Tuesday, 13 February 2018

Simba, Yanga Kumaliza Vipolo Vyao Kabla ya Kusafiri kwa Mechi za Kimataifa.

Vinara wa ligi kuu soka Tanzania Bara Simba SC iliyopo kileleni mwa msimamo na mabingwa watetezi Yanga SC iliyopo nafasi ya pili zinatarajiwa kucheza mechi zao za viporo za VPL kabla ya kusafiri kwa mechi za kimataifa.


Yanga ambayo haikucheza mchezo wake wa raundi ya 18 kutokana na wikiendi ililiyopita kucheza mchezo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya St. Lousi ya Shelisheli, itaikaribisha Majimaji FC kwenye uwanja wa Uhuru.

Simba wao hawakucheza mchezo wao wa raundi ya 18 kutokana na kuiwakilisha nchi kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika ambapo walicheza na Gendarmerie ya Djibouti. Alhamisi watakuwa mjini Shinyanga kucheza na Mwadui FC.

Tayari Yanga wameshaweka wazi kuwa watasafiri siku ya Jumapili Februari 18 kuelekea Shelisheli kwaajili ya mchezo wa marudiano utakaopigwa Februari 21. Simba bado hawajatangaza lini wataondoka nchini.

Simba wanaongoza ligi wakiwa na alama 41 huku wapinzani wao wa Alhamisi Mwadui wakiwa katika nafasi ya 12 na alama 18. Yanga ina alama 34 katika nafasi ya tatu huku Majimaji wakiwa nafasi ya 14 na alama 14.

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Siku ya Leo.

Bonyeza Links zifuatazo:

10 Job Opportunities at Tanzania Civil Aviation Authority (TCAA)

Job Opportunity at TAZAMA Pipelines Limited, Security Officer

Job Opportunity at Tanzania Forest Conservation Group (TFCG), Capacity Building Officer

Job Opportunity at Jhpiego, Senior Health Informatics Advisor

Job Opportunity at Capital Markets And Securities Authority (CMSA)

Call For Interview-State House (BSAAT)

Job Opportunity at Pyrethrum Company of Tanzania Ltd, Purchasing Engineer

Nafasi zingine ingia www.ajirayako.co.tz

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Huu Hapa Ujumbe wa Zari Baada ya Picha za Hamisa Mobetto na Videographer wa Diamond Kusambaa.

Baada ya muimbaji wa Bongofleva Diamond Platnumz na mzazi mwenzake Hamisa Mobetto kufikishana Mahakamani wiki iliyopita inadaiwa kuwa mambo yao yapo sawa kwa sasa na wamemaliza tofauti zao, hiyo ni baada ya kusambaa kwa picha za official videographer wa Diamond Platnumz ambaye ni Lukamba kusambaa kwa picha mtandaoni akiwa na Hamisa.

Kitendo cha Lukamba kuonekana kumfanyia photoshoot Hamisa kimeanza kuhusishwa kuwa Diamond na Hamisa wapo sawa kwa sasa ndio maana Lukamba ameonekana akifanya kazi za Hamisa ambaye ni mzazi mwenza na boss wake Diamond Platnumz.

Baada ya muda kupita baada ya picha ya Hamisa na Lukamba kusambaa mtandaoni Zari alipost ujumbe huu kupitia ukurasa wake wa instagram story na kuandika “Nafukuzana na pesa sio binadamu” ujumbe ambao unadaiwa kuwa amepost baada ya kuona picha ya Lukamba na Hamisa wakiwa pamoja kitu ambacho kinadaiwa kuzidi kuyumbisha penzi na Zari na Diamond na indaiwa kuwa bado hawapo sawa kwa sasa.


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Jacob Zuma Amepewa Saa 48 Awe Amejiuzulu.

Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma amepewa saa 48 awe amejiuzulu, katika nafasi hiyo.

Hatua hiyo inakuja baada ya mazungumzo yaliyofanywa na chama tawala cha nchini, ANC kwa muda.

Taarifa zinaeleza kuwa ANC walituma watu wawili nyumbani kwa Rais Zuma, Pretoria kumfikishia ujumbe wa chama kwamba anatakiwa ajiuzulu mwenyewe au chama kimng’oe madarakani.

Hatua hii ya ANC inaonekana ndio njia rahisi zaidi ya chama hicho kumng’oa Rais Zuma madarakani badala ya kusubiri utaratibu wa bunge ambao ungeweza kuwa mrefu na wenye madhara zaidi kwa chama cha ANC.

Kiongozi wa ANC, Cyril Ramaphosa anaongoza shinikizo za kumuondoa Zuma katika nafasi yake hiyo ya Urais, na hatimaye kushika pia nafasi hiyo. 

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Karani Adai Nyoka Alikula Mamilioni ya Pesa.

Karani mmoja nchini Nigeria amefukuzwa kazi baada ya kuwaambia wakaguzi wa hesabu kuwa nyoka alikula naira milioni 36.

Pesa hizo ni sawa na dola 100,000 za kimarekani.

Karani Philomena Chieshe alikuwa akifanya kazi katika ofisi ya bodi ya mtihani ya Nigeria inayokusanya pesa za mtihani.

Bodi hiyo ya mtihania iliiambia BBC kuwa ilitupilia mbali madai yake na imeanisha kumchukulia hatua za kinidhamu.,

Kisa hicho kimezua shutuma na dhihaka kwenye mitandao ya kijamio nchini Nigeria.

Nayo tume ya kupambana na rushwa nchini Nigeria iliandika ujumbe huu katika Twitter ambayo nembo yake ni mwewe.

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Thursday, 8 February 2018

Tundu Lissu Amuumbua Lemutuz Baada ya Kudai ni Rafiki yake " Lemutuz Asilazimishe Urafiki".

Baada ya Lemutuz kuandika katika ukurasa wake kuwa Tundu Lissu alikuwa rafiki yake mkubwa...Tundu Lissu amefunguka na kudai Lemutuz asilazimishe urafiki ambao haukuwepo...

Jisomee Hapa chini:
_

From @tundulissutz - LEMUTUZ ASILAZIMISHE URAFIKI USIOKUWEPO!!! .

Leo nimeonyeshwa post iliyopo kwenye Instagram account ya William Malecela aka Lemutuz.

Kwenye post yake, Lemutuz amedai kwamba mimi ni rafiki yake mkubwa na wa miaka mingi, kabla vijana wengi wanaopiga makelele mitandaoni hawajazaliwa.

Lemutuz ameeleza kwamba mwaka 2010 alinipokea Uwanja wa Ndege wa John F. Kennedy, mjini New York, nilipoenda kwenye mahafali ya dada yangu. .

Amewaambia wasomaji wake kwamba alinichukua kwenye gari yake binafsi kutoka JFK hadi Connecticut kwenye graduation ya dada yangu aliyodai ilikuwa Connecticut State University. .

Ili kuthibitisha kauli zake, Lemutuz ameambatanisha picha niliyopiga naye, ambayo nitaielezea shortly. .

Naomba kuweka ukweli wa kauli za Lemutuz wazi ili kuweka rekodi sawa.

Kwanza, nimemfahamu Lemutuz tangu mwezi Mei, 2011. Nilikutana naye mara ya kwanza kwenye mahafali ya mdogo wangu kaka (sio dada) Vincent Mughwai, aliyekuwa anasoma Bridgeport University (sio Connecticut State University). Kama nakumbuka vizuri, Lemutuz alikuwa MC kwenye shughuli hiyo. Na siku hiyo kulikuwa na Watanzania wengine wengi waishio Marekani. .

Lemutuz hakunipokea mimi JFK wala kunipeleka Bridgeport, Connecticut, kwenye gari yake binafsi. Hatukuwa tunafahamiana kabla ya kukutana kwenye graduation ya kaka Vince, siku kadhaa baada ya mimi, mke wangu na ndugu zangu wengine kuwasili Marekani. .

Pili, ni kweli tulipiga picha ambayo ameitoa kama uthibitisho wa 'urafiki' wetu. Siku hiyo, kama ilivyo kwenye shughuli kama hizo, nilipiga picha na Watanzania karibu wote waliohudhuria graduation hiyo...

Kama Lemutuz, wengi wa niliyopiga nao picha nilikuwa siwafahamu kabisa kabla ya kukutana nao siku hiyo. .

Tatu, tangu siku hiyo sijawahi kufanya mawasiliano na Lemutuz ya aina yoyote. Nakumbuka tu kukutana na kusalimiana nae bungeni mwaka 2012, wakati alipokuja Dodoma akitaka kugombea ubunge wa Afrika Mashariki. .

Mimi sijajua sababu ya Lemutuz kutaka kulazimisha urafiki na mimi usiokuwepo. Yeye ni rafiki mkubwa wa Bashite na mpiga debe wa Rais Magufuli. .

Mimi ni mpinzani mkubwa wa Magufuli na nimelipa gharama kubwa kwa sababu ya msimamo wangu tangu Magufuli aingie madarakani. .

Huo 'urafiki mkubwa' unaodaiwa kuweka kati yangu na Lemutuz msingi wake ni nini???
.

Mwisho, ukitaka kuongopa hadharani basi angalau uwe na kumbu kumbu sahihi. Lemutuz anadai tulikutana 2010 wakati ilikuwa Mei 2011. .

Anadai nilikwenda kwenye graduation ya dada yangu (ambaye hata jina hakumtaja!) wakati ilikuwa graduation ya kaka yangu Vincent Mughwai. .

Anadanganya ilikuwa Connecticut State University wakati ilikuwa Bridgeport University. Anadai alinipokea JFK wakati nilipokelewa na kaka yangu Vincent. .

Na tangu nimepigwa risasi na kujeruhiwa vibaya na wanaoitwa 'watu wasiojulikana', rafiki yangu mkubwa huyu hajawahi kunitumia hata kadi ya pole!!! .

Huu ni urafiki feki wa kuwadanganyia Watanzania wasioelewa. .

Msidanganyike!!!

By Tundu Lissu

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Wema Sepetu na Diamond Watinga Mahakamani Kisutu.

KISUTU: Msanii Wema Sepetu leo amefika Mahakamani kufuatilia kesi yake ya kukutwa na msokoto wa Dawa za Kulevya aina ya Bangi

Wema amefika Mahakamani hapo akiwa na Wakili Albert Msando aliyetangaza kumtetea baada ya Wakili Peter Kibatala kujitoa kumtetea msanii huyo
Wakati huo huo, Msanii wa Muziki nchini, Naseeb Abdul(Diamond Platnumz) naye amefika Mahakamani hapo na Mzazi mwenzake Hamisa Mobetto kwa ajili ya kusikiliza shauri lao la matunzo ya mtoto

Shauri hilo la matunzo ya mtoto lilifunguliwa na Hamisa Mobetto akiomba Mahakama iamuru Diamond kutoa matunzo ya mtoto kila mwezi
Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Hoteli ya Hyatt Regency Yatangaza Chumba cha Milioni 22..4 kwa Usiku Mmoja tu wa Valentine, Wabongo Waduwaa.

Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam juzi ilitangaza ofa ya chumba cha Sh22.4 milioni katika Usiku wa Valentine na kusema kuwa Watanzania mbalimbali wamekuwa wakipiga simu kutaka kujua kama ni bei halisi na wengine kuomba punguzo.


Hayo yalisemwa na Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo, Denis Glibic alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana kuhusu chumba hicho na namna watu walivyolipokea tangazo hilo.


Glibic alisema tangu watangaze ofa hiyo ambayo ni kwa ajili ya wapendano katika sikukuu ya Valentine, wamepokea simu nyingi kutoka kwa Watanzania wakitaka kujua kama kweli hilo ni tangazo lao halisi na wengine wakitaka wapate nafasi hiyo kwa punguzo la bei. 


Kuhusu chumba hicho ambacho kinatumiwa na marais mbalimbali duniani wanapokuja nchini, meneja mwendeshaji wa hoteli hiyo, Timothy Mlay alisema, kwa kawaida bei yake huwa ni Sh11.4 milioni kwa siku.


Alisema pamoja na kuwapo kwa malalamiko ya maisha magumu, wanaamini watu watapatikana kwani kwao kuanzia Desemba mpaka sasa ni kipindi ambacho hupata wateja wengi.


Alisema huduma zitakazotolewa kwa wateja wa chumba hicho siku hiyo zitakuwa tofauti kwa wateja wengine, kwani mbali ya kwenda kuchukuliwa na gari la kifahari eneo wanaloishi, pia watapatiwa zawadi za mapambo ya mwilini yenye madini ya Tanzanite

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Majibu ya Serikali Kuhusu Zile Milioni 50 Ilizoahidi Kwa Kila Kijiji

Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dk. Hassan Abbasi amesema kuwa serikali itaweka utaratibu utakaowezesha kutekelezwa kwa ahadi ya kutolewa milioni 50 kila kijiji, hivyo wananchi wasiwe na hofu.


Dkt Abbasi aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu masuala mbalimbali na miradi inayotekelezwa na serikali, na kuweka bayana kwamba, tayari mambo makubwa zaidi yameshafanyika, na hivyo hilo la milioni 50 kila kijiji litatekelzwa pia.


Majibu hayo aliyatoa baada ya mmoja wa waandishi wa habari kuulizwa swali, baada ya kuona ni mwaka wa tatu sasa tangu Rais Dkt Magufuli alipoingia madarakani, lakini ahadi yake ya kutoa TZS milioni 50 kila kijiji kwa ajili ya kuwasaidia kina mama na vijana kujikwamua kiuchumi haijatekelezwa.


“… 50 nyenyewe tutaweka utaratibu itakuja tu ikifika. Lakini maji si yanakuja bana, dawa si zipo, barabara si zipo, sasa kama wewe ulitaka ile 50 ili upige dili, tulia kwanza.”


Aidha, Dkt Abbasi amesema kwamba, ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) haikusema ni lini ahadi hiyo itatekelezwa, kama ni 2017 au 2018, hivyo akawataka wananchi kuwa na subira, pindi utaratibu ukikamilika watapatiwa fedha hizo.


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Sunday, 4 February 2018

Mzee Kingunge Kuzikwa Leo Hii Hapa Ratiba ya Mazishi.

RATIBA  ya mazishi ya aliyekuwa mwanasiasa mkongwe, Kingunge Ngombale Mwiru, iliyotolewa na familia yake jana inaonyesha atazikwa leo Jumatatu katika shughuli itakayoanza saa 9:30 hadi 11:30 katika makaburi ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam.

Taarifa hiyo iliyotolewa na mwenyekiti wa kamati maalum ya shughuli hiyo, Omary Kimbau, inaonyesha kwamba mwili wa marehemu utatolewa leo saa 10 jioni Hospitali ya Muhimbili na kupelekwa nyumbani kwake Victoria/Makumbusho ambako ibada na mila zitafanywa usiku mzima.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, shughuli zitakazofanywa kesho ni kama ifuatavyo:



Jumatatu tarehe 5/2/2018
– Saa 1:00 asubuhi mpaka saa 2:00 asubuhi waombolezaji kuwasili nyumbani kwa ajili ya kuanza taratibu za mazishi.
– Saa 2:00 asubuhi mpaka saa 3:30 asubuhi kupata kifungua kinywa
– Saa 4:00 asubuhi mpaka saa 5:00 misa nyumbani kwa marehemu
– Saa 6:00 mwili kuwasili Karimjee Hall  kuagwa
– Saa 6:00 mchana 9;00 kuaga mwili wa marehemu
– Saa 9:00 alasiri mpaka 9:30 kuelekea makaburini Kinondoni
– Saa 9:30 mpaka 11:30 maziko
– Saa 11:30 jioni 12:30 kuelekea nyumbani kwa chakula cha jioni
1:30 usiku mpaka. 2:45 chakula cha usiku waombolezaji wote
3:00 usiku- waombolezaji wote hitimisho la shughuli nzima

Kingunge Ngombale-Mwiru alifariki Ijumaa wiki hii katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alikokuwa amelazwa akitibiwa majeraha baada ya kuumwa na mbwa wake.

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Mke wa Mzee Majuto: Namuombea Sana Mume Wangu Apone Maana Ndiye Furaha Yangu.

MKE wa mchekeshaji maarufu Bongo, Amri Athuman ‘Majuto’, Aisha Yusuf amesema kuwa siku za hivi karibuni alipoanza kuugua tena mumewe amekuwa akikesha na kumuombea arudi katika hali ya kawaida kwani anapoumwa vitu vyote vinalala.

Akichonga na gazeti hili mke huyo alisema mume wake ni mcheshi sana na ni mtu anayeifanya familia kuwa na furaha kila wakati sasa anapokuwa mgonjwa nyumba inakuwa haina amani kabisa na hata watoto ambao amezoea kucheza nao wanapoa.

“Kila siku dua zangu ni kwa mume wangu maana ndiyo nguzo katika familia yetu na ni mtu mcheshi sana kwa familia hivyo namuombea sana apone maana ndiye furaha yangu,“ alisema mke wa Majuto.


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Wastara Aondoka India kwa Matibabu Amwaga Chozi Airport Wakati Akiondoka.

Muigizaji wa filamu nchini Tanzania, Wastara ameondoka nchini kuelekea India kwa ajili ya matibabu ya mguu wake ulioanza kumsumbua mwishoni mwa mwaka jana huku akiwashukuru watanazania na Vyombo vya Habari kwa kuwa pamoja naye kipindi alivyokuwa akihitaji msaada wa fedha.

Wastara akiongea na waandishi wa Habari mapema leo Jumapili Februari 4, 2018 katika Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam, amesema “nina washukuru sana vyombo vya habari wote kwa moyo wa upendo walionesha kwa sababu bila ya wao hata mimi nisingekuwa Wastara. Napenda kuwaambia watanzania kwamba tuamini sana maneno anayosema mtu kuliko neno analosema mtu mwingine kwa hiyo naamini kuna wengine watakuja na matatizo tujaribu kuwaangalia nawao pia”.

Na alipoulizwa kuhusu tuhuma za kutumia fedha za matibabu kwa starehe kama alivyowahi kuchangiwa kipindi cha nyuma na kwenda Dubai, Wastara amesema hajawahi kuchangiwa na Watanzania bali alisaidiwa Makamu wa Rais na hakutumia kwa matumizi mengine.

“Kwanza niseme sijawahi kuchangiwa na Watanzania mimi kama mimi, mara ya kwanza nilipoumwa aliyenichangia asilimia kubwa alikuwa ni Makamu wa Rais, na uzuri ni kwamba mpaka nafika hospitalini nilikuwa nampigia simu. Kilichosababisha watu waseme baada ya kufika hospitali kama hivi ninavyokwambia wiki tatu linapotokea tatizo kama umefanyiwa Oparesheni au upasuaji wowote niliambiwa unauwezo wa kukaa au kuishi kwenye hoteli karibu na hospitali..Ndipo watu wa karibu yangu wa Oman wakawa wamenipa Visa nikaenda kukaa huko kwa muda.“ameongea Wastara.

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Baunsa wa Diamond Amwagiwa Maji Jukwaani na suti zake Kaeleza Alivyojisikia.

Baunsa maarufu anaye mlinda msanii Diamond, Mwarabu leo ilikuwa ni siku yake ya kuzaliwa ambapo Harmonize alimuita kwenye stage na kisha kumwagia maji na kumuimbia wimbo wa Happy Birthday, Bonyeza play kutazama ilivyokuwa..

VIDEO:


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Friday, 2 February 2018

Hatari Tupu! Huu Hapa Uamuzi Alioufanya Zari kwa Diamond.

Saa chache zimepita toka msanii Diamond Platnumz kudaiwa kutoka kimapenzi na wasichana wengine tofauti na mama watoto wake Zari the bosslady.

Inasemekana kuwa Diamond Platnumz hupeleka wasichana tofautitofauti nyumbani kwake Madale, kutokana na tetesi zilizokuwa zikiendelea kwenye mitandao ya kijamii ikaonekana Zari kukasirishwa na tabia hiyo.

Hivyo kupitia instagram account ya Zari ameonekana kumu’unfollow baba watoto wake Diamond Platnumz, kitu hiki kimeleta maswali mengi kwa baadhi ya mashabiki na wengi kuhusisha ukaribu uliotokea kati ya Wema Sepetu na Diamond siku ya uzinduzi wa kutambulisha rasmi Marombosso WCB.

Zari amwambia Mama Diamond “Tuhame Guest House tumwachie mwanao” 

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

TANZIA: Mzee Kingunge Ngombale Mwiru Afariki Dunia.

Mzee Kingunge Ngombale–Mwiru amefariki dunia alfajiri ya leo.

Tupo hapa na masikitiko makubwa.

Poleni sana sana wafiwa na kijana wake Kinje (Mama yake alifariki 4/1/2018 na Baba yake leo)

May his soul Rest in Eternal Peace.

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Thursday, 1 February 2018

Wema Sepetu Kuja Kivingine.

Malkia wa filamu nchini Tanzania, Wema Sepetu baada ya kufungua App yake sasa anakuja na kitu kingine ambacho bado kipo kwenye mabano hadi ifikapo Juni 30, 2018.


Muigizaji huyo amekuwa aliwaomba mashabiki wake kuitunza tarehe hiyo na kuikumbuka ili kufahamu kiundani ujio wa siku hiyo

Ujumbe huo ametuma Kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Diamond Platinumz aendelea kudhirisha ushikaji wake na mlimbwende Wema Sepetu kwa kumsapoti katika hili kwa kuposti kwenye ukurasa wake na kuandika ”Save the date” huku Wema akimjibu You are the Best”.

Ni kweli bado haijawekwa wazi nini hasa kina kuja, kwani tunavyojua Wema Sepetu ni mwanamke aliyejikita katika shughuli mbalimbali katika jamii.

Hivyo kaa tayari.

Kupitia ukurasa wake wa Instagrama Wema Sepetu ameandika,

Just save the date,

wiki,week 21

siku/day 151


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Kampuni ya TTCL Yafutwa.

Akizungumza na waandishi wa habari, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Makame Mbarawa, amesema kuwa anamshukuru sana Rais Magufuli kwa kuona umuhimu wa kuona wa kuwa na shirika la mawasiliano madhubuti kwa ajili ya kuleta maslahi mapana ya nchi, huku akitoa shukrani pia kwa Wabunge wote kwa kukubali kupitisha muswada huo.

Aidha Prof Mbarawa, amesema uwepo wa sheria ya shirika la mawasiliano unatoa fursa ya kuboresha sekta kwa kuweka mazingira mazuri ya usimamizi wa miundombinu ya mikakati chini ya shirika hilo.

Profesa Mbarawa pia amewajulisha Watanzania wote kuwa mabadiliko ya kuhama kutoka kampuni kuwa shirika la mawasiliano hayatawaathiri kwa namna ya utoaji wa huduma mbalimbali ambazo zilikuwa zinatolewa na kampuni ya simu ya (TTCL) huku akielezwa kuwa wanaodaiwa na iliyokuwa kampuni hiyo watatakiwa kulia madeni yao kama mikataba yao inavyosema na wanaoidai watalipwa pia.

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Polisi Wakamata Machungwa Yaliyoibiwa.

Polisi wa huko jijini Seville nchini Hispania wakamata watu watano jana baada ya kufukuzana nao kwa kasi na ndipo hapo polisi waligundua tani hizo za machungwa zilizoibiwa ambazo watuhumiwa walikuwa wameyajaza ndani ya magari.

polisi walipatwa na shaka wakati walipoona magari matatu yakikunja kona ya haraka kutokana na Ripoti ya Europa Press. Baada ya kukimbizana nao, polisi waliweza kusimamisha magari mawili. Walipofungua mlango wa nyuma wa gari mamia ya machungwa yalidondoka chini.

Machungwa hayo yalirudishwa katika mji wa Carmona, ambayo ndiyo mji uliotoa ripoti za wizi masaa machache tu kabla ya tukio hilo.

Polisi walisema kuwa karibu poundi 9,000 za matunda yalipatikana na uchunguzi wa wizi unaendelea.

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Download wimbo wa Manfongo unaitwa Lau Nafasi.

https://my.notjustok.com/track/download/id/313582


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

"Nyumba Yangu ina vyumba Viwili Nimenunua Milioni 100" Lulu Diva.

Msanii LuluDiva ambaye ameachia wimbo mpya hivi karibuni kaelezea gharama za video hiyo ambayo amesema kuwa sichini ya millioni 15 lakini pamoja na Hilo kaelezea mjengo wake mpya ambao anadai kanunua millioni 100 na kaukarabati upya.

VIDEO:

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Download wimbo wa Snura Ft Aslay unaoitwa "Moyo Niache".


https://my.notjustok.com/track/download/id/313585


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Download wimbo wa vanessa-mdee-ft-reekado banks unaoitwa "bambino".


https://my.notjustok.com/track/download/id/313587


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Msanii wa Uganda Radio Afariki Dunia.

Msanii wa muziki kutoka nchini Uganda, Radio amefariki dunia.

Msanii huyo ambaye alikuwa akifanya vizuri na mwenzie Weasel,  tangu January 23 mwaka huu hali yake ilikuwa ikiripotiwa kuwa mbaya kufuatia majereha aliyoyapata kutokana na ugomvi wa klabu.

Hapo jana Rais wa Uganda, Yoweri Museven alitoa Milioni 30 kwa ajili ya  matibabu ya msanii huyo, pia kulikuwa na maombi maalumu yalikuwa yameandaliwa kwa ajili ya kumuombea ambayo yalitarajiwa kufanyika February 4 mwaka huu katika kanisa la Light the World.

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa