Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ndege la ATCL, Lasislaus Matindi
amesema wamefanikiwa kukusanya shilingi Bilioni 9 kwa miezi minne tu kwa
kutumia ndege hmbili zilizonunuliwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli.
Kipindi ndege hizo zinanunuliwa baadhi ya watu walikosoa kuwa hazikuwa na tija kwa Taifa.
Kampuni ya Ndege ya Tanzania (ATCL) ilianzishwa mwezi Novemba 2002 baada
ya Serikali kubinafsisha lililokuwa Shirika la Ndege la Tanzania (Air
Tanzania Corporation, ATC). katika Shirika hilo, Shirika la Ndege la
Afrika Kusini (SAA) lilinunua hisa asilimia 49 ndani ya ATC.
Hata hivyo ubia kati ya ATCL na SAA ulikabiliwa na matatizo ya
kiuendeshaji na kulazimika kusitishwa mwezi Agosti 2006 na ATCL
kurejeshwa tena serikalini kwa asilimia 100.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment