Timu
ya taifa ya Tanzania chini ya miaka 17, Serengeti Boys, leo imeibuka na
ushindi mnono wa mabao 3-0 dhidi ya vijana wenzao wa Burundi katika
mchezo wa kirafiki uliopigwa kwenye Uwanja wa Kaitaba, Kagera.
Katika
mchezo huo ambao Serengeti Boys inautumia kwa ajili ya maandalizi yao
kabla ya kwenda Gabon kushiriki michuano ya Kombe la Mataifa Afrika kwa
vijana chini ya miaka 17, ulishuhudiwa mpaka mapumziko timu hiyo ikiwa
mbele kwa mabao 2-0.
Mabao
hayo yalifungwa na Muhsin Makame dakika ya 20 na Nickson Kibabage, huku
Yohana Mkomola akimalizia msumari wa mwisho dakika ya 72 kwa njia ya
mkwaju wa penalti na kukamilisha idadi hiyo ya mabao 3-0.
Baada
ya leo kumalizana na Burundi, Jumatatu ijayo kikosi cha Serengeti Boys
kinatarajiwa kucheza mchezo wa mwisho wa kirafiki jijini Dar es Salaam
dhidi ya Ghana kabla ya kwenda Morocco kuweka kambi ya mwisho ya
kujiandaa na michuano hiyo ya vijana.
Katika michuano hiyo itakayoanza kuunguruma Mei 14, mwaka huu, Serengeti Boys imepangwa Kundi B sambamba na timu za Mali,
Niger na Angola. Kama Serengeti Boys itafanya vizuri kwenye michuano
hiyo, basi itajikatia tiketi ya kwenda kushiriki michuano ya Kombe la
Dunia chini ya miaka 17 itakayofanyika hapo baadaye nchini India.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment