Timu
ya taifa ya mpira wa miguu ya vijana wenye umri wa miaka 17 maarufu kwa
jina la Serengeti Boys imetumia ndege ya Shirika la Ndege la Tanzania
(ATCL) kutoka Dar es Salaam alfajiri ya leo Machi 26, mwaka huu na kutua
Bukoba mkoani Kagera kwa kambi ya wiki moja.
Serengeti
Boys itakuwa kambini Bukoba hadi Aprili 2, mwaka huu ambako inatarajiwa
kucheza michezo miwili ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya timu vijana ya
Burundi kwenye Uwanja wa Kaitaba, mjini Bukoba mkoani Kagera. Michezo
hiyo itafanyika Machi 30, 2017 na kurudiana Aprili mosi, mwaka huu.
Serengeti
Boys ambayo inajiandaa na michuano Afrika huko Gabon itarejea Dar es
Salaam Aprili 2, mwaka huu ambako imepangwa kucheza na Ghana Aprili 3,
mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Mchezo huo utatanguliwa
na hafla ya kuagwa kwa kukabidhiwa bendera.
Timu
itaelekea Morocco Mei 5, mwaka huu baadaye itapita Cameroon kwenye
kambi ya zaidi ya mwezi mmoja baadaye itakwenda Gabon katika michuano
itakayoanza Mei 14, 2017. Ikiwa Cameroon itacheza mechi mbili za
kimataifa dhidi ya wenyeji kabla ya kwenda kwenye fainali.
Serengeti
Boys ni timu ya vijana ambayo imefuzu kwa fainali za Kombe la Mataifa
ya Afrika zitakazofanyika Gabon kuanzia Mei 14, mwaka huu. Timu hiyo
imepangwa Kundi ‘B’ pamoja na mabingwa watetezi Mali, Niger na Angola.
Ina lengo la kurejea na Kombe la Afrika kwa vijana.
La
ikitokea imekosa nafasi hiyo angalau ikafika nusu fainali ambako kwa
mafanikio hayo itakuwa tayari ina tiketi mkononi ya kucheza fainali za
Kombe la Dunia huko India, Novemba, mwaka huu.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment