Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa ametinga kwenye mgodi wa dhahabu wa Buzwagi uliopo
Kahama mkoani Shinyanga na kuchukua sampuli za mchanga kwa lengo la
kwenda kuyapima kwa wataalamu wa madini ili kubaini kiasi cha dhahabu
kilichomo.
Amesema
wanataka kuona mchanga unaosafirishwa na mwekezaji huyo una kiasi gani
cha dhahabu, pia Serikali inataka kufahamu kama kodi inayolipwa ni
sahihi.
“Tumeamua
kuchukua sampuli za mchanga ambao mwekezaji anasema wanaupeleka nje ya
nchi kwa ajili ya kwenda kutenganisha madini ya dhahabu na shaba. Hata
hivyo nimemuhoji kwa nini mitambo hiyo isiletwe nchini ili kila kitu
kifanyike hapahapa,” Amesema Majaliwa
Waziri
Mkuu amesema sera ya uwekezaji inasema mtambo huo unatakiwa uwepo
nchini ili kila hatua ya uchenjuaji ifanyike hapa hapa, hivyo tunataka
kujiridhisha na mwenendo wa mwekezaji na mapato tunayoyapata kama
yanastahili.
Aliongeza kwamba “Hili
lipo miongoni mwa masharti ya uwekezaji kwenye sekta ya madini nchini
kwamba mitambo hiyo ije kujengwa hapa nchini na itaongeza fursa ya ajira
na kukuza sekta nyingine ikiwemo ya kilimo,”.
Kuhusu uzalishaji mgodini hapo
Kwa
upande wake Meneja Uendelezaji wa mgodi huo Bw. George Mkanza alisema
mgodi huo ulionzishwa mwaka 2009 umeajiri watumishi 720 pamoja na
vibarua 500.
Alisema
kwa siku wanachenjua makontena matatu hadi sita ambapo katika kila
kontena moja wanapata kilo tatu za madini ya dhahabu na tani nne za
madini ya shaba.
Bw.
Mkanza alisema wanazalisha asilimia 50 ya madini ya dhahabu na asilimia
50 ya dhahabu iko kwenye mchanga na inakuwa imechanganyika na madini ya
shaba ambayo ndiyo unaosafirishwa kwenda nje ya nchi kwa ajili ya
kutenganishwa.
“Hapa
Buzwagi tuna makontena 179, makontena mengine 152 yako Dar es Salaam
kwenye bandari kavu ya Nazam na 21 yako bandarini. Kila siku
tunapoendelea kuzalisha tunakuwa na makontena manne hadi sita. Ndugu
zetu wa Bulyanhulu nao wanamakontena 108 yako mgodini na 104 yako Nazam
Cargo Dar es Salaam,” alisema.
==>Video ya tukio hilo
==>Video ya tukio hilo
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment