, bangi, utapeli, uchangudoa na shughuli nyingine za namna hiyo maisha yao si ya furaha kama watu wanavyodhani. Wanaishi maisha ya wasiwasi huku wakihofi a usalama wa maisha yao.
Uchunguzi unaonesha kwamba wengi wanaofanya biashara hizo haramu mwisho wao huwa mbaya sana ambapo baadhi yao huishia kuuawa, kufa ama kufungwa jela.
Nenda kwenye magereza leo hii utakuta waliojaa huko wanatuhumiwa kwa ujambazi, wizi, uuzaji wa madawa ya kulevya, watu ambao walidhani kwa kufanya hivyo wanaweza kuyafanya maisha yao yakawa mazuri kumbe ndiyo wanajiweka katika wakati mgumu zaidi.
Mimi nadhani zipo kazi nyingi tu ambazo unaweza kuzifanya na ukawa tajiri ama kuwa na mafanikio makubwa bila kuiba kitu cha mtu wala kudhulumu. Kwa kutumia akili yako, nguvu zako pamoja na maarifa aliyokujaalia Mungu naamini unaweza kufanikiwa na kuishi maisha ya amani yaliyojaa furaha tele.
Siyo mpaka uibe ndiyo unaweza kufanikiwa, siyo lazima uuze madawa ya  kulevya wala kuuza mwili wako ndiyo ufanikiwe. Fahamu kwamba wapo watu wengi waliopata mafanikio makubwa kwa kupigana kihalali.
Hivi unadhani watu mabilionea na wenye mafanikiio makubwa duniani
walifi kia hatua hiyo kwa njia za mkato? La hasha! Hao walitumia akili na nguvu zao katika kuusaka utajiri huo.
Siku zote ukae ukijua kwamba maisha hayana njia ya mkato. Kwa maana hiyo basi wanaoendesha maisha yao kwa njia ya mkato, hawana furaha na mafanikio ya kweli katika maisha yao.
Kimsingi wanaotegemea kuendesha maisha yao kwa kufanya kazi ambazo siyo halali wako kwenye nafasi nzuri ya kukumbwa na balaa katika maisha yao kiasi cha kuwafanya kutozifurahia fedha walizonazo.
Wapo akina dada ambao wameridhika kuendesha maisha yao kwa kufanya biashara ya kuuza miili yao. Wanaofanya hivyo wanaeleza kwamba kinachowasukuma kufanya hivyo ni ugumu wa maisha.
Maisha yanaweza kuwa magumu kama hutajishughulisha.
Lakini hata kama maisha ni magumu kiasi gani ndiyo ufi kie hatua ya kuweka rehani maisha yako?
Asikudanganye mtu wengi wanaofanya biashara ya uchangudoa maisha yao yako hatarini hasa kipindi hiki ambacho ugonjwa wa Ukimwi unasumbua kila kona ya ulimwengu.
Labda nihitimishe kwa kusema kwamba, kuna kila sababu ya kubadilika na kuangalia njia sahihi za kuendesha maisha yetu. Tuachane na tamaa zisizo na msingi na kutaka kujipatia fedha kwa njia za makato. Tuelewe kwa kufanya hivyo hatuwezi kupata mafanikio ya kweli na tutakuwa tunayahatarisha maisha yetu.


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa 

0 comments:

Post a Comment