Jeshi la majini la Marekani limekabidhiwa rasmi aircraft carrier yake ya kisasa zaidi USS Gerald R. Ford.
Jeshi hilo limesema kwamba carrier hiyo itafanyiwa majaribio mbalimbali
baharini mpaka hapo 2020 ambapo itaanza kazi rasmi ndani ya jeshi hilo.
Jeshi hilo pia limesema kwamba meli hiyo ya Gerald Ford ni ya kisasa
zaidi ikiwa na mifumo mingi mipya yenye teknolojia ya juu, kubeba ndege
nyingi zaidi,pia mfumo mpya wa kurusha ndege utasaidia kuongeza ufanisi
wa jeshi hilo katika operesheni zake kwa zaidi ya mara tatu.
Meli hiyo iliyokabidhiwa May 31 ilitarajiwa kua tayari September
2015,huku ikigharimu dola bilioni 12.9 badala ya dola bilioni 10.5
ikiyokadiriwa hapo awali.
Nini kipya kwenye USS Gerald R. Ford?!
1.Mfumo mpya wa kidijitali ambao unawezesha meli kuhudumu wafanyakaz wachache kulinganisha na carrier nyingine mfano; Nimitz
2.Mfumo mpya na wa kisasa wa radar (Dual band radar) kuiwezesha kudetect
vitisho kwa haraka na pia kwa umbali mrefu. (Mfumo huu pia unapatikana
kwenye USS Zumwalt)
3.Mfumo mpya wa kurushia ndege Electromagnetic Aircraft Launch System
ambao huwezesha ndege nyingi kutumia mda mchache zaidi kuruka na kutua
ukilinganisha na mifumo ya sasa
4.Uwezo wa kubeba hadi ndege 90 ikiwemo F-35C Lightning II.
5.Radar cross section ndogo hivyo kuifanya kutokuonekana kirahisi kwenye radar za adui
6.Mifumo mipya ya kujilinda (SAMs), nk
7.Reactor mpya ya nuclear (A1B reactor) ambayo inaarifiwa kua na nguvu
mara tatu zaidi ya ile inayotumika kwenye Nimitz (A4W) ambayo huzalisha
megawat 190(190MW). Hivyo hii mpya ya Ford itakua na uwezo wa kuzalisha
megawatts 570 (570MW).
Aircraft carrier hii inatarajiwa kutumika kwa kipindi cha miaka hamsini
bila kujazwa mafuta huku ikiwa na mfumo wa Open Architecture kwa ajili
ya uboreshaji zaidi huko mbeleni.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment