Malaria ni nini? Malaria ni ugonjwa wa kuambukizana unaoletwa na chembe
chembe zinazoitwa plasmodium.Chembe chembe hizi huingia ndani ya mwili
wa binadamu baada ya kuumwa na mbu wa kike kwa jina Anopheles. Mbu
mwenye chembe chembe za plasmodium anapomuuma mtu,humuingizia baadhi ya
mate yenye viini vya kuambukizana kwenye kidonda hivyo kusabaza Malaria.
Viini hivi husafiri hadi kwenye maini ambapo hukaa hadi vifikie
ukomavu. Viini hivi baadaye huingia na mtu kama huyu akiumwa na mbu,mbu
huyu hubeba chembe chembe hizi na anaweza kumuambukiza mtu atakaye
muuma.
Kuna aina 4 za Malaria: P. vivax, P. malariae, P. ovale na P.
falciparum. Zimepewa majina kulingana na aina ya plasmodium
inayozisababisha. Aina 3 za kwanza sio hatari lakini Falciparumni hatari
sana na hata inaweza kusababisha kifo. Hii ni kwa sababu ikishaingia tu
mwilini huzaana kwa wingi ndani ya damu.. Hii ni kwa sababu chembe
chembe nyekundu za damu(ambazo husambaza oksijeni mwilini)zilizoadhirika
huwa nzito na haziwezi kuingia kwenye kapilari. Hii husababisha kufa
kwa sehemu ya ubongo,maini,mapafu,figo na matumbo kwa sababu ya ukosefu
wa oksijeni. Hali hii inaweza kusababisha kifo kama haita tibiwa haraka.
Malaria hutambulika vipi?
Baridi,kuuma kwa misuli na kichwa zinaweza kuwa dalili za magonjwa mengi
mengine. Njia ya pekee unayoweza kudhihirisha kama una Malaria ni
kuenda hiospitalini kupimwa damu. Watu wengi wanaotoka sehemu
zilizoadhirika na Malaria pindi wanapoona dalili hizi huenda kwenye
maduka ya kuuza madawa kununua dawa za kupambana na Malaria. Huu sio
ushauri mzuri. Ni muhimu kupimwa damu ili aina ya plasmodium
inayosababisha maradhi yako itambulike na upewe matibabu yanayostahili.
Nani yuko kwenye hatari ya kuambukizwa Malaria?
Watoto wachanga,watoto na akina mama waja wazito wako kwenye hatarikubwa
ya kushambuliwa hata kufa kutokana na Malaria. Watoto wachanga na
watoto wako kwenye hatari kwa sababu wameambukizwa mara chache
nahawajajenga
kinga dhidi ya chembechembe hiziVamizi la Malaria kwa wanawake
wajawazito kalikwa sababu kinga yao dhidi ya maradhi huwa chini wakati
wa uja uzito. Malaria huongeza tishio kwa mtoto ambaye hajazaliwa kama
kuzaliwa kabla ya wakati
kutimia, uaviaji wa mimba, maambukizi ya sehemu za siri, uzani mdogo wa
mtoto anapozaliwa, kupoteza uja uzito na pia ugonjwa huu unaweza
kumsababishia mama kifo.
Naweza jilinda vipi dhidi ya Malaria?
Msafiri: Kama unasafiri hadi kwenye eneo linalolotambulika kwa
Malaria,mtembelee daktari wako ili akupe dawa mahsusi ya kupambana na
Malaria ya eneo unalotembelea.Hakikisha umefuata maelezo vizuri.
Wenyeji wa maeneo yalioadhirika na Malaria: Mbu wa aina ya anopheles
hupenda kuuma watu nyakati za macheo na machweo kwa hivyo ni bora
kujikinga nyakati hizi.Wakati wa machweo unaweza keti ndani ya nyumba
iliyoekewa dawa na usiku unaweza kulala neti iliyotibiwa.
Haribu sehemu mbu wanapozaliana: Kipindi cha mwisho katika ukuaji wa mbu
hufanyika majini.Mbu wa aina ya anopheles hupendelea maji yasiyo ya
chumvi.Ni muhimu kuharibu ama kunyunyuzia na dawa sehemu zote ambazo mbu
wanaweza kutaga mayai.Unafaa kutoa chupa,ndoo ama chochote ambacho
kinaweza kusimamisha maji,bacillus thuringiensis(Bti) dawa asili ya kuua
wadudu kutoka BioVision inaweza kutumiwa kuua mbu wachanga bila
kuharibu maji.
Watoto na mama waja wazito lazima wakingwe na Malaria: Nchini
Kenya,wanawake waja wazito wana haki ya kupata matibabu 2 ya bure na
neti zilizotibiwa. Chukua moja kutoka katiki kliniki yako.
Neti zilizotibiwa: Kila mtu anapaswa kupata neti iliyotibiwa.Kuna aina
mbili ya neti hizi nchini Kenya ambazo zinauwa mbu pindi tu wadudu hawa
wanapozigusa.Kuna zile zinazopaswa kutibiwa kila baada ya miezi 6nba
PowerTabs na zile zinazodumukwa miaka 3 hadi 5 baada ya kutibiwa
Ni zipi dalili za Malaria?
Dalili za Malaria ni kama zile za Flu; homa, baridi na kuuma kwa misuli
na kichwa. Watu wengine hupatwa na kichefuchefu, kutapika na kuharisha.
Vipindi vya baridi, homa na kutokwa na jasho hujirudia kila siku moja,
mbili au tatu. Watu wenye aina ya P. falciparum wanaweza kupata Malaria
ya ubongo ambayo husababisha kuishiwa na fahamu ama kuchanganyikiwa
kiakili.
Tiba ya Malaria
Tiba ya Malaria inategemea mambo kadhaa:
Hali ya mgonjwa (mtoto, mama mja mzito, mtu mzima, ni kali ama sio kali)
Nguvu ya dawa dhidi ya ambukizo la viini vya plasmodium.
Eneo la kijiografia ambalo mtu aliambukizwa. Kwa mfano,
P.falciparuminayopatikana katika nchi za Mashariki ya kati inaweza
kutibiwa na dawa ya chloroquine, lakini inayopatikana Africa, katika
nchi zilizo kusini mwa jangwa la Sahara haitibiki kwa chloroquine.
Aina ya plasmodium inayodhuru mgonjwa. Malaria yasiyo makali hutibiwa na
dawa za kumeza ilhali wagonjwa wenye P. falciparum kali hulazwa
hospitalini na kupewa sindano ya maji.
Kwa bahati mbaya aina fulani za plasmodium zimeleta upinzani dhidi ya dawa ya chloroquine.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment