Home »
Habari Moto
» Hoteli ya Hyatt Regency Yatangaza Chumba cha Milioni 22..4 kwa Usiku Mmoja tu wa Valentine, Wabongo Waduwaa.
Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam juzi ilitangaza ofa ya chumba cha Sh22.4 milioni katika Usiku wa Valentine na kusema kuwa Watanzania mbalimbali wamekuwa wakipiga simu kutaka kujua kama ni bei halisi na wengine kuomba punguzo.Hayo yalisemwa na Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo, Denis Glibic alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana kuhusu chumba hicho na namna watu walivyolipokea tangazo hilo.Glibic alisema tangu watangaze ofa hiyo ambayo ni kwa ajili ya wapendano katika sikukuu ya Valentine, wamepokea simu nyingi kutoka kwa Watanzania wakitaka kujua kama kweli hilo ni tangazo lao halisi na wengine wakitaka wapate nafasi hiyo kwa punguzo la bei. Kuhusu chumba hicho ambacho kinatumiwa na marais mbalimbali duniani wanapokuja nchini, meneja mwendeshaji wa hoteli hiyo, Timothy Mlay alisema, kwa kawaida bei yake huwa ni Sh11.4 milioni kwa siku.Alisema pamoja na kuwapo kwa malalamiko ya maisha magumu, wanaamini watu watapatikana kwani kwao kuanzia Desemba mpaka sasa ni kipindi ambacho hupata wateja wengi.Alisema huduma zitakazotolewa kwa wateja wa chumba hicho siku hiyo zitakuwa tofauti kwa wateja wengine, kwani mbali ya kwenda kuchukuliwa na gari la kifahari eneo wanaloishi, pia watapatiwa zawadi za mapambo ya mwilini yenye madini ya Tanzanite
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa
Related Posts:
Lowassa Atua Kenya Kumnadi Uhuru Kenyatta.
Zikiwa
zimebaki siku mbili nchi ya Kenya kufanya Uchaguzi Mkuu, Mjumbe wa
Kamati Kuu ya CHADEMA, Edward Lowassa amefunguka sababu kuu zinazofanya
amtetee na kumnadi mgombea Urais kupitia chama cha Jubilee Uhuru
Kenyatt… Read More
Rais Magufuli awapatanisha Ruge na Makonda.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli amewaunganisha
marafiki waliogeuka kuwa mahasimu wakubwa, Mkuu wa Mkoa wa Dar es
Salaam, Paul Makonda na Mkurugenzi wa vipindi wa Clouds Fm, Ruge
Mutahaba.Rais… Read More
Soma Nafasi za Kazi Zilizotangazwa Leo.
Bonyeza links Zifuatazo Kusoma na Kuapply:
35 Job Opportunities at Tigo Tanzania
Job Opportunity at Equity for Tanzania Ltd (EFTA), Operations Officer
Job Opportunities at MVIWATA, Deadline 25th August 2017
Job Opportu… Read More
Kesi ya Yusuf Manji Yashindwa Kuendelea Kisutu.....Wenzake Warudishwa Rumande.
Kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili mfanyabiashara,Yusuf Manji (41) na wenzake watatu imeahirishwa hadi Agosti 9, mwaka huu.
Hakimu
Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi, aimeiahirisha kesi hiyo leo baada ya Wakili
wa Serik… Read More
Rais Paul Kagame ashinda uchaguzi kwa asilimia 98.
Tume ya Uchaguzi nchini Rwanda inasema kuwa Paul Kagame ameshinda uchaguzi wa uraisi uliyofanyika jana nchini humo.
Tume
hiyo imesema matokeo ya awali yameonyesha kuwa Rais Kagame alishinda
kwa asilimia 98 ya kura zil… Read More
0 comments:
Post a Comment