DAR ES SALAAM Skendo ya mjini iliyotapakaa mjini na kwenye mitandao ya
kijamii inamgusa modo maarufu Bongo, Hamisa Mobeto akidaiwa kujichora
‘tatuu’ ya mwanamuziki maarufu Bongo, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’,
ishu iliyosababisha mwandani wa jamaa huyo, Zarinah Hassan ‘Zari The
Boss Lady’ kumporomoshea matusi.
Kuhusu sakata hilo, mama mzazi wa Mobeto ameshindwa kujizuia na kujikuta
akimtolea povu Zari juu ya mwanaye huyo. Akizungumza na gazeti hili kwa
uchungu alipoulizwa kuhusu sekeseke hilo la mwanaye, mama Mobeto
alisema kuwa, hakuna wakati mgumu kama kuona mtoto wake huyo
anazungumziwa vibaya kila wakati katika mitandao ambapo wakati mwingine
siyo jambo la kweli zaidi ya kumchafua tu.
“Jamani mimi kama mzazi, sidhani kama kuna mzazi yeyote anayeweza
kuvumilia kuona mwanaye kila mara yuko kwenye midomo ya watu au
kuongelewa vibaya kwenye mitandao ya kijamii kwa vitu ambavyo
hajafanya,” alisema mama Mobeto. Alifunguka kuwa, habari ambayo
imesambaa kuhusu mwanaye kujichora tatuu ya Diamond, anaona ni mambo
ambayo hayana msingi wowote zaidi ya kumchafua na kumdhalilisha mwanaye.
“Unajua unapomuona Hamisa (Mobeto) amenyamaza, kila wakati wanatafuta
kumuwekea jambo baya, kitu ambacho siyo sahihi, mimi sijawahi kuiona
hiyo tatuu wanayosema zaidi ya kuona kuwa wanampandikizia maneno tu ya
kumchafua, sipendezwi kabisa na tabia hiyo,” alisema mama Mobeto.
Hivi karibuni Zari alimtolea matusi Mobeto kupitia mitandao mbalimbali
ya kijamii akimtahadharisha juu ya habari zilizozagaa kuwa, huwa
anachepuka na Diamond kwa siri hasa mwanamama huyo anapokuwa nyumbani
kwake, Afrika Kusini na kumwacha baba watoto wake huyo jijini Dar.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment