Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni Susan Kaganda, amesema kuwa
yeye hakutoa maelekezo ya kuzuia mkutano wa aliyekuwa Waziri wa Habari,
Sanaa, Utamaduni na Michezo Nape Nnauye pamoja na Waandishi wa Habari
Jana Protea Hotel.
Akifafanua kupitia kipindi cha Maisha Mseto cha Times Fm mapema Leo
asubuhi, Susan amedai yeye kama Kamanda hana mamlaka ya kuingilia
biashara binafsi (Protea Hotel), na alikwenda pale kuhakikisha Usalama
unaimarika zaidi na si vinginevyo.
“Protea ni private Hotel sio Mali ya Serikali, ile ni Biashara huru
kamanda hawezi kuzuia, lakini nilikuta Waandishi wengi pale na alipata
fursa ya kuongea nao.
” Mimi kazi yangu ni kusimamia Usalama wa Raia na Mali zao, mkutano unanihusu ukiwa wa Hadhara” alisema RPC Susan.
Alipoulizwa kuhusiana na kipande cha ‘Picha Jongefu’ (video)
inayomuonyesha mtu anayedhaniwa kuwa Askari akimtolea silaha Nape
Nnauye, amesema hawezi kuliongelea swala hilo kwa sasa mpaka uchunguzi
utakapokamilika kwa maana kipande hicho hakionyeshi Sura ya mtu Huyo.
“Jeshi la Polisi tunawafundisha Askari wetu kutumia nguvu kwa namna
wanavyokutana na mazingira, sikuwepo sikuona nilielezwa na ndio maana
nilikwenda nikamuuliza Mh uko sawa akanijibu yuko salama,”
“Lakini kama kuna Silaha imetumika kama ambavyo nimeona kwenye vyombo
vya Habari tunalifanyia Uchunguzi, sikuwepo eneo la tukio picha ile
inaonyesha KISOGO, kuwa mtulivu tunachunguza” alifafanua.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment