Home »
Michezo
» Okwi Aikutanisha Simba na Waarabu Baada ya Kufanikiwa Hatua ya Kwanza.
SIMBA imefanikiwa kutinga hatua ya kwanza ya michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika baada ya jana kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Gendarmarie nchini Djibouti.Mshambuliaji raia wa Uganda, Emmanuel Okwi, aliifungia Simba bao hilo pekee katika dakika ya 53 na kuifanya Simba sasa kukutana na 'Waarabu' wa Al Masry.Simba imesonga mbele kwa jumla ya mabao 5-0 kufuatia ushindi wa bao 4-0 walioupata kwenye mchezo wa kwanza uliochezwa jijini Dar es Salaam wiki iliyopita.Al Masry yenyewe pia imesonga mbele kwa jumla ya mabao 5-1 baada ya jana kubanwa na Green Buffaloes na kutoka sare ya bao 1-1 nchini Zambia.Katika mchezo wa kwanza uliochezwa Misri, wenyeji walishinda kwa mabao 4-0.Simba sasa itakuwa na kibarua mbele ya Waarabu hao, katika kuwania kutinga hatua ya makundi ya michuano hiyo.Timu hizo zitakutana kati ya Machi 6, 7 mwaka huu, huku Simba wakianzia nyumbani kabla ya kuwafuata Al Masry wiki mbili baadaye.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa
Related Posts:
MAVUGO AUNGANA NA BURUNDI JIJINI DAR, KAZI IPO NA BANDA JUMANNE.FAHAMU ZAIDI HAPA.
Kikosi cha timu ya taifa ya Burundi, tayari kipo nchini kwa ajili ya mechi ya kirafiki dhidi ya Taifa Stars, Jumanne.
Mshambuliaji wa Simba, Laudit Mavugo ameungana na kikosi hicho leo.
Lakini Amissi Tambw… Read More
Hatariii.. Kocha wa Botswana Amefunguka Haya ya moyoni Kuhusu Mbwana Samatta.Fahamu zaidi hapa.
Kocha wa Botswana, Peter Butler ameukubali uwezo wa mshambuliaji wa
Taifa Stars, Mbwana Samatta aliyepachika mabao mawili kwenye mchezo wa
kirafiki, ambao ulichezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Samatta aliwaadhibu … Read More
HIVI NDIVYO MITANDAO YA ULAYA ILIVYO MWANDIKA SAMATA BAADA YA KUFUNGA BAO 2.FAHAMU ZAIDI HAPA.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
&nbs… Read More
Rasmi..Okwi Kutua Simba ..Kaburu Afunguka Haya Mazito Juu ya Ujio Wake.Fahamu zaidi hapa.
MAKAMU wa Rais wa Simba, Geoffrey Nyange ‘Kaburu’, ameonekana
kuwaweka gizani mashabiki wa Yanga kutokana na kitendo chake cha kila
wakati kumtaja Mganda Emmanuel Okwi.
Okwi ni miongoni mwa wachezaji wanaotajwa … Read More
SERENGETI BOYS WAKO BUKOBA, IKIRUDI NI KAZI YA KUIVAA GHANA.FAHAMU ZAIDI HAPA.
Timu
ya taifa ya mpira wa miguu ya vijana wenye umri wa miaka 17 maarufu kwa
jina la Serengeti Boys imetumia ndege ya Shirika la Ndege la Tanzania
(ATCL) kutoka Dar es Salaam alfajiri ya leo Machi 26, mwaka huu na kutua… Read More
0 comments:
Post a Comment