Nina maswali yananitatiza sana kichwani kwangu juu ya nani mwenye
mamlaka ya kulitumikia taifa bila bughuza na kuheshimiwa mawazo yake.
Jana nilikuwa natizama bunge, nikastaajabisha kuona wabunge wa CCM
kuanza kumshambulia kwa maneno mbunge wa CHADEMA Mh. John Mnyika huku
wakikataa kufuta kauli zao huku wakiwa comfortable bila wasiwasi wowote.
Naona jinsi gani mbunge yule kijana mdogo kabisa anavyovunjwa moyo na
wabunge wenye uwezo mdogo ambao hawakuweza kulinyasua kivyovyote taifa
hili maskini kwa miaka kibao japo wapo katika chama tawala, mfano yule
mbunge wa mtela ambako hali yake siyo nzuri kabisa unaweza sema ni kati
ya majimbo duni kabisa hapa Tz.
Swala la pili:- Najiuliza kwanini viongozi wa bunge na wabunge wanataka
bunge liwe lilelile la kukubali kila kitu na hawataki akili mpya na
mawazo mapya yatolewe ili kujitathmini na kuliendeleza taifa na siyo
kila siku hali kuwa ileile ya kukubali kila kitu? Nani amewaambia kwamba
sisi watanzania tunavutiwa zaidi na wanachotaka wao na sio mawazo yenye
kuhoji kama akina Mnyika?
Kwann viongozi wa bunge wanataka wabunge wa upinzani wawe kama watoto
wakiwa ambao hawana uhalali na nchi hii na wabunge wa CCM wawe
comfortable kama kwamba nchi ni yao peke yao?
Mwisho, hivi hawa walinzi wa bunge kwanini hawana staha kwa viongozi wa
upinzani kusema kwamba wao wameajiliwa na CCM na hao wanaowasukuma
sukuma kwa dharau siyo viongozi wao na hawatakuja kuwa viongozi wa juu
kabisa wa nchi hii, askari wa bunge wajia asses upya, hawako fair hata
kidogo, wanalipwa na kodi za hao wanaowasukuma kama Mbwa na siyo
vingine.
Chanzo JF
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment