Thursday, 30 March 2017

ILE TAARIFA YA NYASI BANDIA ZA SIMBA ZILIZO BANDARINI KUTAKA KUPIGWA MNADA IKO HIVI.

Kuna taarifa ya nyasi za bandia za Simba kutaka kupigwa mnada imekuwa ikisamabaa kwa kasi kubwa mitandaoni na iko hivi.

"Kampuni ya udalali ya Majembe Auction Mart inataka kupiga mnada nyasi bandia za SIMBA SPORTS CLUB na magoli yake, sababu kubwa ni uongozi (wamiliki) kushindwa kuzilipia kodi. 

Mnada utafanyika siku ya:
Alhamisi 30/03/2017. 

Eneo:Nyuma ya "The Waterfront Sunset Restaurant and Beach Bar", barabara ya Yatch Club, Masaki, ofisi mnada utakaofanyika zinaitwa LW9.

Juhudi za kuwasaka viongozi wa Simba ili walizungumzie hili zinaendelea. Baadhi yao bado hawajapokea simu na wengine tunaendelea kuwatafuta.


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

DOWNLOAD WIMBO MPYA WA BIBI CHEKA UNAOITWA "SONG NALIA".




Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

Serengeti Boys yatoa kipigo kwa warundi kwa goli 3-0.Fahamu zaidi hapa.

Timu ya taifa ya Tanzania chini ya miaka 17, Serengeti Boys, leo imeibuka na ushindi mnono wa mabao 3-0 dhidi ya vijana wenzao wa Burundi katika mchezo wa kirafiki uliopigwa kwenye Uwanja wa Kaitaba, Kagera.

Katika mchezo huo ambao Serengeti Boys inautumia kwa ajili ya maandalizi yao kabla ya kwenda Gabon kushiriki michuano ya Kombe la Mataifa Afrika kwa vijana chini ya miaka 17, ulishuhudiwa mpaka mapumziko timu hiyo ikiwa mbele kwa mabao 2-0.

Mabao hayo yalifungwa na Muhsin Makame dakika ya 20 na Nickson Kibabage, huku Yohana Mkomola akimalizia msumari wa mwisho dakika ya 72 kwa njia ya mkwaju wa penalti na kukamilisha idadi hiyo ya mabao 3-0.

Baada ya leo kumalizana na Burundi, Jumatatu ijayo kikosi cha Serengeti Boys kinatarajiwa kucheza mchezo wa mwisho wa kirafiki jijini Dar es Salaam dhidi ya Ghana kabla ya kwenda Morocco kuweka kambi ya mwisho ya kujiandaa na michuano hiyo ya vijana.


Katika michuano hiyo itakayoanza kuunguruma Mei 14, mwaka huu, Serengeti Boys imepangwa Kundi B sambamba na timu za  Mali, Niger na Angola. Kama Serengeti Boys itafanya vizuri kwenye michuano hiyo, basi itajikatia tiketi ya kwenda kushiriki michuano ya Kombe la Dunia chini ya miaka 17 itakayofanyika hapo baadaye nchini India.


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

WATU WAHOJI HUU UMATI WA WAANDISHI WALIOHUDHURIA MKUTANO WA MAKONDA LEO KAMA SIO UNAFIKI NI NINI ? FAHAMU ZAIDI HAPA.

Waandishi wakimsubiri RC Makonda leo mjini Dodoma kabla ya mkutano wake na wanahabari.

WATU WANAHOJI KAMA WAANDISHI WALIKUWA NA MGOMO NA RC MAKONDA VP HUU UMATI WA WAANDISHI WAKAHUDHURIA HUU MKUTANO WA RC MAKONDA ULIOFANYIKA DODOMA LEO.



Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

Ripoti: Tanzania Yaongoza Afrika kwa Kupokea Wageni Wengi Zaidi kwa Njia ya Anga.Fahamu zaidi hapa.

Tanzania imechangia asilimia 19.3 ya jumla ya wageni wa kimataifa kupitia anga (international air arrivals) ukilinganisha na asilimia 18.2 ya Kenya, asilimia 17.2 Misri na asilimia 12.1 ya Afrika Kusini katika kipindi cha kuanzia September 2016 hadi January 2017.
Takwimu hizi ni kwa mujibu wa ripoti mpya ya shirika la ufuatiliaji wa masuala usafiri wa ndege, ForwardKeys ambayo hulinganisha ukataji tiketi za ndege zaidi ya milioni 16 kila siku ili kuiweka Afrika kwenye ramani ya utalii duniani.
Kwa jumla, Afrika Mashariki ina asimilia 16.4 ya ufikaji wa wageni kwa njia ya anga. Na kwa ujumla pia, kuna ongezeko la asilimia 10.3 ya ufikaji wageni Afrika



Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

#BREAKING NEWS>>>CLOUDS WAMSIMAMISHA MTANGAZAJI KWA KUTANGAZA HABARI ZA PAUL MAKONDA.FAHAMU ZAIDI HAPA.

Bodi ya Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) imekutana jijini Dar es Salaam leo Machi 30, 2017. Pamoja na mambo mengine imejadili mwenendo wa vyombo vya habari ndani ya wiki moja tangu tulipotoa msimamo wa kutotangaza habari za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.
 
Bodi imepitia habari za Mkuu wa Mkoa zilizochapishwa tangu ulipotolewa msimamo wa kumfungia. Bodi inapenda kawapongeza wahariri wote waliotekeleza kwa usahihi msimamo wa kutochapisha habari za Mkuu wa Mkoa kwa wiki nzima.
 
Bodi inapenda kusisitiza kuwa wahariri katika vyombo vya habari; magazeti, radio na televisheni waendelee na msimamo wa kususia habari za Mkuu wa Mkoa, Paul Makonda, hadi atakapotimiza takwa la kuomba radhi kwa tukio la kuvamia kituo cha Clouds.
 
Bodi inatoa wito kwa viongozi wa mitandao ya kijamii kuunga msimamo huu. Bodi inapenda kufafanua kuwa Mhe. Makonda amewekewa vikwazo Maalum (Smart Sanction) kwa mikutano atakayoiandaa au matukio atakayoyaongoza habari zake hatutazichapisha.
 
Bodi inakipongeza Kituo cha Clouds kwa kumsimamisha kazi mtangazaji aliyekiuka msimamo wa kutotangaza habari za Makonda. Bodi pia imewasiliana na Uongozi wa UTPC na kukubaliana kwamba msimamo huu uendelee.
 
Theophil Makunga,
 
Mwenyekiti TEF
 
Imetolewa Leo,
 
Machi 30, 2017



Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

Jide Afunguka ya Kuachwa na Mnigeria Wake.Fahamu zaidi hapa.

Jide afunguka ya kuachwa na Mnigeria wake

Wakati maneno ya chini chini yakiwa yanaendelea kuhusu kupigwa kibuti na mpenzi wake mpya Spicy kutoka Nigeria, Judith Wambura ‘Lady Jaydee’ amefunguka na kusema wabongo wengi wanapenda wenzao waharibikiwe na kuwataka kuacha kuwaziana mabaya.

Jide amelazimika kutoa kauli hiyo baada ya maneno kuzagaa kuwa amepigana kibuti na Mnigeria huyo ikiwa ni siku wiki chache baada ya kuandika maneno yaliyomo kwenye wimbo wa  Rosella katika mtandao wa Instagram.

“Niko vizuri na Spicy, yale maneno niliandika kwa ajili ya muziki, watu wanapenda kuona wenzao wanaharibikiwa, kwanini wanakimbilia kuamini nina matatizo na Spicy na hawafikirii kuhusu kazi yangu? Niwakaribishe waje kwenye show yangu ya uzinduzi pale Lugalo Uwanja wa Gofu Ijumaa hii,” alisema Jide.
Lady Jaydee anayetamba na wimbo wa Rosella alioshirikiana na h_art the band kutoka Kenya anatarajiwa kuzindua albamu yake ya saba tarehe 31 ya mwezi huu.


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

Kimenukaa..Mama Yake Hamisa Mobeto Atolea Kichambo Hiki Zari the Boss Lady,Amtaka Akome Kumtajataja Mwanae Mitandaoni.Fahamu zaidi hapa.

DAR ES SALAAM Skendo ya mjini iliyotapakaa mjini na kwenye mitandao ya kijamii inamgusa modo maarufu Bongo, Hamisa Mobeto akidaiwa kujichora ‘tatuu’ ya mwanamuziki maarufu Bongo, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, ishu iliyosababisha mwandani wa jamaa huyo, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ kumporomoshea matusi.
Kuhusu sakata hilo, mama mzazi wa Mobeto ameshindwa kujizuia na kujikuta akimtolea povu Zari juu ya mwanaye huyo. Akizungumza na gazeti hili kwa uchungu alipoulizwa kuhusu sekeseke hilo la mwanaye, mama Mobeto alisema kuwa, hakuna wakati mgumu kama kuona mtoto wake huyo anazungumziwa vibaya kila wakati katika mitandao ambapo wakati mwingine siyo jambo la kweli zaidi ya kumchafua tu.
“Jamani mimi kama mzazi, sidhani kama kuna mzazi yeyote anayeweza kuvumilia kuona mwanaye kila mara yuko kwenye midomo ya watu au kuongelewa vibaya kwenye mitandao ya kijamii kwa vitu ambavyo hajafanya,” alisema mama Mobeto. Alifunguka kuwa, habari ambayo imesambaa kuhusu mwanaye kujichora tatuu ya Diamond, anaona ni mambo ambayo hayana msingi wowote zaidi ya kumchafua na kumdhalilisha mwanaye.
“Unajua unapomuona Hamisa (Mobeto) amenyamaza, kila wakati wanatafuta kumuwekea jambo baya,  kitu ambacho siyo sahihi, mimi sijawahi kuiona hiyo tatuu wanayosema zaidi ya kuona kuwa wanampandikizia maneno tu ya kumchafua, sipendezwi kabisa na tabia hiyo,” alisema mama Mobeto.
Hivi karibuni Zari alimtolea matusi Mobeto kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii akimtahadharisha juu ya habari zilizozagaa kuwa, huwa anachepuka na Diamond kwa siri hasa mwanamama huyo anapokuwa nyumbani kwake, Afrika Kusini na kumwacha baba watoto wake huyo jijini Dar.




Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

Acha Kubaka Wewe...Fahamu Njia Adimu za Kumfanya Mwanamke Afike Kileleni Haraka.Fahamu zaidi hapa.

Kuna njia mbalimbali za kumuongezea wigo mwanamke kufika kileleni na kuna kitu kimoja wanawake wote husema, "Kufika kileleni huitaji utulivu wa akili na hisia ".
Kama ukimweka mwanamke kwenye mazingira mazuri kiakili na kihisia, kuna uwezekano mkubwa na mwili wake kufuata na kumfanya afike kileleni.
Japo wanawake wanatofautiana, imejaribu kuongea na baadhi ya wanawake na wametumegea siri na kutupa njia nzuri ya kumfikisha kileleni mwanamke kwa haraka, japo ilikua mpaka tulipowapa baadhi ya siri zetu za kiume kidogo ndo wakalainika kutuambia...
Kama ukitaka kumfikisha kileleni kwa haraka, ni vizuri mwanamke ukamweka juu yako ili aweze kudhibiti kasi, msuguano na engo ya uume wako ndani yake, japo nawe unaweza kupata matamanio ya kumsaidia, ila ni vizuri ukamwacha mwenyewe ili usije kumharibia kasi anayoitaka yeye na kuitumia.
Inabidi upambane na matamanio yako na uendelee kutulia na umsikilize anataka wewe ukaeje ili ajiongezee msisimko zaidi na kwa sasa inabidi uutulize mwili huku mikono yako ikishughurika na uitumie vizuri, unaweza kuwa unampapasa sehemu za makalio yake au nyuma ya kichwa chake sehemu za shingoni mpaka kisogoni kwa hali ya kimahaba, na kama umekaa wima utajiongezea pointi zaidi kwa kumbusu shingoni na kuongea maneno mazuri ya kimahaba na kumsifia kwa uzuri wake na sifa nyingine


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

Wakili kaeleza sababu za Mbunge Lijualikali kuachiwa huru.

Mahakama Kuu kanda ya Dar es Salaam March 30 2017  imetengua hukumu iliyotolewa na Mahakama ya Wilaya Kilombero dhidi ya Mbunge Peter Lijualikali baada ya kukubali kuwa hati ya mashtaka iliyomtia hatiani ilikuwa na mapungufu.

Mmoja wa mawakili waliokuwa wakisimamia rufaa ya mbunge Lijualikali, Fred Kiwelo amesema sababu mojawapo iliyopelekea kuachiwa huru ni pamoja na hati mashtaka kuwa na mapungufu ambapo kosa ambalo alikuwa amehukumiwa nalo limetofautiana na maelezo ambayo amesomewa.


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

Jukwaa la Wahariri Latoa Tathmini ya iki moja ya Kususia Habari Makonda.Fahamu zaidi hapa.

Bodi ya Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) imekutana jijini Dar es Salaam leo Machi 30, 2017. Pamoja na mambo mengine imejadili mwenendo wa vyombo vya habari ndani ya wiki moja tangu tulipotoa msimamo wa kutotangaza habari za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

Bodi imepitia habari za Mkuu wa Mkoa zilizochapishwa tangu ulipotolewa msimamo wa kumfungia. Bodi inapenda kawapongeza wahariri wote waliotekeleza kwa usahihi msimamo wa kutochapisha habari za Mkuu wa Mkoa kwa wiki nzima.

Bodi inapenda kusisitiza kuwa wahariri katika vyombo vya habari; magazeti, radio na televisheni waendelee na msimamo wa kususia habari za Mkuu wa Mkoa, Paul Makonda, hadi atakapotimiza takwa la kuomba radhi kwa tukio la kuvamia kituo cha Clouds.

Aidha, Bodi inatoa wito kwa viongozi wa mitandao ya kijamii kuunga msimamo huu. Bodi inapenda kufafanua kuwa Mhe. Makonda amewekewa vikwazo Maalum (Smart Sanction) kwa mikutano atakayoiandaa au matukio atakayoyaongoza habari zake hatutazichapisha.

Wakati huo huo, kituo cha Clouds kimepongezwa kwa kumsimamisha kazi mtangazaji aliyekiuka msimamo wa kutotangaza habari za Makonda.

Bodi pia imewasiliana na Uongozi wa UTPC na kukubaliana kwamba msimamo huu uendelee.

Theophil Makunga,
Mwenyekiti TEF

Imetolewa Leo,
Machi 30, 2017


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

Mashabiki wa Muziki Wamdhihaki Diamond Mtandaoni.Fahamu zaidi hapa.

MASHABIKI  wa muziki wa  Bongo Fleva nchini wamekuwa wakisambaza picha ya mwanamuziki nyota, Nassib Abdul ‘Diamond Platnumz’,  ikimuonyesha akiwa katika hali duni tofauti na ukwasi alionao hivi sasa.

Mashabiki hao wamekuwa wakiisambaza picha hiyo kwa lengo la kumdhihaki ili kuonyesha kuwa maisha huanzia mbali,  hivyo watu wasisahau walikotokea.

Picha hiyo imekuwa ikisambazwa pamoja na ujumbe tofauti hivyo kuwaudhi  mashabiki wa mwanamuziki huyo na kuwafurahisha mahasimu wake.

Aidha  picha hiyo inawaonyesha Diamond na mwigizaji Irene Uwoya ambapo Diamond anaonekana katika taswira ya kijana mwenye hali duni tofauti na alivyo hivi sasa.


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

Wednesday, 29 March 2017

Mwenyekiti Wa Chama Cha Mapinduzi CCM Rais Dkt. Magufuli Aendesha Kikao Cha Kamati Kuu Ya Halmashauri Kuu Ya Taifa Ya CCM Jijini Dar Es Salaam.Fahamu zaidi hapa.

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais  Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akijiandaa kuendesha Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi CCM leo jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais  Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Rais wa Zanzibar ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti CCM (Zanzibar) Dkt. Ali Mohamed Shein, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge Job Ndugai, Waziri Mkuu Mstaafu Dkt. Salim Ahmed Salim, Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi wakiwa pamoja na Wajumbe wengine wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi CCM, mara baada ya kumalizika kwa kikao hicho jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais  Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Rais wa Zanzibar ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti CCM (Zanzibar) Dkt. Ali Mohamed Shein mara baada ya kumalizika kwa kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama cha  Mapinduzi CCM kilichofanyika jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais  Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama cha  Mapinduzi CCM Dkt. Salim Ahmed Salim mara baada ya kumalizika kwa kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama cha  Mapinduzi CCM kilichofanyika jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

BAADA YA FIFA KUMFUNGIA MESSI MECHI NNE, BARCELONA YATOA INACHOKIAMINI.FAHAMU ZAIDI HAPA.

Baada ya Lionel Messi kufungiwa mechi nne na Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) baada ya kumshushia matusi mwamuzi wa pembeni, Klabu ya FC Barcelona imetoa tamko.


FC Barcelona imesema haiungi mkono waamuzi kunyanyaswa lakini adhabu ya Messi kwa timu yake ya taifa ni kubwa sana.


Uongozi wa Barcelona umesisitiza Fifa wametoa adhabu kubwa sana kwa Messi na walipaswa kumfikiria.

Messi alimtukana mwamuzi huyo wakati Argentina ilipocheza mechi ya kufuzu Kombe la Dunia na kuifunga Chile kwa bao 1-0, yeye akiwa mfungaji.


Mechi iliyofuata, ikiwa ndiyo inamkosa Messi, Argentina ilitwangwa kwa mavao 2-0 na Bolivia.

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

OZIL SASA ACHOSHWA NA MASHABIKI ARSENAL WASIOISHA LAWAMA, ATOA POVU.FAHAMU ZAIDI HAPA.

Kiungo nyota wa Arsenal, Mesut Ozil ameonekana kuchoshwa na lawama za mashabiki wa Arsenal ambao ameamua kuwatolea uvivu.


Ozil raia wa Ujerumani, amesema anaamini amefanya vizuri katika soka kabla hajatua Arsenal na baada ya kutua katika kikosi hicho.

“Mafanikio yangu na Real Madrid kila mmoja anajua, mchezaji wa Ujerumani hadi Kombe la Dunia, inajulikana.

“Hapa Arsenal nilifunga mabao kadhaa, nikatoa pasi 20 zilizozaa mabao katika mechi zote. Sasa ajabu kabisa, timu ikifanya vibaya, ninawekwa pembeni na kupokea lawama zote.


“Kila ninapofanya vizuri inakuwa ni sisi, timu ikifanya vibaya ni mimi. Hii si sawa hata kidogo,” alisema akizungumza na kituo cha runinga cha ITV cha Uingereza.


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

Zitto: Tumejulishwa na NECTA Hakuna Rekodi za Daud Albert Batishe Wala Paul Makonda.Fahamu zaidi hapa.

Tumejulishwa Kwenye Kamati Kuwa Nacte Hawana Rekodi ya Albert Bashite Wala Paul Makonda..Yani Wote Hawapo kwenye Taarifa za NECTA

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

Rais Magufuli Afungua Mkutano Wa Mawaziri Wa Tanzania Na Uganda Ulioongelea Maendeleo Ya Mradi Wa Ujenzi Wa Bomba La Mafuta Ghafi Kutoka Hoima Hadi Tanga Fahamu zaidi hapa.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifungua kikao cha pamoja cha Mawaziri wa Serikali za Tanzania na Uganda pamoja na wadau kuzungumzia mradi wa ujenzi wa Bomba la Kusafirishia Mafuta Ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga.

Mkutano huo, uliofanyika Ikulu, Dar es salaam JANA  Jumanne Machi 28, 2017, ulihudhuriwa na Mawaziri wa Nishati na Madini pamoja na Mawaziri wa Ardhi wa nchi hizo mbili, Wanasheria wa Serikali  na kampuni washirika wa mradi huo Lake Albert (CNOOC, TOTAL na TULLOW).

Pamoja na mambo mengine, Mawaziri, Maafisa na Wataalam wa pande zote husika walikaa na kukubaliana kwamba rasimu ya  makubaliano rasmi ya kuanza kwa mradi yawe yamekamilika na kuwa tayari katika kipindi cha wiki mbili ili kuwezesha Marais wa Tanzania na Uganda kuweka jiwe la msingi kuashiria kuanza ujenzi wa kihistoria wa mradi huo wa bomba la mafuta kutoka Hoima nchini Uganda hadi Chongoleani mkoani Tanga, Tanzania.


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

Orodha Ya Majina Yaliyopitishwa Na Kamati Kuu CCM Kugombea Ubunge Afrika Mashariki.Fahamu zaidi link hapa.

Chama cha Mapinduzi (CCM) kimetangaza majina ya wanachama wake 12 walioteuliwa kugombea ubunge wa Bunge la Afrika Mashariki, uchaguzi unaotarajiwa kufanyika kwenye mkutano wa Bunge ujao.

Akisoma majina hayo leo wakati wa Mkutano na waandishi wa habari, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole amesema kuwa wameteua wananchama hao miongoni mwa wengi zaidi ya 400 waliokuwa wamechukua fomu kugombea nafasi hizo.

Mchanganuo
Miongoni mwa wabunge 9 watakaokwenda Bunge la Afrika Mashariki kuiwakilisha Tanzania, 6 watatoka CCM. Kufuatia idadi, hiyo CCM imesema kuwa itatoa wabunge watatu wa kiume na watatu wa kike ambapo miongoni mwao wanne watatokea Tanzania Bara na wawili watatokea Tanzania Visiwani.

Walioteuliwa kugombea nafasi hizo ni;

Wanawake Tanzania Bara;
  1.     Zainabu Rashid Mafaume Kawawa
  2.     Happiness Elias Lugiko
  3.     Fancy Haji Nkuhi
  4.     Happiness Ngoti Mgalula
Wanaume Tanzania Bara;
  1.     Dkt Ngwaru Jumanne Maghembe
  2.     Adam Omari Kimbisa
  3.     Anamringi Issay Macha
  4.     Charles Makongoro Nyerere
Wanawake Zanzibar;
  1.     Maryam Ussi Yahya
  2.     Rabia Abdallah Hamid
Wanaume Zanzibar;
  1.     Abdallah Hasnu Makame
  2.     Mohammed Yussuf Nuh
Miongoni wa wagombea hawa 12, Bunge litapiga kura kuchagua wabunge sita watakaoiwakilisha Tanzania kwenye Bunge la Afrika Mashariki kwa tiketi ya CCM.


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

Ajali mbaya ya Basi la Mwendokasi yatokea maeneo ya Fire.Fahamu zaidi hapa.

Ajali mbaya ya basi la mwendo kasi imetokea leo hii maeneo ya Fire jijini Dar es salaam.Haijajulikana bado nini chanzo cha ajali hiyo.


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

YANGA YAKWAMA KUWAPELEKA WAARABU UWANJA WA KIRUMBA.FAHAMU ZAIDI HAPA.

Kuna kila dalili Yanga itabaki jijini Dar es Salaam na kucheza na kikosi cha MC Alger kutoka Algeria.

Awali Yanga ilitaka kucheza mechi yake hiyo mjini Mwanza kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, mechi ambayo imepangwa kucheza Aprili 8.

Lakini masharti ya kufanya ukarabati, kuweka ofisi ndogo ya Caf na kadhalika, inaonekana kuifanya Yanga ibaki Dar es Salaam.

Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa naye amesema ni kama asilimia miaka wanaweza kuendelea kubaki.

“Nafikiri tutabaki, siwezi kusema tunawakimbia Mwanza lakini kuna mambo mengi yamejitokeza katikati.

“Kikubwa ni kwamba kuna mambo mengi ya ukarabati katika uwanja wa CCM Kirumba na hayajakamilika. Tutabaki Dar es Salaam na ikitokea siku nyingine, tunaweza kwenda Mwanza au kwingine kokote ambako tunajua Wanayanga wanastahili kuiona timu yao,” alisema.


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa