Thursday, 8 February 2018

Majibu ya Serikali Kuhusu Zile Milioni 50 Ilizoahidi Kwa Kila Kijiji

Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dk. Hassan Abbasi amesema kuwa serikali itaweka utaratibu utakaowezesha kutekelezwa kwa ahadi ya kutolewa milioni 50 kila kijiji, hivyo wananchi wasiwe na hofu.


Dkt Abbasi aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu masuala mbalimbali na miradi inayotekelezwa na serikali, na kuweka bayana kwamba, tayari mambo makubwa zaidi yameshafanyika, na hivyo hilo la milioni 50 kila kijiji litatekelzwa pia.


Majibu hayo aliyatoa baada ya mmoja wa waandishi wa habari kuulizwa swali, baada ya kuona ni mwaka wa tatu sasa tangu Rais Dkt Magufuli alipoingia madarakani, lakini ahadi yake ya kutoa TZS milioni 50 kila kijiji kwa ajili ya kuwasaidia kina mama na vijana kujikwamua kiuchumi haijatekelezwa.


“… 50 nyenyewe tutaweka utaratibu itakuja tu ikifika. Lakini maji si yanakuja bana, dawa si zipo, barabara si zipo, sasa kama wewe ulitaka ile 50 ili upige dili, tulia kwanza.”


Aidha, Dkt Abbasi amesema kwamba, ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) haikusema ni lini ahadi hiyo itatekelezwa, kama ni 2017 au 2018, hivyo akawataka wananchi kuwa na subira, pindi utaratibu ukikamilika watapatiwa fedha hizo.


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

0 comments:

Post a Comment