Home »
Michezo
» Mzee Akilimali Aibeza Simba "Hakuna Dalili za Simba Kufanikiwa Waarabu ni Moto wa Kuotea Mbali".
KATIBU wa Baraza la Wazee wa Yanga, Mzee Ibrahim Akilimali amesema haoni dalili yoyote ya watani wao Simba kusonga mbele kwenye Kombe la Shirikisho Afrika kwani wamepewa chuma.Kauli hiyo ya Mzee Akilimali imekuja baada ya Simba kutinga raundi ya kwanza ya Kombe la Shirikisho Afrika ambapo sasa itacheza na Al Masry ya Misri Machi 6, mwaka huu.Akizungumza na Championi Jumamosi, Mzee Akilimali alisema haoni dalili za Simba kufanikiwa kwenda hatua kubwa kufuatia kukutana na Waarabu ambao ni moto wa kuotea mbali katika michuano hiyo.“Safari hii naona nao wamepata chuma kwa sababu miaka ya nyuma walikuwa wanatucheka kwamba hatuwezi kucheza na Waarabu nao ndiyo walikuwa wanajifanya wanawamudu kwa kuangalia historia.“Lakini jambo zuri wamepata bahati na wamerejea kwenye michuano ya kimataifa ila sasa wale wanaokutana nao ni chuma cha moto, Simba hawawezi kwenda popote,” alisema Mzee Akilimali.Al Masry ni miongoni mwa timu ambazo zinatoa upinzani mkali kwa vigogo wa soka Misri ambapo ni Zamalek na Al Ahly na sasa wapo nafasi ya nne katika Ligi ya Misri wakiwa na pointi 42.Kocha wa Al Masry ni mshambuliaji wa zamani wa Zamalek, Hossam Hassan ambaye alikuwepo kwenye kikosi cha Zamalek kilichong’olewa na Simba mwaka 2003 katika Klabu Bingwa Afrika.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa
Related Posts:
CHEKA Adai Hakupigwa India, Aeleza Alichofanyiwa na Mwamuzi.Fahamu zaidi hapa.
Bondia Mtanzania Francis Cheka ambaye mwishoni mwa wiki alipoteza
pambano lake nchini India alilopigana na raia wa nchi hiyo Vijender
Singh, ameibuka na kusema kuwa mpinzani wake huyo hakumpiga, ila
alibebwa na mwamuzi.
… Read More
NYOTA WA MAN UNITED WANAVYOKWENDA MAZOEZINI, MWANAYE ROONEY AMFUATA BABA YAKE.FAHAMU ZAIDI HAPA.
Nyota wa Manchester United wanavyokwenda mazoezini, hawatumii basi kama ilivyozoeleka hapa nyumbani.
Mfumo wao ni kila mmoja ni kwenda na usafiri wake na inatumika hivyo, sehemu nyingi za Ulaya.
Lakini juzi, Kai a… Read More
Uhamiaji Yazipiga Marufuku Simba, Yanga na Azam Kutumia Wachezaji wa Kigeni.Fahamu zaidi hapa.
Serikali
imevipiga marufuku Klabu za ligi kuu Tanzania hususani Simba, Yanga na
Azam kuwatumia wachezaji wa kigeni mpaka watakapokamilisha taratibu zao
za uhamiaji.Uamuzi huo umekuja siku chache baada ya klabu ya
Ndanda… Read More
HUYU NDO Jamaa aliyeshinda milioni 760 kwa mkeka mmoja.Fahamu zaidi hapa.
Jamaa mmoja nchini Kenya sikukuu ya Christmas imemjia vizuri baada ya kushinda na mkeka wake kwenye kampuni ya Sport Pesa.
Jamaa mwenyewe jina lake ni Peter Byegon ni mfanyakazi wa hotel moja
huko Nairobi ameshinda baada … Read More
KILICHOJIRI Katika Mgomo wa Saa 24 Wachezaji wa Yanga.Fahamu zaidi hapa.
WACHEZAJI wa Yanga jana walifikisha siku ya pili sawa na saa 24 tangu
wakubaliane kuweka mgomo wa kutofanya mazoezi ya timu hiyo
uliosababishwa na madai ya mshahara wao wa Novemba, mwaka huu.
Kocha Mkuu mpya wa timu hiyo… Read More
0 comments:
Post a Comment