Staa wa filamu Bongo, Wema Sepetu anatajwa kuhusika na majanga
yanayomkumba Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda kufuatia yale ambayo
amekuwa akiyafanya tangu atajwe kwenye listi ya wanaotumia madawa ya
kulevya.
Makonda tangu ajiingize kwenye vita dhidi ya madawa ya kulevya,
amekumbana na changamoto nyingi ikiwepo kuibuliwa kwa madai kuwa vyeti
vyake vina walakini na ‘kung’ang’aniwa’ na jamii ya waandishi wa habari
baada ya kuvamia katika Studio za Clouds Media akiwa na askari wenye
silaha.
Majanga haya yanadaiwa kuwafanya wale wabaya wake kuchekelea huku Wema akitajwa kuwa mmoja wao.
KIVIPI?
Wema alitajwa kwenye listi hiyo Februari 2, mwaka huu na kutakiwa
kuripoti kwenye Kituo Kikuu cha Polisi ‘Sentro’ wakiwemo mastaa wengine
ambapo yeye alionekana kutofurahishwa na kitendo hicho hivyo ikadaiwa
kuwa, manung’uniko yake huenda yamechangia Makonda kuandamwa na majanga.
TASBIHI YAHUSISHWA
Aidha, mara baada ya Wema kutajwa kwenye listi hiyo kisha soo
kwenda polisi na hatimaye kupandishwa kizimbani, mdada huyo mara kadhaa
anapokwenda mahakamani amekuwa na kitu kinachoitwa tasbihi (angalia
picha ndogo ya Wema ukurasa wa mbele sehemu iliyozungushiwa) ambacho
kinatajwa kuwa na nguvu ya kumuweka mtu mbali na matatizo lakini pia kwa
wale wenye nia ya kutaka upatwe na majanga, yanaweza kuwarudia.
TASBIHI NI NINI?
Hiki ni kifaa chenye vitu vya mviringo vilivyochomekwa kwenye uzi
ambacho Waislam hukitumia kwenye kufanyia ibada. Akizungumza na Ijumaa,
ustaadhi mmoja aliyeomba jina lake lisitajwe gazetini alisema kuwa,
tasbihi inapoombewa kisha ukawa unatembea nayo na kuitumia kiibada, inao
uwezo wa kukuepusha na mabalaa lakini pia inao uwezo wa kuwafanya
wanaokuombea mabaya, yawarudie.
“Unajua haya mambo ni ya kiimani sana, tasbihi kiimani ina nguvu
kubwa kama utaitumia vizuri, wapo mashehe wanaoweza kuisomea ile kisha
ukapewa na ukawa unatembea nayo, kama umeiva kiimani mabaya hayawezi
kukupata lakini wabaya wako yatawafika kwa uwezo wa Mungu,” alisema
ustaadhi huyo.
WEMA NA MAKONDA
Licha ya maelezo hayo, baadhi ya watu kwenye mitandao mbalimbali
wamekuwa wakidai kuwa, huenda lile chozi la Wema na watu walio nyuma
yake lina nafasi kwenye haya mabalaa yanayompata Makonda licha ya kwamba
huenda yametokea kwa mipango ya Mungu tu.
“Wema lazima huko aliko atakuwa anafurahia yanayomkuta Makonda,
inawezekana kweli anatumia hayo madawa ya kulevya kama ilivyodaiwa
lakini huenda kwa yeye ambaye amekuwa nao karibu sana alitaka busara
itumike kwenye kumtaja.
“Yawezekana nia ya Makonda ilikuwa njema ya kumtaka kumsaidia Wema
aondokane na tatizo hilo lakini ‘approach’ iliyotumika ni wazi
haikumfurahisha na ndiyo maana inawezekana sana na yeye alikuwa akiombea
yamfike kiongozi huyo,” alidai Husna Juma, mkazi wa Sinza, Dar.
KISOMO NACHO CHAHUSISHWA
Aidha, wapo waliounganisha yanayomkuta Makonda sasa hivi na kisomo
alichokifanya Wema nyumbani kwa mama yake, Sinza jijini Dar ambacho
nacho kiimani kinatajwa kuwa kina nguvu ya kumfanya anayeombewa
kuepushwa na shari na wanaomuombea shari, iwarudie.
USAHIHI
Hata hivyo, usahihi kamili ni kwamba unapofanya kisomo lengo ni
kumuomba Mungu akujaalie kila la kheri na kukuepushia kila shari lakini
huwezi kuomba maaalum ili kumuombea f’lani mabaya. Kwa maana hiyo
wanaodhani kisomo alichofanya Wema K inahusika moja kwa moja kwenye
majanga yanayompata Makonda watakuwa wanakosea.
WEMA ANASEMAJE?
Ijumaa lilifanya jitihada za kumpata Wema ili kuzungumzia madai
kwamba sononeko lake linahusika katika haya yanayompata Makonda lakini
simu yake iliita bila kupokelewa na hata alipotumiwa SMS, hakujibu.
Hata hivyo, kuonesha kuwa hamfagilii Makonda bali yuko upande wa
Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima, staa huyo ambaye
hivi karibuni alijiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)
alitupia kwenye ukurasa wake wa Instagram picha ya Gwajima kisha kuweka
maneno yaliyosomeka:
“Huyu ni kati ya wanaume ninaowapenda kwa sasa.”
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment