Monday, 5 June 2017

Eh..Kumbe Mrisho Ngasa Yupo Yanga kwa Makubaliano Haya Eti.

WINGA aliyekipiga Mbeya City msimu uliopita, Mrisho Ngassa, amerejea kwenye klabu yake ya zamani ya Yanga na leo amejumuishwa kwenye kikosi hicho kilichocheza na Tusker kwenye michuano ya Super Cup, katika Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam.
 Ngassa, ambaye mkataba wake na Mbeya City umemalizika baada ya msimu wa Ligi Kuu Tanzania Bara, ameonekana akifanya mazoezi na kikosi cha klabu hiyo ya Jangwani katika Uwanja wa Chuo cha Polisi Kurasini, Dar es Salaam.
Taarifa ambazo BINGWA imezinasa jana kwenye mazoezi hayo, ni kwamba Ngassa ameagizwa kujiweka fiti ili kuangaliwa uwezekano wa kusajiliwa kwa ajili ya msimu ujao.
“Ngassa ameomba kurejea Yanga na benchi la ufundi kupitia uongozi limempa masharti ya kuhakikisha anajifua na kurejesha kiwango chake ili waangalie uwezekano wa kumpa mkataba,” kilisema chanzo hicho.
Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Mkwasa, alisema michuano hiyo haimzuii mchezaji kutoka timu nyingine kushiriki, bali kikubwa ni kufuata kanuni zao walizoweka.
“Kwa sasa Ngassa yupo na timu yetu akifanya mazoezi na ikibidi anaweza kutumika pia katika michuano hiyo, suala la kumsajili itategemeana na mapendekezo ya kocha, akimhitaji tutampa mkataba,” alisema Mkwasa.
Kocha msaidizi wa Yanga, Juma Mwambusi, amesema anachofahamu yeye kuhusu Ngassa ni kwamba amekwenda Yanga kwa ajili ya kufanya mazoezi ili ajiweke fiti na wapo wengine wengi.
“Siyo Ngassa pekee anayefanya mazoezi na Yanga, wapo wachezaji wengi ambao huwezi kuwazuia wala kuwauliza wamefuata nini, kwani kazi yangu ni kufundisha, jukumu la kuuliza nani yupo kwa sababu gani ni la uongozi wa juu,” alisema.
Mbali na Ngassa, wachezaji wengine waliojiunga na kikosi hicho kwenye mazoezi ya kujiandaa na michuano hiyo ya Super Cup ni Babu Ally wa Kagera Sugar, Zahora Pazi (Mbeya City), Haruna Chanongo aliyecheza Mtibwa Sugar msimu uliopita, Emmanuel Kichiba na mshambuliaji mmoja wa Ghana.


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Askari wa Bunge Wapangiwa Vituo Vingine vya Kazi kwa Kusuasua Kumtoa Nnje ya Bunge Mnyika.

Askari walioagizwa kumtoa, Mbunge wa Kibamba, John Mnyika bungeni Ijumaa iliyopita, wamepangiwa vituo vingine vya kazi kwa kuchelewa kutekeleza agizo la Spika.
Spika wa Bunge, Job Ndugai amesema aliwashangaa askari hao kwa jinsi walivyokuwa wanambeleza mbunge huyo wa Kibamba kutoka nje.
"Askari hawa wataendelea kuhamishwa mpaka pale tutakapowapata wanaofaa," amesema Ndugai.
Mnyika alitolewa bungeni Ijumaa iliyopita baada ya mmoja wa wabunge kusema ‘Mnyika mwizi’ akimhusisha na wizi wa madini.
Kutokana na hali hiyo Mnyika alimtaka Spika kuchukua hatua dhidi ya mbunge aliyesema kuwa yeye ni mwizi lakini Spika alisema hajui hilo na haijaingia kwenye hansadi.
Hata hivyo Mnyika alisisitiza kuwa mambo hayawezi kwenda hivyo. 
Baada ya majibizano kati yao Spika aliamuru walinzi wamtoe Mnyika nje ya Bunge

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Issue ya John Bocco na Okwi Kusaini Simba...Hans Poppe Aanika Mambo Yote Hadharani.

Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili wa Mabingwa wa Kombe la Shirikisho nchini Simba SC, Zakaria Hans poppe amekanusha timu yake kuwasajili wachezaji Aishi Manula, John Bocco, Shomari Kapombe pamoja na Emmanuel Okwi na kusema taarifa hizo ni za uongo.
Hans poppe amebainisha hayo baada ya kuenea kwa tetesi kuwa timu hiyo imeshawasajili wachezaji hao baada ya msimu 2016/2017 kuisha hivi karibuni.
“Ni uongo kusema kuwa sisi tumeshaingia mkataba na mchezaji yoyote maana hadi sasa mikataba ya wachezaji bado haijamalizika, tukisajili mtu sasa itakuja kuwa kama suala la Kessy ambalo tuliwaambia Yanga lakini wakajifanya wajuaji, matokeo yake wametema milioni 50 tena kwa huruma yetu” alisema Poppe.
Pamoja na hayo, Hans poppe amesema kwa sasa hawezi kusema chochote kama wameanza mazungumzo na wachezaji hao wanaotajwa zaidi.


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Sunday, 4 June 2017

Shabiki wa simba Fc aonyesha mapenzi ya zati kwa timu yake baada ya nyimbo yake kukonga moyo ya shabiki.

Shabiki wa simba Fc aonyesha mapenzi ya zati kwa timu yake baada ya nyimbo yake kukonga moyo ya shabiki.
https://my.notjustok.com/track/download/id/223072



Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Maajabu..Namba ya Simu ya Ben Saanane (Msaidizi wa Mbowe) Aliyetoweka Yatumika Whats App.

Wakati hofu ikiwa imetenda baada ya jumla ya miezi minane kupita tangu alipopotea kwenye mazingira ya kutatanisha, matumaini mapya yameanza kuibuka baada ya simu yake kuonekana imetumika kwenye mitandao ya kijamii.

Ben Saanane ambaye alikuwa msaidizi wa Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe alitoweka mwaka jana na kumekuwapo na hisia nyingi kuwa huenda alishafariki dunia kutokana na kuwa, hakuna yeyote anayefahamu alipo kijana huyo aliyekuwa akichipukia katika siasa nchini Tanzania.

Kwa mujibu wa gazeti la TanzaniaDaima, simu ya Ben jana alitumika majira ya saa tatu asubuhi ambapo ilionekana namba yake ikijitoa kwenye makundi ya WhatsApp. Imeelezwa kuwa namba yake ilijitoa kwenye makundi mengi huku ikiwaacha na mshangao mkubwa wajumbe (members) wa makundi hayo.

Hofu ya kuwa kijana huyo hayupo hai ilichangiwa na jibu alilolitoa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa bungeni ambapo alisema, “familia ya mtajwa (Ben Saanane) aliyetangulia mbele za haki au vinginevyo, uchunguzi wa suala lake utakapokamilika, taarifa rasmi itatolewa.”

Waziri Mkuu alitoa kauli hiyo alipokuwa akijibu swali la Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe Aprili 20 mwaka huu aliyetaka kujua kwanini serikali imekuwa kimya sana kwenye suala la kupotea kwa msaidizi wake.

Namba ya Ben Saanane iliyotoka kwenye makundi ya whatsapp ni 0768078523 ambayo imesajiliwa kwa jina lake na amekuwa akiitumia kabla ya kutoweka.

Makundi ambayo namba hiyo inadaiwa kujitoa ni pamoja na Jukwaa la Siasa, Chadema Tanzania, Friends of Bavicha, Tanzania nchi yetu sote na Bantu Politics Tz Kwanza.
Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano, Uenezi na Mambo ya Nje wa CHADEMA, John Mrema alisema kuwa tukio hilo limewashtua sana kuona mtu ambaye ametoweka simu yake ikitumika kujitoa kwenye makundi ya whatsapp. Aidha, alihoji Polisi wanachukua hatua gani kujua alipo au simu yake ilipo.

Kwa upande wa familia yake, Erasto Saanane ambaye ni mdogo wake Ben alisema kuwa hawajui kama ni yeye au ni nani anatumia simu hiyo kwani hata kwenye kundi la familia amejitoa.

Ndugu huyo alisema hata rafiki zake Ben walisema kwenye makundi mengine amejiondoa pia, na kuwa Jumatano iliyopita ukurasa wake wa Facebook ulitumika ukimuonyesha yupo Tengeru, Arusha.

Aidha baada ya kuona kaka yake amejitoa kwenye makundi hayo, alitoa taarifa katika kituo cha polisi Tabata, na kuwa uchunguzi wa suala hilo umeanza.

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Hii sauti ukiisikiliza ni kama ya WEMA Sepetu na MBOWE, lakini nina mashaka na huyu mtu mmoja.

Hii audio note inayosambaa inawezekana ikawa ya Wema sepetu na Mwenyekiti Freeman Mbowe lakini bado hakuna proof yoyote, wengi wana mashaka inawezekana ni Steven ndo ameigiza sauti ya Mbowe kumchafua kwa njia moja au nyingine lakini wengine wana mashaka kwamba sauti ya wema ni ya Mtangazaji fulani hivi wa Redio ambae ameigiza sauti hiyo.

Hapa nani Mchawi ni Siasa au Kuliamsha dude kwa KIKI?
Steven inabidi akane kama sio yeye au kama vipi akili mwenyewe kama ni uzushi tu..

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Lowassa - Tumuache Rais Magufuli Afanye Kazi Yake Ipasavyo..Kama Kukosolewa Akosolewe Baadae Lakini Sio Sasa Hivi.

Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA na aliyekuwa Waziri Mkuu, Mh. Edward Lowassa amefunguka na kusema kuwa Rais Magufuli alianza vizuri kwani yapo mambo aliyoyafanya ni mazuri lakini pia yapo mambo mengine amefanya yana matatizo.
Lowassa amesema haya alipokuwa akifanya mahojiano na kusema kwa sasa tumuache Rais Magufuli aendelee na kazi yake lakini baadaye ndiyo watu waweze kumuhukumu kutokana na mambo ambayo ameyafanya.
"Rais Magufuli ameanza vizuri kubna mambo mazuri amefanya lakini kuna mambo mengine yana matatizo, lakini Mwalimu Nyerere aliwahi kusema wakati unafagia, unaweza kufagia hata shilingi sasa Rais Magufuli anafagia shilingi nyingi. Lakini tumuachie aendelee na kazi tumuhukumu baada ya kipindi fulani" alisisitiza Lowassa


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Mashabiki 400 wa Juventus Waanguka kwa Presha Turin Baada ya Timu Yao kuchakazwa Goli 4-1 na Madrid Jana.

Zaidi ya Mashabiki 400 wa Juventus wameripotiwa kuzirai baada ya timu yao kupokea kipigo cha aibu cha mabao 4-1 kutoka kwa Real Madrid jana Jumamosi.
Mashabiki mbalimbali walikusanyika maeneo mbalimbali kufuatilia mechi hiyo ikiwamo katika mgahawa wa Piazza San Carlo, nchini Italia.
Video mbalimbali zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii zilionyesha mashabiki wakiwa wamefura kwa hasira, huku wengine wakionekana kuinamisha vichwa chini.
Hali hiyo ya mashabiki kuanguka, ilielezwa ilitokana na hazira za kipigo ilichopokea timu  yao.
Kocha wa Juventus, Massimiliano Allegri baada ya mchezo aliwatuliza wachezaji na mashabiki wa klabu hiyo akisema, “Nimesikitishwa kwa kile kilichotokea kwa mashabiki wetu kule Turin. Watambue kwamba hii kilichotokea, haikuwa bahati yetu.”
Kocha huyo, alinukuliwa na Shirika la AFP akiwataka mashabiki na wachezaji wapunguze hasira kutokana na kukosa ubingwa wa Ulaya.

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Kimenukaa..Gwajima Aaanzisha Upya Vita na Makonda,Magufuli na Mmiliki wa Star Tv..Leo Amefunguka Haya Mazito Kanisani Kwake.

Leo akiongea katika kanisa la UFUFUO NA UZIMA maeneo ya Ubungo Tanesco amesema kwamba Makonda au bashite ni ziro brain na kwamba bado hana uwezo wa kuongoza watu na pia kumuomba Mh Rais Magufuli ampangie kazi nyingine.
" Professa Muhongo alipendwa na Rais Magufuli sana lakini siku ya mwisho ameondolewa, itakuwa huyu mwenye ziro brain yaani sifuri kabisa..." alisema MchungajiJosephat Gwajima.
Pia amesema hawezi kila siku kuongelea kuhusu huyu Bashite na kwamba ana shughuli nyingi za maendeleo za kuzifanya na huu mjadala wa Daudi Albert Bashite ameshaufunga sema kuna vijana wanamchokono chokonoa sana.
"..alikuwepo Kamanda Kova, Sheikh Yahaya lakini Leo wako wapi? Atakuwa huyu ziro brain kabisa yaan hamna kitu kichwani (Bashite)..." Alisema Dr Bishop Josephat Gwajima.
Pia ameenda zaidi na kutoa no ya baba yake Paul makonda ambaye ni Albert Nyange Bashite ambaye ana no ya simu iliyosajiliwa kwa jina hilo 0755543803 MPESA.
Amesema Makonda anamtukana Ruge wa Clouds na kwamba RUGE ana Degree of Marketing toka Califonia Marekani (USA) pia kitendo cha makonda kuvamia Clouds sio Uvamizi but ni igizo lakini kwa nini alienda na Askari wenye silaha katika studio za Cloids Media.
Nape ana elimu kubwa sana amesoma India diploma, degree pia na Masters amechukua Mzumbe lakini Bashite/ Makonda hana hata Cheti cha Nursery wala Certificate..
Gwajima amesema pia kwamba yeye ana PhD na kwamba Makonda sio size yake kabsa kwa sababu yeye ni ziro brain.
Amwambia Antony Diallo kwamba kwa nini alimruhusu huyu Ziro Brain ambaye alikataliwa na Media zote.
Antony Dialo amemwambia Gwajima kwamba " nilimpa nafasi Mh Paul Makonda katika kituo changu ili atoe vyeti vyake kwa maana ndo tulivyokubaliana..." in Gwajima voice
"wakati Makonda akiwa Mkuu wa wilaya ya kinondoni, majimbo yote ya Kinondoni kama Kawe, kinondoni etc yalichukuliwa na upinzani hii inamaanisha kwamba jamaa bado ni ziro brain kabsa.." in gwajima Voice


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Saturday, 3 June 2017

Sakata la Manula Kusaini Simba..Azam Watoa Tamko Hili.

Afisa Habari wa klabu ya Azam, Jaffar Iddi amefunguka na kukanusha taarifa zinazoendelea mitaani kuwa kipa namna moja wa Azam FC, Aishi Manula amesaini mkataba na klabu ya Simba na kudai kuwa mchezaji huyo bado atabaki Azam FC.
Jaffar Iddi amesema hayo leo wakati akiongea na waandishi wa Habari ambapo alikuwa akitoa picha jinsi klabu ya Azam itakavyoendeshwa sasa kwa kusema saizi wao watatoa kipaumbele zaidi kwa wachezaji wanaochipukia na kusema klabu hiyo saizi haiwezi haiwezi kutumia gharama kubwa sana kama ilivyokuwa kipindi cha nyuma katika usajili, huku akisisitiza kuwa mazungumzo ya kuwabakisha Manula na Shomari Kapombe yapo katika hutua nzuri. 
"Nisema tu kwamba Aishi Manula, Shomari Kapombe mikataba yao inakaribia kuisha lakini mazungumzo ya Aishi Manula na Shomari Kapombe yapo katika hatua za mwisho kabisa na nisema tu yanakwenda vizuri. Aishi Manula ataendelea kubaki Azam FC kilichobaki saizi tunategemea wakitoka Misri basi tukamilishe taratibu zao na ninawatoa shaka kuwa Aishi ataendelea kubaki Azam FC hata yeye wakati anakwenda Misri na timu ya taifa aliongea na waandishi wa habari akisema 
"Sitatoka Azam FC labda niende nje ya nchi nikacheze lakini kwa timu za hapa nyumbani sitaweza kufanya hivyo" kwa hiyo kauli yake inaenda na kauli ya klabu ni kweli alikuwa anazungumzwa kuwa anakwenda kwenye klabu za hapa nyumbani lakini yeye mwenyewe ameweka wazi hilo" alisema Jaffar Iddi 
Mbali na hilo Jaffar Iddi amesema kikosi cha Azam FC hakitakwenda nchi yoyote ili kupiga kambi kwa ajili ya maandalizi ya msimu mwingine wa Ligi Kuu Tanzania Bara bali wao wataweka kambi hapa hapa nchini na kudai watakuwa Chamanzi, huku akibainisha kuwa wao wataanza maandalizi ya msimu mpya mwezi wa saba.

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Gigy Aumbuka Na Tattoo Ya Bwanaa’ke.

IKIWA imepita miezi michache tangu ajiapize kuwa hatakuja kujichora tattoo ya mwanaume yeyote atakayekuwa naye katika uhusiano, muuza sura kwenye video mbalimbali za wasanii wa Bongo Fleva, Gift Stanford ‘Gigy Money’ ameumbuka baada kunaswa akiwa amejichora jina la mwandani wake, Mourad Alpha ‘Moj’.

Mwanadada huyo ambaye mara kwa mara amekuwa akiingia kwenye mgogoro na Moj kwa madai kuwa amekuwa akimpiga bila sababu za msingi hivyo anatumia nguvu kubwa kuachana naye lakini anashindwa, amejikuta akiumbuka kwa kujichora tattoo ya jina lake. Alipobanwa baada ya kunaswa na tattoo hizo, Gigy alisema;


“Haa unaniuliza, sijui hata nikujibu nini? Nguvu ya mapenzi ndiyo imenisababisha kufanya hivi, migogoro ni kawaida katika mapenzi na kupigwa kila wakati nimeshazoea.
Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Download wimbo mpya wa Timbulo unaoitwa "Ndotoni".

https://my.notjustok.com/track/download/id/225051


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

MSUVA AFUNGUKA HAYA JUU YA TIMU TATU ZA KIMATAIFA ZINAZOMUHITAJI.

Timu tatu kutoka katika nchi tatu, sasa zinataka kumsajili kiungo wa pembeni wa Yanga, Simon Msuva.
Timu hizo zinatokea katika nchi za Morocco, Misri na Afrika Kusini na Msuva amethibitisha hilo.
 
Akizungumza na Msindi, amesema tayari ofa hizo zimetua mezani Yanga na yeye ana taarifa.
 
“Nina tarifa nao na klabu inajua, hivyo ni suala la makubaliano kati yao na klabu na kati yao na mimi,” alisema.
 
Alipoulizwa katika ofa hizo tatu angependelea kwenda wapi kati ya Morocco, Misri au Afrika Kusini, alijibu.
“Hapa ni suala la ofa tu, nitaangalia timu na maslahi. Hivyo ni suala la kusubiri tu,” alisema.
 
Msuva amemaliza Ligi Kuu Bara akiwa na mabao 14 sawa na Abdulrahman Mussa na wote mwisho wameibuka wafungaji bora.

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Chuchu Afungukia Kubuma 40 Ya Mwanaye.

BAADA ya 40 ya mtoto wa mastaa wa filamu za Kibongo, Chuchu Hans na Vincent Kigosi ‘Ray’, anayejulikana kwa jina la Jaden kudaiwa kubuma, mwanamama huyo amefunguka kuwa licha ya kuchelewa bado ipo na inakuja ‘soon’. Chuchu aliongea hayo baada ya habari kuenea kuwa mastaa hao wameshindwa kumfanyia mtoto wao sherehe ya kumtoa nje ‘40’ kutokana na hali ya kifedha kuwa mbaya kwao.



“Ni kweli tumechelewa kumfanyia 40 mtoto wetu lakini ‘soon’ itafanyika tu na haya yote yanatokana na maamuzi ya baba yake ndiye aliyepanga hivyo siyo kukosa pesa kama wanavyodai, siku ya shughuli ikikaribia utasikia fununu tu,” alisema Chuchu.


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Kuna Beef Baraka The Prince na Ali Kiba? Baraka Afunguka Yote Kwanini Hawako Karibu Tena Kama Zamani.

Moja ya story ambayo iliwahi kuchukua headlines nyingi katika mitandao siku za nyuma ni kuhusu staa wa Bongofleva Baraka the Price kutokuwa karibu na staa mwingine Alikiba baada ya kuwa pamoja wakifanya shuguli za muziki.

New story leo June 2, 2017 ni kuwa Baraka the Price amefunguka na kueleza sababu za watu hao kutokuwa karibu tangu alipotoa wimbo aliomshirikisha Alikiba akisema sababu ni kuwa buys akiandaa album yake mpya.

Akiongea kwenye XXL ya Clouds FM Baraka the Prince amedai kuandaa albamu yake mpya kumemfanya awe busy huku Alikiba akiwa kwenye tour nje ya nchi:


“Ujue mimi natoa Albam mwaka huu kwa hiyo tangu mwaka umeanza nimekuwa busy natengeneza album yangu ndio maana sionekani niko karibu na Ali. Kwanza Ali amekuwa haonekani Dar es Salaam sana. Amekuwa yupo safarini na tunakuwa tunawasiliana sana kwenye simu na massage lakini ile kuonekana kama zamani ni kwa kuwa yupo kwenye kazi zake na mimi nipo kwenye kazi zangu.

“Zamani kilichokuwa kinatufanya tuwe karibu ni kwa sababu tulikuwa tufanya kazi ya kutukutanisha. Tulikuwa chini ya Rock Star kampuni moja na ikitokea suala la wasanii wa Rock Star lazima utaniona niko na Ali lakini sasa hivi nilikuwa na maandalizi ya album yangu na inakaribia kwisha.” – Baraka the Prince

Baraka The Prince haukubali wimbo wa Ben Pol, aeleza sababu

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Bodaboda Achinjwa Kinyama na Kuporwa Pikipiki.

Mwanaume mmoja (30) mkazi wa Nyankumbu wilayani Nyamagana mkoani Geita anashikiliwa na jeshi la polisi kwa kosa la mauaji ya dereva bodaboda yaliyotokea majira ya 3:00 Usiku tarehe 06.05.2017.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza ACP Zarau Mpangule amemtaja mtuhumiwa huyo kuwa ni Andrea anayedaiwa kupora pikipiki na kumuua dereva wa pikipiki Bw. Alphonce Sekagi (32) mkazi wa wilayani Sengerema wakilishirikiana na wenzake wawili kisha kutoroka na pikipiki kusikojulikana.

Taarifa zinaeleza kuwa marehemu alikuwa dereva bodaboda wa mji wa Sengerema na siku ya tukio alipakia abiria watatu kwenye pikipiki yake wakitokea Sengerema mjini kwenda kijiji cha Tabaruka na kwamba wakati wakiwa njiani abiria hao walimkata dereva huyo na kitu chenye ncha kali shingoni kisha wakamchinja kwa kutumia panga shingoni na kupelekea kupoteza maisha papo hapo.

Kamanda Mpangule amesema wananchi walitoa taarifa polisi kuhusiana na tukio hilo ambapo askari walifanya ufuatiliaji wa haraka hadi eneo la tukio na kufanya msako mkali wa kuwatafuta watuhumiwa wa mauaji hayo katika maeneo mbalimbali kwa kushirikiana na wananchi ndipo  tarehe 01.06.2017 majira ya saa 8:30 mchana wakafanikiwa kumtamata mtuhumiwa mmoja akiwa na pikipiki waliyoipora katika mauaji hayo.

Kamanda Mpangule ameendelea kwa kusema upelelezi na msako wa kuwatafuta watuhumiwa wengine wawili ambapo wanadaiwa kushiriki katika mauji hayo pamoja na uporaji unaendelea huku mtuhumiwa aliyekamatwa anafanyiwa mahojiano na uchunguzi ukikamilika atapandishwa mahakamani.


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Ukweli Mchungu..Askari wa Bunge, Wabunge wa CCM Mjipiime Upya. Hawa Wabunge wa Upinzani Tumewaagiza Sisi Walipa Kodi.

Nina maswali yananitatiza sana kichwani kwangu juu ya nani mwenye mamlaka ya kulitumikia taifa bila bughuza na kuheshimiwa mawazo yake.
Jana nilikuwa natizama bunge, nikastaajabisha kuona wabunge wa CCM kuanza kumshambulia kwa maneno mbunge wa CHADEMA Mh. John Mnyika huku wakikataa kufuta kauli zao huku wakiwa comfortable bila wasiwasi wowote.
Naona jinsi gani mbunge yule kijana mdogo kabisa anavyovunjwa moyo na wabunge wenye uwezo mdogo ambao hawakuweza kulinyasua kivyovyote taifa hili maskini kwa miaka kibao japo wapo katika chama tawala, mfano yule mbunge wa mtela ambako hali yake siyo nzuri kabisa unaweza sema ni kati ya majimbo duni kabisa hapa Tz.
Swala la pili:- Najiuliza kwanini viongozi wa bunge na wabunge wanataka bunge liwe lilelile la kukubali kila kitu na hawataki akili mpya na mawazo mapya yatolewe ili kujitathmini na kuliendeleza taifa na siyo kila siku hali kuwa ileile ya kukubali kila kitu? Nani amewaambia kwamba sisi watanzania tunavutiwa zaidi na wanachotaka wao na sio mawazo yenye kuhoji kama akina Mnyika?
Kwann viongozi wa bunge wanataka wabunge wa upinzani wawe kama watoto wakiwa ambao hawana uhalali na nchi hii na wabunge wa CCM wawe comfortable kama kwamba nchi ni yao peke yao?
Mwisho, hivi hawa walinzi wa bunge kwanini hawana staha kwa viongozi wa upinzani kusema kwamba wao wameajiliwa na CCM na hao wanaowasukuma sukuma kwa dharau siyo viongozi wao na hawatakuja kuwa viongozi wa juu kabisa wa nchi hii, askari wa bunge wajia asses upya, hawako fair hata kidogo, wanalipwa na kodi za hao wanaowasukuma kama Mbwa na siyo vingine.
Chanzo JF


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Friday, 2 June 2017

Hatimae Jeshi la Marekani Lakabidhiwa Aircraft Carrier Yake ya Kisasa Zaidi..Inauwezo wa Kukaa Miaka 50 Bila Kujazwa Mafuta.

Jeshi la majini la Marekani limekabidhiwa rasmi aircraft carrier yake ya kisasa zaidi USS Gerald R. Ford.
Jeshi hilo limesema kwamba carrier hiyo itafanyiwa majaribio mbalimbali baharini mpaka hapo 2020 ambapo itaanza kazi rasmi ndani ya jeshi hilo. 
Jeshi hilo pia limesema kwamba meli hiyo ya Gerald Ford ni ya kisasa zaidi ikiwa na mifumo mingi mipya yenye teknolojia ya juu, kubeba ndege nyingi zaidi,pia mfumo mpya wa kurusha ndege utasaidia kuongeza ufanisi wa jeshi hilo katika operesheni zake kwa zaidi ya mara tatu. 
Meli hiyo iliyokabidhiwa May 31 ilitarajiwa kua tayari September 2015,huku ikigharimu dola bilioni 12.9 badala ya dola bilioni 10.5 ikiyokadiriwa hapo awali. 
Nini kipya kwenye USS Gerald R. Ford?! 
1.Mfumo mpya wa kidijitali ambao unawezesha meli kuhudumu wafanyakaz wachache kulinganisha na carrier nyingine mfano; Nimitz 
2.Mfumo mpya na wa kisasa wa radar (Dual band radar) kuiwezesha kudetect vitisho kwa haraka na pia kwa umbali mrefu. (Mfumo huu pia unapatikana kwenye USS Zumwalt) 
3.Mfumo mpya wa kurushia ndege Electromagnetic Aircraft Launch System ambao huwezesha ndege nyingi kutumia mda mchache zaidi kuruka na kutua ukilinganisha na mifumo ya sasa
4.Uwezo wa kubeba hadi ndege 90 ikiwemo F-35C Lightning II. 
5.Radar cross section ndogo hivyo kuifanya kutokuonekana kirahisi kwenye radar za adui
6.Mifumo mipya ya kujilinda (SAMs), nk
7.Reactor mpya ya nuclear (A1B reactor) ambayo inaarifiwa kua na nguvu mara tatu zaidi ya ile inayotumika kwenye Nimitz (A4W) ambayo huzalisha megawat 190(190MW). Hivyo hii mpya ya Ford itakua na uwezo wa kuzalisha megawatts 570 (570MW).
Aircraft carrier hii inatarajiwa kutumika kwa kipindi cha miaka hamsini bila kujazwa mafuta huku ikiwa na mfumo wa Open Architecture kwa ajili ya uboreshaji zaidi huko mbeleni.


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Download wimbo mpya wa Wagosi-Wa-Kaya -Ft-Amara unaoitwa "Tonight".

https://my.notjustok.com/track/download/id/224659




Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Download wimbo mpya wa Kleyah X Mayunga unaoitwa "Boom Bye Bye".

https://my.notjustok.com/track/download/id/224653

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Download wimbo mpya wa Steve RNB unaoitwa "Dawa".

https://my.notjustok.com/track/download/id/224650



Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Fundisho kwa Serikali ya CCM. Upinzani sio Uadui.

Katika kuazimisha Siku ya Uhuru wa Kenya, Rais Kenyatta amewaalika viongozi wa upinzani kwa mazungumzo Ikulu. Hii inaonyesha katika mambo ya kitaifa wao ni wamoja na siasa haziwatenganishi undugu wao.

Hapa kwetu hata kwenda kwenye harusi ya mpinzani taarifa zako zinachunguzwa maana unahisiwa kuwa ni msaliti. Tujifunze kutoka Kenya ambako tumekuwa tunawatolea mifano mibaya kumbe wao ndio wako vizuri kuliko sisi.

Leo mtu kuwa Chadema kesho ccm au ccm kesho Chadema au CUF lionekane ni jambo la kawaida muhimu utetezi kwa nchi tuu. Maana ndani ya nchi wapo ndugu na jamaa zako watakuwa katika vyama tofauti na chako.


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Hii Ndio App Pekee Iliyopo Kwenye Simu Anayotumia Rais wa Marekini Donald Trump.

Watu wengi wanaotaka kununua simu janja/Sikanu (Smartphone), mojawapo ya jambo wanaloangalia pindi wafanyapo uchaguzi wa simu ni ukubwa wa uhifadhi wa ndani (storage).

Sababu kubwa ya kufanya hivyo ni kupata wasaa wa kusanidi (Install) App nyingi zaidi kadri iwezekanavyo, lakini hilo ni tofauti sana kwa Rais wa Marekani Donald Trump.

Kwa mujibu wa ripoti mpya imeelezwa Simu binafsi ya Rais wa Donald Trump imesanidiwa (Installed) App moja tu.

Mwandishi wa habari za kisiasa na mhariri wa AXIOS Media, Mike Allen, anasema Rais Trump anatumia simu ya iPhone na kwamba simu yake imewekwa App ya Twitter tu.

Sababu ya kufanya hivyo na kumuwekea App hiyo ni kupunguza hatari ya uwezekano wa simu yake kudukuliwa. Aidha pia kumpunguzia muda wa matumizi ya simu na ili ajielekeze zaidi katika mambo ya kio�si zaidi.

Muda mwingi hutumia kuangalia TV ili kujua matukio yanayoendelea duniani.

Simu ya awali ambayo alizuiwa kuitumia baada ya kuwa Rais ilikuwa ni Samsung. Alibadili kutoka Android kwenda iOS mwezi Machi mwaka huu.

Mpaka anaapishwa kuwa Rais wa Marekani inaelezwa simu aliyokuwa anatumia ni Samsung Galaxy S3 ambayo ilitolewa mwaka 2012.

Rais aliyepita Baraka Obama alisema wakati wa kuingia madarakani kwamba anatumia BlackBerry na matumizi yake yalikuwa ni kutuma ujumbe, kupiga picha na kusikiliza Muziki.

Chanzo: Teknokona


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Download wimbo mpya wa G Nako WARA WARA unaoitwa "LUCKY ME".

https://my.notjustok.com/track/download/id/223037




Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Download wimbo mpya wa Wagosi Wa Kaya unaoitwa "Upepo Sio".

https://my.notjustok.com/track/download/id/223035


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Download wimbo mpya wa Kriticos ft Harmorapa & Ronei unaoitwa "Kideo".



Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

#Breaking News>>>>Wabunge wa Upinzani Wasusia Bunge na Kutoka Nje...Kisa John Mnyika.

Mbunge John Mnyika atolewa nje ya Bunge kwa amri ya Spika Job Ndugai na kuamriwa kutohudhuria vikao kwa siku 7 baada ya kutokea malumbano leo.

Kufuatilia tukio hilo Wabunge wa Upinzani wametoka nje baada ya Mbunge huyo kutolewa nje na Askari wa Bunge kwa amri ya Spika.

Vilevile, Mamlaka ya Bunge kupitia Kamati ya Maadili kumjadili Mbunge Esther Bulaya kwa kuhamasisha wabunge kutoka nje ukumbi wa Bunge


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Mwanasheria Aomba Mahakama Uganda Iruhusu Kaburi la Ivan Don Kufukuliwa.

Mwanasheria Tugume Gideon ameiomba Mahakama Kuu ya Uganda iruhusu kaburi la Ivan Semwanga lifukuliwe ili watoe fedha zilizomwagwa ndani akidai kuwa ni kunyume cha Sheria


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Yanga Wamemfanya nini Hamis Tambwe...Mwenye Afunguka Haya Kwa Uchungu Akiwa Kwao Burundi.

STRAIKA wa Yanga, Amissi Tambwe, huenda msimu ujao asionekane katika kiko­si cha timu hiyo kutokana na kutojua hatima yake ndani ya klabu hiyo mpaka sasa.

Tambwe ambaye ameon­goza Yanga kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara mara tatu mfululizo tangu alipojiunga nayo msimu wa 2014/15 akitokea Simba, ame­liambia Championi Ijumaa kuwa kwa jinsi mambo yanavyoenda inawezekana asiitumike timu hiyo msimu ujao.

Alidai kuwa mpaka sasa hakuna chochote kina­choendelea kati yake na uongozi, hivyo kama hali hiyo itaendelea mpaka mwezi Julai, basi ata­chukua uamuzi wa kwen­da kutafuta maisha sehe­mu nyingine katika timu ambazo zimeonyesha nia ya kutaka kusajili za hapa nchini na nje ya nchi.

Kwa sasa Tambwe amei­fungia Yanga mabao 46 katika michuano ya ligi kuu tangu alipojiunga nayo, yupo kwao nchini Burundi kwa ajili ya mapumziko na hajui lini atarejea nchini.


“Kwa hiyo, kutokana na hali hiyo sijui nitarejea lini nchini, lakini ninachoweza kusema ni kwamba bado ninaipenda Yanga na ndiyo maana nimeamua kusitisha mipango yangu mingine mpaka niwasikilize wao kwanza.

“Lakini wakiendelea kuwa kimya mpaka Julai basi ni­tachukua uamuzi mwingine kwa sababu soka ndiyo kazi yangu, naweza kujiunga na timu yoyote hapo nchini au nje ya nchi ambazo tangu zamani zimekuwa zikinihi­taji,” alisema Tambwe am­baye mkataba wake na Yan­ga tayari umeshamalizika.

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa