Askofu wa kanisa la Ufufuo na Uzima Ministries, Josephat Gwajima amesema
Jumapili hii atatembelewa na wachekeshaji Kitale ‘Mkudesimba’ pamoja na
Stan Bakora.
Gwajima amekuwa akitamka mara kadhaa kwamba anavutiwa na wachekeshaji
hao ambao wamekuwa maarufu kutokana na vichesho vyao ambavyo vilikuwa
vinarushwa kupitia redio ya EFM.
Jumamosi hii mchungaji huyo ambaye amekuwa akizuru katika vituo
mbalimbali vya redio kutoa pole kuhusiana na tukio la RC Makonda kuvamia
kituo cha Clouds Media siku chache zilizopita, ametoa taarifa ya
kutembelewa kanisani kwake na wachekeshaji hao.
“Tutakuwa na ugeni wa waigizaji na wachekeshaji wawili rafiki yangu
Mkude Simba (Kitale) na Stan Bakora watapata nafasi ya kuperform live
pia, kwa niaba ya familia ya Ufufuo na Uzima tunawakaribisha. Ufufuo na
uzima tunasapoti vipawa mbalimbali ambavyo watu wamepewa na Mungu,”
aliandika Gwajima Instagram.
Askofu huyo amekuwa gumzo katika mitandao ya kijamii hivi karibuni baada
ya kutajwa kwenye sakata la dawa za kulevya na RC Makonda.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment