Rapper Nay wa Mitego, Alhamis hii aliitikia wito wa Waziri wa
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt Harrison Mwakyembe kukutana
naye mjini Dodoma kwaajili ya kuzungumza namna ya kuuboresha wimbo wake
Wapo ambao licha ya kuikosoa vikali serikali pamoja na Rais Dkt John
Magufuli umepokelewa kwa mikono miwili.
Hatua hiyo ilikuja baada ya Rais Magufuli kuamuru kuachiwa huru kwa
Nay ambaye alikuwa amekamatwa na polisi na wimbo wake kufungiwa na
BASATA. Akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma, Dkt Mwakyembe
alisema wasanii wana nafasi kubwa katika kuisaidia serikali kukemea
mambo maovu.
Amewataka vijana kutambua kuwa Tanzania ni nchi inayozingatia
utawala wa sheria na kwamba wana uhuru wa kukosoa bila kutukana au
kwenda nje ya maadili. “Na ndio maana tukasema kwa wimbo wa Nay hapana,
hebu ngoja tuusikie, mbona ni wimbo mzuri tu,” alisema Mwakyembe.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment