Tuesday, 30 August 2016

#YALIYOJIRI>>>>WAPINZANI Wamkumbuka Jakaya Kikwete.Fahamu zaidi hapa.

Jakaya Kikwete
Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu amesema wanamkumbuka Rais mstaafu Jakaya Kikwete kwa namna utawala wake ulivyowaruhusu kufanya siasa bila kubughudhiwa.

Akizungumza ofisini kwake jijini Dar es Salaam, amesema “Ninamkumbuka Kikwete. Ninaposema kwamba ninamkumbuka sikumbuki udhaifu wa Serikali yake, siikumbuki Serikali yake ….. Na tumemsema sana. Tulisema huyu rais ni dhaifu na mimi nilimwandika kwenye orodha ya mafisadi.”

Katika utawala wake wa miaka 10, Rais mstaafu Kikwete alikebehiwa ndani na nje ya Bunge kwa kuitwa rais dhaifu, lakini miezi 10 tu tangu astaafu, wapinzani wake wa kisiasa wameanza kumkumbuka.

Kikwete, ambaye alistaafu urais baada ya Rais John Magufuli kuapishwa Novemba 5, 2015, anakumbukwa na wapinzani kwa namna utawala wake ulivyoongeza kasi ya kukua demokrasia na kuukuza upinzani.

#YALIYOJIRI>>>>Lowassa, Mbowe Watakiwa Kuripoti Polisi Leo.Fahau zaidi hapa.

Viongozi waandamizi wa Chadema akiwamo Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa jana walikamatwa na Jeshi la Polisi wakati wakiwa katika kikao cha ndani katika Hoteli ya Giraffe mkoani Dar es Salam

Lowassa, ambaye alikaa kituoni hapo kwa takribani saa tatu anaweza kuwa kiongozi wa kwanza aliyewahi kushika nafasi ya Waziri Mkuu kuhojiwa na polisi.

Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu aliwataja viongozi wengine waliokamatwa kuwa ni Mwenyekiti, Freeman Mbowe, Katibu Mkuu, Dk Vincent Mashinji, Naibu Katibu Mkuu Bara, John Mnyika na Makamu Mwenyekiti Zanzibar, Said Issa.
Mara baada ya kukamatwa, walipelekwa katika Kituo Kikuu cha Polisi ambako baadhi ya wajumbe na wabunge waliwafuata na kuwasubiri nje ya kituo hicho kujua hatima yao. 

Viongozi hao walionekana wakiingia Polisi saa 10.30 jioni na kutoka saa 1.25 usiku, jambo ambalo liliwafanya wakae kituoni hapo kwa saa tatu. 

Lissu alisema polisi walivamia kikao hicho kilichokuwa na wajumbe 170, wakiwamo baadhi ya wabunge wa chama hicho na kuwakamata viongozi hao kwa maelezo kuwa wamekaidi amri ya Jeshi la Polisi ya kuzuia mikutano ya ndani na nje ya vyama vya siasa. 

Imeelezwa kuwa viongozi hao wa Chadema walikuwa na mkutano uliotanguliwa na kikao cha viongozi wakuu na kufuatiwa na cha viongozi hao kikijumuisha wabunge, mameya na wenyeviti wa halmashauri. 

Wakiwa katika kikao hicho, ilielezwa kuwa watu wanne waliingia wakiwa wamevalia kiraia na kuwaeleza kuwa viongozi wao wanahitajika kituo kikuu cha polisi kutokana na kufanya mkutano kinyume cha sheria. 

Mbunge wa Viti Maalumu, Upendo Peneza ambaye  alikuwa kwenye mkutano huo alisema pamoja na mambo mengine ya chama, walikuwa wakijadili suala la operesheni Ukuta la Septemba Mosi kama liendelee au lisiendelee kutokana na hali ilivyo.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro alipoulizwa kuhusu kukamatwa kwao, alisema viongozi hao walikamatwa kwa kukukaidi amri ya polisi ya kuzuia mikusanyiko ya kisiasa na kuchochea wananchi kuandamana kinyume cha sheria Septemba Mosi. 
Alisema baada ya kuachiwa kwa dhamana, viongozi hao wametakiwa kuripoti kituoni hapo leo. 

Wiki iliyopita, Jeshi la Polisi kupitia kwa Kamishana wa Operesheni na Mafunzo, Nsato Marijani lilipiga marufuku mikutano ya ndani likisema inatumika kuhamasisha watu kuvunja sheria za nchi na kupambana na askari. 

Hatua hiyo ilikuja huku jeshi hilo likiwa limepiga marufuku mikutano ya hadhara na maandamano kufuatia uamuzi wa Rais John Magufuli kuzuia shughuli  za kisiasa hadi 2020.

Monday, 29 August 2016

#MICHEZO>>>CHEKI ZAZA ALIVYOKAMILISHA NA KUTUA WEST HAM, SUBIRI MAMBO YAKE.FAHAMU ZAIDI HAPA.

West Ham wamekamilisha usajili wa mshambuliaji Simone Zaza kutoka Juventus ya Italia.

West Ham inayoshiriki Ligi Kuu England, imetoa pauni milioni 4.3 ingawa dili lenye litahusisha jumla ya pauni million 17.

Zaza alipata umaarufu mkubwa kati Euro nchini Ufaransa alipoingizwa katika kipindi cha dakika za nyongeza ikionekana ameingizwa kusaidia litakapofikia suala la kupiga penalti lakini ulipofikia wakati huo akakosa kwa kupiga penalti iliyopewa nina la Mwendo Kasi.

#MICHEZO>>>>MKWASA AMPUMZISHA DIDA TAIFA STARS, YULE KIPA MTAMU WA JKT APATA ULAJI.FAHAMU ZAIDI HAPA.

Kocha Mkuu wa timu ya Mpira wa Miguu Tanzania ‘Taifa Stars’, Charles Boniface Mkwasa, amefanya mabadiliko kwenye kikosi kinachotarajiwa kusafiri Jumatano Agosti 31, 2016 kwenda Nigeria kwa ajili ya mchezo wa mwisho wa kuwania kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2017) dhidi ya timu ya taifa ya nchi hiyo, Super Eagles.
Mabadiliko yaliyofanyika ni kwa kumchukua Kipa kinda wa JKT Ruvu, Said Kipao kuchukua nafasi ya Deogratius Munishi ambaye amefiwa na baba yake mzazi katika kifo kilichotokea jijini Dar es Salaam jana Agosti 28, 2016.

Kipao alikuwa nyota wa mchezo katika mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Simba na mechi ikaisha kwa sare ya bila bao huku yeye akionyesha umahiri mkubwa wa kuokoa michomo ya washambuliaji na viungo wa Simba.

Licha ya mchezo huo wa Septemba 3, 2016 kuwa sehemu ya mchuano wa kuwania nafasi ya kucheza fainali hizo za AFCON 2017 huko Gabon, lakini utakuwa ni wa kukamilisha ratiba baada ya Misri kufuzu kutoka kundi G ambalo mbali ya Nigeria na Tanzania, pia ilikuwako Chad ambayo iliyojitoa katikati ya mashindano.

Wachezaji wanaounda kikosi hicho kwa sasa na kuanza kuingia kambini Hoteli ya Urban Rose jijini Dar es Salaam ni:

Makipa-
Said Kipao – JKT Ruvu
Aishi Manula – Azam FC
Mabeki
Kelvin Yondani - Young Africans
Vicent Andrew - Young Africans
Mwinyi Haji - Young Africans
Mohamed Hussein – Simba SC
Shomari Kapombe - Azam FC
David Mwantika - Azam FC
Viungo
Himid Mao - Azam FC
Shiza Kichuya – Simba SC
Ibrahim Jeba – Mtibwa Sugar
Jonas Mkude – Simba SC
Muzamiru Yassin – Simba SC
Juma Mahadhi - Young Africans
Farid Mussa Tenerif ya Hispania
Washambuliaji
Simon Msuva - Young Africans
Jamal Mnyate – Simba SC
Ibrahim Ajib – Simba SC
John Bocco - Azam FC

 Mbwana Samatta - Genk ya Ubelgiji

Faiza Awataka Wasichana Kuwakimbia Wanaume wa Namna hii.Fahamu zaidi hapa.

Msanii wa filamu Faiza Ally amewataka wasichana wenzake kuwakimbia wanaume ambao wanawataka wasichana ili kufanya nao mapenzi kinyume na maumbile.
Faiza Ally

Muigizaji huyo ambaye yupo mbioni kuachia filamu yake mpya ‘Baby Mama Drama’, amewataka wasichana wenzake kuwaepuka wanaume wa nanma hiyo.

“Mtu anayekutaka kinyume na maumbile ni mtu katili sana,” aliandika Faiza instagram “Wanawake wenzangu msikubali kufanyiwa hivyo, mwananume anaetaka kukufanyia hivyo ni adui na hana mapenzi zaidi ya kuiridhisha nafsi yake tu,”

“Na ukikubaliana nae anaona amepata boya, mifano nimeona mingi sana na wengi wanalia na wamebaki namaumivu na chuki, hata ukinunuliwa gari halita kuwa milele, hata ukiwa na nyumba hutakula matofali, ukipewa hela zitaisha, ukipewa kazi mkataba utaisha pia, ukiolewa baada ya muda utachoka kugeuzwa kila siku na ndoa itakua haina amani moyoni, maana kigezo sio cha kumpendeza Mungu lakini utu wako utabaki milele,” alifafanua.

“Pia siku zote usifike mwisho ukakosa plan b siku zote kuna plan nyingine maana wanawake tunatabia ya kujitolea tupate jambo fulani lakini si kweli kwamba bila kutoa nyuma utafeli kila sehemu, ukikutana na jambo kama hili basi acha tafuta kungine ! hakuna kisicho wezekana haijalishi una haso muda gani, usikubali kuna watu wame haso miaka 30 na akapata wa 31. Mungu anatoa kwa wakati sahihi,” aliongeza.
Aliongeza,

FIESTA MULEBA KAGERA NI BALAA USIKU HUU ..UMATI MKUBWA WA WATU WAJITOKEZA.FAHAMU ZAIDI HAPA.

Kwa updating zaidi endelea kufatilia hii blog>>>"www.hebronmalele.blogspot.com"

#MICHEZO>>>>ALICHO ONGEA WYNE ROONEY BAADA YA KUSIKIA NDUGU YAKE KAPANDA MLIMA KILIMANJARO.FAHAMU ZAIDI HAPA.

August 18 2016 ilikuwa ni siku ya kihistoria kwa Anthony McLoughlin ambaye ni shemeji wa mshambuliaji wa kimataifa wa England anayeichezea Man United Wayne Rooney, Anthony August 18 alifanikiwa kupanda mlima Kilimanjaro uliopo Tanzania.

Anthony amepanda mlima Kilimanjaro ikiwa kama ni sehemu ya kumkumbuka mdogo wake Rosie aliyefariki akiwa na umri wa miaka 14 kutokana na matatizo ya rare genetics disorder (Rett Syndrome) na kuchangisha fedha kwa ajili ya Claire House Charity ambao walikuwa na mchango mkubwa kwa Rosie.
Wayne Rooney

Siku nane baada ya Anthony kupanda mlima Kilimanjaro  na kufika kileleni, Wayne Rooney ambaye ni shemeji yake na Anthony alitumia ukurasa wake wa twitter kumpongeza Anthony, kama hufahamu Anthony ni kaka wa mke wa Wayne Rooney ambaye anajulikana kwa jina la Coleen Rooney.

#YALIYOJIRI>>>>>Lowassa, Mbowe, Mnyika wakamatwa.Fahamu zaidi hapa.

Viongozi wa Chadema wamekamatwa na polisi na kupelekwa Kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam kwa ajili ya mahojiano.

Akizungumzia kukamatwa kwa viongozi hao Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu alisema; “Tulikuwa kwenye kikao cha Kamati Kuu kilichojumuisha wajumbe na wabunge kwa ajili ya kujadili masuala mbalimbali ya chama. Jumla ya wajumbe walikuwa 170. Tukiwa kwenye kikao walikuja watu wanasema tunatakiwa polisi kwa sababu tumekiuka agizo lililokataza mikutano.”

Waliotakiwa kufika makao makuu ya polisi, ni pamoja na mwenyekiti wa chama hicho taifa, Freeman Mbowe; mjumbe wa Kamati Kuu na waziri mkuu mstaafu, Edward Lowassa; Katibu Mkuu, Vicenti Mashinji na naibu katibu mkuu (Bara), John Mnyika.

Mkutano wa kamati kuu ya Chadema, umeitishwa ili kujadili ufanikishaji wa maandamano ya oparesheni UKUTA.

#BURUDANI>>>>Diamond Ajibu Comment ya Shabiki Inayodai Anamuiga Ne-Yo.Fahamu zaidi hapa.

Baada ya mashabiki kumtuhumu Harmonize kumuiga Diamond – sasa imekuwa ni zamu ya hitmaker huyo wa ‘Kidogo’ kuambiwa anamuiga msanii wa Marekani Ne-Yo ambaye tayari ameshafanya naye collabo miezi kadhaa iliyopita.
Kupitia mtandao wa Instagram, mmoja wa mashabiki anayetumia jina la 41732043sandra amecomment moja ya picha ya Diamond aliyoiweka kwenye mtandao huo na kuandika, “You are good and talented in your own way n I love you n ur songs but u should stop copying @neyo… Be ueself boy @diamondplatnumz.”



“Not only copying him, and now in the flight heading to Los Angeles to shoot my new Video Ft. Him….,” amejibu Diamond comment ya shabiki huyo kwenye mtandao huo.

Baada ya kujibiwa comment yake, shabiki huyo aliandika tena, “Unfortunately av no time to argue with ppl….@diamondplatnumz n the rest.. Safe flight n am glad you read my comment n that’s my stand.. Haha be blessed.. I ain’t shaken boo.”

#YALIYOJIRI>>>Polisi Wamevamia Kikao cha Ndani cha Kamati Kuu ya CHADEMA.Fahamu zaidi hapa.

Kikao cha Kamati Kuu (CHADEMA) Kinachofanyika Dar es salaam kimevamiwa na polisi na viongozi walioko meza kuu wa natakiwa kwenda polisi.

Kikao hicho kilikuwa kinafanyika katika Hoteli ya Giraffe iliyopo Mbezi Jijini Dar.

=> Muda mfupi uliopita Mwenyekiti wa Chama Freeman Mbowe, Naibu Katibu Mkuu Bara John Mnyika, Katibu Mkuu Vincent Mashinji na Mjumbe wa Kamati Kuu Edward Lowassa watakiwa polisi.

Msafara huo uko Njiani unaelekea Polisi kituo Kati baada kutaka kikao cha kamati kuahirishwa kwamba vikao na mikutano vimezuiliwa.

#MICHEZO>>> Jose Mourinho Ampiga Mkwara Rashford.Fahamu zaidi hapa.

MWACHENI Jose Mourinho na kiburi chake aisee. Ungeweza kudhani angetoa maneno ya kufariji kwa kinda Marcus Rashford baada ya juzi kuibuka na ushujaa wa dakika za mwisho katika pambano gumu dhidi ya Hull City ugenini. Mourinho bado hajalainika kirahisi hivyo.
Rashford alitokea katika benchi akichukua nafasi ya Juan Mata katika dakika za mwisho za pambano hilo la kusisimua lililopigwa Uwanja wa KCOM jijini Hull na dakika chache baadaye akaifungia Man United bao la ushindi.

Rashford bado hajaanza mechi yoyote chini ya Mourinho licha ya kutamba katika msimu uliopita akiwa na Kocha aliyetimuliwa, Louis van Gaal kiasi cha kuitwa katika kikosi cha timu ya taifa ya England kilichoshiriki michuano ya Euro nchini Ufaransa.

Kwa sasa ametoswa na kocha mpya wa England, Sam Allardayce kwa sababu hiyo hiyo ya kutochezeshwa na Mourinho huku akimpeleka katika kikosi cha timu ya taifa ya England chini ya umri wa miaka 21.

Hata hivyo, licha ya kufunga bao muhimu jana, Mourinho amedai kwamba bao hilo halijamshawishi kuanza kumpanga Rashford tangu mwanzo kwa sababu inabidi afanye kazi kwani, wachezaji wanaoanza wamekuwa wakifanya kazi nzuri.

“Sio kwa sababu amekuwa mshindi wa mechi basi nitabadili mawazo. Huwezi kutompanga mchezaji mwingine wakati wanaoanza wanacheza vizuri. Mshambuliaji wetu namba moja (Zlatan Ibrahimovic) ni mchezaji hatari. Si tu kwamba ni mfungaji lakini anacheza vyema kitimu.

Anatengeneza nafasi,” alisema Mourinho.

 “Ni kweli tunaweza kuanza na mchezaji mwingine mbele ya Zlatan lakini inabidi utawale sana uwanjani ili ulingane naye. Rashford anaweza kucheza au kukaa katika benchi. Hata hivyo, atacheza mechi nyingi msimu huu. Najua alikuwa mzuri msimu uliopita na sasa nafanya naye kazi kila siku na nafikiria hivyo. Alitupa mbinu tofauti alivyoingia.”

Mourinho alikiri kwamba timu yake ilikuwa imeshinda katika dakika za Sir Alex Ferguson, lakini aliamini kuwa bao lilikuwa njiani linakuja huku pia akiipigia saluti safu ya ulinzi ya Hull City ambayo ilicheza kwa ushirikiano mkubwa ndani ya dakika 90 mpaka Rashford alipofunga bao la ushindi kwa krosi fupi ya Wayne Rooney.

“Sir Alex Ferguson ni mtu anayeheshimika katika klabu hii na nina furaha kusema kwamba tulishinda katika muda wa Fergie. Nina furaha sana kusema hivyo,” alisema Mourinho ambaye anajulikana kwa tabia yake ya kumheshimu kocha huyo mkongwe wa Scotland.

“Najua tunapofunga mwishoni watu watasema kuna bahati kidogo lakini ukweli ni kwamba tulistahili, sana sana katika kipindi cha pili. Tulitawala sana mechi, tulicheza kwa nguvu kasi tukishambulia na niliamini kuwa bao lingekuja tu,” alisema Mourinho.

“Inabidi niseme kwamba Hull City walifanya kazi ya ajabu na walijilinda sana kwa kila namna. Hawakuweza kufanya mashambulizi ya kushtukiza kwa sababu naamini tulijilinda vizuri sana. Hongera kwao na kama ningekuwa Mwenyekiti wao ningempa kazi ya kudumu kocha Mike Phelan haraka sana.”

“Kila mtu anaona kwa macho yake, wachezaji wanatoa kila walichonacho kwa ajili yake. Wasingeweza kufanya zaidi ya kile walichofanya na hongera sana kwa Mike na vijana wake,” alisema Mourinho ambaye kwa ushindi huo United yake inakuwa na pointi tisa baada ya kushinda mechi zote tatu za mwanzo dhidi ya Southampton, Bournemouth na Hull City juzi usiku.

Hata hivyo, mtihani wa kwanza halisi kwa United unatazamiwa kuwa dhidi ya Manchester City katika pambano lijalo la Ligi Kuu baada ya mechi za kimataifa zinazotazamiwa kuchezwa wikiendi ijayo.

Pambano hilo litachezwa Septemba 10 huku likitazamiwa kuwakutanisha makocha wawili mahasimu wa muda mrefu, Jose Mourinho na Pep Guardiola wa Manchester City.

#YALIYOJIRI>>>Wasomi: JPM Na Lowassa Wameonyesha Kuwa Mazungumzo Yataleta Muafaka.Fahamu zaidi hapa.

Na Tiganya Vincent
Wasomi na Wanazuoni mbalimbali wamepongeza hatua ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli na Waziri Mkuu zamani  Edward Lowassa kushikana mikono na kusalimiana wakati wa Jubilei ya dhahabu ya miaka 50 ya ndoa ya Rais Mstaafu Benjamin William Mkapa na Anna Mkapa.

Wanazuoni hao wametoa  kauli hiyo jana katika mahojiano maalum na Idara ya Habari iliyokuwa ikitaka kupata maoni yao kuhusu kitendo kilichoonyeshwa na viongozi hao kwa jamii.

Profesa Kitila Mkumbo wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam alisema kuwa hatua hiyo imeonyesha kuwa huo ndio Utanzania ulivyo wa kutofautiana bila kugombana.

Alisema kuwa kitendo hicho kimewaonyesha wananchi kuwa mazungumzo yana nafasi kubwa ya kuondoa tofauti zilizopo kuliko kutumia njia nyingine kama vile maandamano na mabavu katika kutafuta ufumbuzi wa baadhi ya matatizo.

“Kukutana kwa viongozi hao na kupeana mikono wakati wa kusalimiana kunakumbusha utamaduni wetu uliojingekea toka siku nyingi wa kutatua matatizo yetu kwa mazungumzo bila kugombana au kutumia mabavu,”alisema Profesa Mkumbo.

Kwa upande wa Profesa Joseph Semboja alisema kuwa amefurahishwa sana na kitendo kilichoonyeshwa na viongozi hao kwani kimeuonyesha ulimwengu kuwa Watanzania ni watu wenye  Amani na upendo.

Alisema kuwa hatua hiyo imeonyesha kuwa Watanzania wanaweza kuwa na tofauti lakini wakaendelea kuishi pamoja na kushirikiana katika mambo mbalimbali ya kijamii kwa ajili ya maendeleo yao na Taifa lao.

Profesa Semboja aliwataka wananchi kujifunza kutokana na kitendo kilichoonyeshwa na viongozi hao ambao wameonyesha kuwa ni lazima wakae pamoja kwa ajili kushughulikia mambo muhimu ya maendeleo ya wananchi badala kuendeleza tofauti ambazo hazina manufaa kwa Watanzania.

Alisema kuwa ipo haja ya kwenda zaidi ya hapo kwa kuweka utaratibu wa kukaa pamoja na kujadiliana ili kutatua vyanzo vya migogoro kwa ajili ya mustakabali mzuri wa Taifa hili.

Profesa alisema kuwa sio sahihi kutumia mfumo wa jino kwa jino kwani utaratibu huo ndio unaoweza kusababisha kukua zaidi kwa migogoro na wakati mwingine unasababisha umaskini kwa wananchi na Taifa kwa ujumla kwani muda mwingi wananchi hawana muda wa kushiriki katika shughuli za maendeleo kwa sababu ya migogoro.

Naye Profesa Samwel Wangwe alisema kuwa hatua ya viongozi hao kukutana na kupeana mikono ni ishara kwa Watanzania kujifunza kuwa mazungumzo yana nafasi kubwa katika kuleta muafaka mgogoro wowote kuliko kutunishiana misuli.

Alisema kuwa mazungumzo yana nguvu kubwa katika kuleta upatanishi katika migogoro mbalimbali inatokea katika jamii kuliko kutumia njia nyingine ambazo zinaweza kusababisha vurugu na uharibifu wa mali za watu na upotevu wa maisha ya watu.

#YALIYOJIRI>>>>WALIMU 22 Azania Sekondari Waondolewa Baada ya Shule Kuwa ya Mwisho Matokeo Kidato cha Sita.Fahamu zaidi hapa.

Walimu 22 wa Shule ya Sekondari ya Azania Manispaa ya Ilala, akiwamo Mwalimu Mkuu, wamehamishwa kwa kile kilichodaiwa ni kutokana na matokeo mabaya ya kidato cha sita.
Chanzo hicho cha habari kiliongeza kuwa kati ya walimu hao, 17 walikuwa wanafundisha kidato cha tano na sita huku wanne kidato cha kwanza hadi cha nne na mmoja aliyekuwa mkuu wa shule hiyo.

Taarifa hizo ziliongeza kuwa kati ya walimu 17, wengi wao walikuwa wanafundisha mchepuo wa ECA ambao wote wamehamishwa na kupangiwa shule nyingine huku wengine wakihamishiwa shule za kata na kupangiwa kufundisha kidato cha kwanza, pili na tatu. Awali, walimu hao walikuwa wakifundisha kidato cha tano na sita.

Hivi karibuni Baraza la Mitihani Tanzania (Necta), lilitangaza matokeo ya kidato cha sita na shule hiyo kongwe ikajikuta imo katika kundi la shule 10 za mwisho zilizokuwa na matokeo mabaya.

#YALIYOJIRI>>>>Lema Aendelea Kugoma kula akiwa mahabusu.Mwanasheria Wake Kufungua Kesi Mahakama Kuu Leo.Fahamu zaidi hapa.

MBUNGE wa Arusha Mjini, Godbless Lema (Chadema), ameendelea kugoma kula kwa siku ya tatu mfululizo tangu alipokamatwa Oktoba 26 mwaka huu, nyumbani kwake mjini hapa, akidaiwa kutoa maneno ya uchochezi.


Lema alikamatwa siku hiyo saa 12 alfajiri akiwa nyumbani kwake, Njiro,  na hadi sasa anashikiliwa katika mahabusu ya kituo kikuu cha polisi mjini Arusha.



Kutokana na kuendelea kugoma kula, Wakili wake, John Mallya amesema leo saa sita mchana atakwenda Mahakama Kuu, Kanda ya Arusha kufungua kesi ya kutaka mteja wake afikishwe mahakamani.



Malya jana alisema katika kesi hiyo atashirikiana na Chadema kuwashtaki mwendesha mashitaka mkuu wa Serikali na mkuu wa upelelezi wa makosa ya jinai, Mkoa wa Arusha.



Tangu mbunge huyo akamatwe amegoma kula kwa  kile anachodai kupinga udhalilishwaji aliofanyiwa na polisi wakati wa kukamatwa.



Pia, Lema anasema alinyanyaswa mbele ya watoto wake nyumbani kwake huku wakijua yeye ni kiongozi na amechaguliwa na wananchi.



Neema, mkewe Lema,jana alithibitisha kwamba  mumewe amegoma kula.



“Anaendelea kugoma kula mpaka sasa kwa sababu  hata sasa nimetoka polisi asubuhi kumpelekea chakula, lakini amekataa kula.



“Lakini nilipouliza pale polisi kuwa wanampeleka lini mahakamani, nilijibiwa wanaendelea kumhoji,”alisema Neema.



Juzi, Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo, alithibitisha kukamatwa kwa Lema na kueleza kuwa alihojiwa dhidi ya matamshi ya uchochezi na kuwa atafikishwa mahakamani baada ya kukamilika   uchunguzi.



Kwa mujibu wa Kamanda Mkumbo, Lema anatuhumiwa kuwachochea wakazi wa Arusha kuandamana Septemba mosi, mwaka huu kuhamasisha kile kinachoitwa Umoja wa Kupinga Udikteta Tanzania (Ukuta).

#BURUDANI>>>>PICHA: Diamond Avunja Rekodi Meru, Kenya.Fahamu zaidi hapa.

 Diamond Platnumz ana miaka mingi ya kuvuna mapesa kutokana na show zake. Kutoka kwenye mapokezi yaliyovunja rekodi, Meru nchini Kenya hadi kuangusha show iliyohudhuriwa na makumi kwa maelfu ya mashabiki wenye kiu, staa huyo ameendelea kujiweka kwenye ligi yake mwenyewe.
 Ilikuwa ni show ya mtu mmoja na kwa picha alizoweka kwenye page yake ya Instagram, inaonesha jamaa alihama na kijiji. Tazama picha hapo chini.

#YALIYOJIRI>>>Profesa Lupumba,Magdalena Sakaya na Abdul Kambaya Wavuliwa Uanachama CUF..Fahamu zaidi hapa.

Chama Cha Wananchi (CUF) kimewasimamisha uanachama aliyekuwa Mwenyekiti wa chama hicho, Profesa Ibrahim Lipumba na Katibu Mkuu wa chama hicho upande wa Bara, Magdalena Sakaya.

Uamuzi huo umetolewa jana na Baraza Kuu la Chama hicho lililofanya mkutano wake visiwani Zanzibar kwa lengo la kuwajadili wanachama kadhaa wakiwemo vigogo hao. Sakaya amevuliwa nyadhifa zote ndani ya chama kabla ya kusimamishwa.

Taarifa kutoka ndani ya Mkutano huo zimeeleza kuwa Baraza hilo limewaadhibu wanachama 15 wakiwemo Sakaya ambaye pia ni mbunge wa Kaliua.
Mbali na vigogo hao, wengine waliopigwa rungu na Baraza Kuu la CUF ni pamoja na Katibu wa Baraza la Wazee, Shashi Lugeye, Thomas Malima na Naibu Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano, Abdul Kambaya.

Aidha, Baraza hilo limemsimamisha uanachama Mbunge wa Mtwara Mjini, Maftah Nachuma. Hatua hii inaweka matatani ubunge wa Sakaya na Nachuma kwani wakifikia hatua ya kufukuzwa watakosa sifa za kuendelea kuwa wabunge.

Lipumba na Sakaya hawakupata nafasi ya kujitetea kutokana na kutohudhuria mkutano huo wakati Shashi alipata nafasi ya kujitetea kutokana na uwepo wake lakini utetezi wake haukuzaa matunda. Katiba ya chama hicho haiwapi nafasi wabunge hao kukata rufaa kutokana na uamuzi wa Baraza hilo.

Uamuzi huo umekuja ikiwa ni siku chacha baada ya Mkutano Mkuu Maalum wa Chama hicho uliolenga kumchagua Mwenyekiti Mpya kuvunjika kutokana na kuwepo vurugu kubwa baada ya Profesa Lipumba kuingia ndani ya ukumbi huo na wafuasi wake wakitaka barua yake ya kutaka kurejea kwenye nafasi yake ijadiliwe na kukubaliwa.

Hata hivyo, kura zilizopigwa na wajumbe wote zaidi ya 800, ni kura 14 pekee zilizotaka Profesa Lipumba aendelee na nafasi ya uenyekiti.

#YALIYOJIRI>>>>>Ufafanuzi wa CHADEMA kuhusu taarifa ya kuahirishwa Operesheni UKUTA.Fahamu zaidi hapa.

CHADEMA inapenda kutoa taarifa kwa umma kuhusu andiko linalosambazwa mitandaoni likimnukuu Mwenyekiti wa Chama Taifa, Freeman Mbowe kuwa ameahirisha Operesheni UKUTA na maandalizi ya Septemba 1.

Tunaomba umma upate taarifa sahihi kuwa Mwenyekiti Mbowe hajafanya mkutano na waandishi wa habari mahali popote pale kuzungumzia kuahirisha Operesheni UKUTA inayoendela nchi nzima wala kuzuia maandalizi ya Septemba 1.

Kupitia taarifa hii, chama kinawataka viongozi, wanachama, wafuasi, wapenzi na mashabiki wa CHADEMA na Watanzania wote wazalendo na wapenda haki, kupuuza andiko linalosambazwa mitandaoni .

Msisitizo unaendelea kutolewa kuwa Operesheni UKUTA ambayo imelenga kusimamia utawala unaoheshimu Katiba ya Nchi na kulinda sheria na maandalizi yanaendelea nchi nzima.

Imetolewa na;

Tumaini Makene
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano
CHADEMA

#BURUDANI>>>Nisamehe ya Barakah Da Prince na Alikiba Kuanza Kuonyeshwa MTV Base.Fahamu zaidi hapa.

Wimbo wa Barakah Da Prince na Alikiba ‘Nisamehe’ utaachiwa wiki hii.
Video na wimbo vyote vitatoka pamoja, kwa mujibu wa Barakah.

“Video itatoka kwenye exclusive MTV Base kabla ya kituo chochote,” Barakah alimweleza mtangazaji wa Jembe FM, JJ.
Hivi karibuni Alikiba pia alishoot video yake mwenyewe na ile aliyoshirikishwa na Ommy Dimpoz nchini Afrika Kusini.

#YALIYOJIRI>>>>Waziri wa Habari Nape Nnauye amevifungia vituo vya redio vya Magic FM na Redio 5 ya Arusha kwa madai ya uchochezi.Fahamu zaidi hapa.

WAZIRI wa Habari, Utamaduni , Sanaa na Michezo Nape Moses Nnauye amezifungia radio mbili kwa muda usiojulikana kwa makosa ya kuandaa vipindi ambavyo vimerushwa hewani vinavyoashiria uchochezi.

Akizungumza na waandishi wa habari, Waziri Nape amesema kuwa uamuzi wa kuvifungia vituo hivyo umefikiwa baada ya kujirdhisha kuwa kipindi cha Matukio kilichorushwa Agosti 25, 2016 muda wa saa 2 usiku hadi saa 3 na kituo cha utangazji cha Radio 5 pamoja na kipindi cha Morning Magic katika kipengele cha Kupaka Rangi Agosti 17 vilikuwa na maudhui ya uchochezi unaoweza kuleta uvunjifu wa Amani.

Nape amesema kuwa kufuatia hilo amevifungia kwa muda usiojulikana kwani wamekiuka masharti ya kanuni ya 5 (a, b, c na d) , kanuni ya 6 (2a, b na c) na kanuni ya 218 ya huduma za utangazaji ya mwaka 2005.

Wakati vituo hivyo vikifungiwa kwa muda usiojulikana kamati ya maudhui imepewa jukuu la kuviita na kusikiliza kwa kina Zaidi utetezi wao na ni hatua gani zaidi ya kuchukua dhidi yao kwa mujibu wa kanuni ya huduma za utangazaji.

Nape ameendelea kuvitahadhalisha vyombo mbalimbali vya habari kutoshawishika kuvunja sheria na kanuni zinazoongoza tasnia ya habari ili kulinda heshima ya tasnia yetu na wakati huo kuhakikisha nchi inabaki na Amani, Mshikamano na Umoja.