Home »
Michezo
» Simba, Yanga Kumaliza Vipolo Vyao Kabla ya Kusafiri kwa Mechi za Kimataifa.
Vinara wa ligi kuu soka Tanzania Bara Simba SC iliyopo kileleni mwa msimamo na mabingwa watetezi Yanga SC iliyopo nafasi ya pili zinatarajiwa kucheza mechi zao za viporo za VPL kabla ya kusafiri kwa mechi za kimataifa.Yanga ambayo haikucheza mchezo wake wa raundi ya 18 kutokana na wikiendi ililiyopita kucheza mchezo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya St. Lousi ya Shelisheli, itaikaribisha Majimaji FC kwenye uwanja wa Uhuru.Simba wao hawakucheza mchezo wao wa raundi ya 18 kutokana na kuiwakilisha nchi kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika ambapo walicheza na Gendarmerie ya Djibouti. Alhamisi watakuwa mjini Shinyanga kucheza na Mwadui FC.Tayari Yanga wameshaweka wazi kuwa watasafiri siku ya Jumapili Februari 18 kuelekea Shelisheli kwaajili ya mchezo wa marudiano utakaopigwa Februari 21. Simba bado hawajatangaza lini wataondoka nchini.Simba wanaongoza ligi wakiwa na alama 41 huku wapinzani wao wa Alhamisi Mwadui wakiwa katika nafasi ya 12 na alama 18. Yanga ina alama 34 katika nafasi ya tatu huku Majimaji wakiwa nafasi ya 14 na alama 14.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa
Related Posts:
#MICHEZO>>>WACOMORO KUAMUA HATMA YA SERENGETI BOYS AGOSTI 21 CHAMAZI.FAHAMU ZAIDI HAPA.
Shirikisho
la Soka Afrika (CAF), limemteua Noiret Jim Bacari wa Comoro kuwa
mwamuzi wa kati katika mchezo wa marudiano utakaozikutanisha timu za
taifa za vijana za Serengeti Boys ya Tanzania na Amajimbos ya Afrika
Kusi… Read More
#MICHEZO>>>Olimpiki: Brazil Yaingia Nusu Fainali Kwenye Soka la Wanaume.Fahamu zaidi hapa.
Timu ya soka ya wanaume ya Brazil, imeingia nusu fainali ya michuano ya Olimpiki baada ya kuwachapa Colombia, 2-0.
Goli la kwanza lilifungwa na mchezaji wa Barcelona, Neymar baada ya
kupiga free-kick dakika 12 tu baada ya… Read More
#MICHEZO>>>MO BEJAIA WAMALIZA ISHU YA MAZOEZI, KESHO WANASUBIRI KAZI DHIDI YA YANGA TAIFA.FAHAMU ZAIDI HAPA.
Wapinzani
wa Yanga, Mo Bejaia wamefanya mazoezi yao ya mwisho kabla ya mechi ya
Kombe la Shirikisho inayotarajia kupigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini
Dar es Salaam, kesho.
Mo
Bejaia kutoka nchini Algeria walionek… Read More
#MICHEZO>>>>SIMBA NA WATOZA KODI WA UGANDA NGUVU SAWA.FAHAMU ZAIDI HAPA.
Wekundu wa Msimbazi Simba leo wamelazimishwa sare goli 1-1 kwenye mchezo
wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya URA ya Uganda uliochezwa kwenye
uwanja wa taifa.
URA walianza kupata bao lililofungwa na Nkugwa Elka… Read More
#MICHEZO>>>MANCHESTER UNITED KUANZA EPL KWA KUTOA KIPIGO CHA 3-1 KWA BOURNEMOUTH.FAHAMU ZAIDI HAPA.
Bournemouth (4-3-3):
Boruc 5.5; Francis 4.5, A. Smith 6.5, S. Cook 5.5, Daniels 5.5; Surman
5.5, Arter 6, L. Cook 6 (Gradel 82); Ibe 6.5 (Afobe 68, 6), Wilson 5.5
(Grabban 68, 6), King 6.
Subs not used:&n… Read More
0 comments:
Post a Comment