Tanzania imechangia asilimia 19.3 ya jumla ya wageni wa kimataifa
kupitia anga (international air arrivals) ukilinganisha na asilimia 18.2
ya Kenya, asilimia 17.2 Misri na asilimia 12.1 ya Afrika Kusini katika
kipindi cha kuanzia September 2016 hadi January 2017.
Takwimu hizi ni kwa mujibu wa ripoti mpya ya shirika la ufuatiliaji wa
masuala usafiri wa ndege, ForwardKeys ambayo hulinganisha ukataji tiketi
za ndege zaidi ya milioni 16 kila siku ili kuiweka Afrika kwenye ramani
ya utalii duniani.
Kwa jumla, Afrika Mashariki ina asimilia 16.4 ya ufikaji wa wageni kwa
njia ya anga. Na kwa ujumla pia, kuna ongezeko la asilimia 10.3 ya
ufikaji wageni Afrika
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment