Friday, 2 June 2017

Hii Ndio App Pekee Iliyopo Kwenye Simu Anayotumia Rais wa Marekini Donald Trump.

Watu wengi wanaotaka kununua simu janja/Sikanu (Smartphone), mojawapo ya jambo wanaloangalia pindi wafanyapo uchaguzi wa simu ni ukubwa wa uhifadhi wa ndani (storage).

Sababu kubwa ya kufanya hivyo ni kupata wasaa wa kusanidi (Install) App nyingi zaidi kadri iwezekanavyo, lakini hilo ni tofauti sana kwa Rais wa Marekani Donald Trump.

Kwa mujibu wa ripoti mpya imeelezwa Simu binafsi ya Rais wa Donald Trump imesanidiwa (Installed) App moja tu.

Mwandishi wa habari za kisiasa na mhariri wa AXIOS Media, Mike Allen, anasema Rais Trump anatumia simu ya iPhone na kwamba simu yake imewekwa App ya Twitter tu.

Sababu ya kufanya hivyo na kumuwekea App hiyo ni kupunguza hatari ya uwezekano wa simu yake kudukuliwa. Aidha pia kumpunguzia muda wa matumizi ya simu na ili ajielekeze zaidi katika mambo ya kio�si zaidi.

Muda mwingi hutumia kuangalia TV ili kujua matukio yanayoendelea duniani.

Simu ya awali ambayo alizuiwa kuitumia baada ya kuwa Rais ilikuwa ni Samsung. Alibadili kutoka Android kwenda iOS mwezi Machi mwaka huu.

Mpaka anaapishwa kuwa Rais wa Marekani inaelezwa simu aliyokuwa anatumia ni Samsung Galaxy S3 ambayo ilitolewa mwaka 2012.

Rais aliyepita Baraka Obama alisema wakati wa kuingia madarakani kwamba anatumia BlackBerry na matumizi yake yalikuwa ni kutuma ujumbe, kupiga picha na kusikiliza Muziki.

Chanzo: Teknokona


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

0 comments:

Post a Comment