Home »
Burudani
» Tausi Awapa Makavu Wanaomsema Vibaya Kuhusu Mavazi Yake.
Msanii wa filamu nchini Tanzania na Rais wa watoto, Tausi Mdegela amefunguka na 'kuwachamba' watu wanaomsema vibaya kuhusiana na mavazi yake anayovaa na kudai kama inawakera basi wakanunue nguo wampelekee na sio kumpangia cha kuvaa.Tausi ametoa kauli hiyo kwenye kipindi cha KIKAANGONI kinachorushwa mubashara kwenye ukurasa wa facebook wa EATV kila siku ya Jumatano kuanzia saa nane mchana mpaka saa 10 alasiri baada ya baadhi mashabiki zake wakimshambulia kuhusu nguo zake katika mitandao ya kijamii."Mimi ni Tausi na nitabaki kuwa Tausi tuu, nivae joho, pensi hata taiti ni mimi tu. Kwa hiyo mtu hawezi kunipangia maamuzi kuhusu mavazi eti usivae hichi vaa kile. Niletee dera halafu chukua zile pensi choma 'simple' tu", amesema Tausi.Pamoja na hayo, Tausi ameendelea kwa kusema "kwa sababu mimi nimenunua hiyo pensi yangu ni hela ambayo niliyokuwa nayo hiyo siku nikaona nisiondoke mikono mitupu nikanunua hiyo pensi. Wewe ambaye inakukwaza niletee nguo ambayo unahisi nitapendeza tofauti na ninavyovaa".Kwa upande mwingine, Tausi amedai kama mpenzi wake akimsifia kuwa amependeza kutokana na mavazi aliyoyavaa hawezi kumpa nafasi mtu mwingine kumsikiliza juu ya alichokivaa.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa
Related Posts:
Msagasumu Awakata Ngebe Wanawake Wanaomshobokea " Nina Mke Wangu Acheni Shobo".
NGULI wa Muziki wa Singeli, Selemani Jabir ‘Msaga Sumu’, amewakata ngebe wanawake ambao wamekuwa wakimshobokea wakati yeye ana mke na watoto wawili.Akizungumza na Full Shangwe, Msaga Sumu anayebamba na Ngoma ya Mwanaume Mas… Read More
Shamsa Ford Amfunda Shilole "Kuwa Mke Bora kwa Mumeo Ustar Weka Pembeni".
STAA wa Filamu nchini, Shamsa Ford amefungukia uamuzi wa msanii mwenzake wa Muziki, Zuwena Mohammed maarufu kama Shilole kwa kuamua kufunga ndoa tena ya Kidini na mpenzi wake, Uchebe ndoa iliyoshuhudiwa hivi karibuni na kut… Read More
Baada ya Kupitia Changamoto Vanessa Mdee Ashuhudia Maajabu.
Malkia wa Bongo Fleva anayefanya vizuri ndani na nje ya nchi, Vanessa Mdee amekiri kushuhudia maajabu ya Mungu baada ya kupitia changamoto miezi ya mwanzo wa mwaka na hatimaye kumaliza mwaka kwa kusaini mkataba mnene na Kam… Read More
Ramsey Awapa Makavu Wema Sepetu na Ray.
STAA wa sinema za Nigeria (Nollywood), Ramsey Nouah amewalipua waigizaji wa filamu za Kibongo kwa kushindwa kuendeleza sanaa hiyo kwa kiwango alichoishia marehemu Steven Kanumba huku akilizungumzia kaburi la staa huyo, Ijum… Read More
Dully Sykse Atokwa Povu Kisa Bomberdier Atangaza Vita kwa Wasanii Wenzake.
ETI kisa Bombardier! Mkongwe wa Bongo Fleva nchini, Dully Sykse ametoa povu ikiwemo kutangaza vita na wasanii wa kizazi kipya kwa sababu ya kushindwa kumsapoti kwenye wimbo wake mpya.Dully Sykes ambaye ameachia wimbo mpya w… Read More
0 comments:
Post a Comment