Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifungua
kikao cha pamoja cha Mawaziri wa Serikali za Tanzania na Uganda pamoja
na wadau kuzungumzia mradi wa ujenzi wa Bomba la Kusafirishia Mafuta
Ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga.
Mkutano
huo, uliofanyika Ikulu, Dar es salaam JANA Jumanne Machi 28, 2017,
ulihudhuriwa na Mawaziri wa Nishati na Madini pamoja na Mawaziri wa
Ardhi wa nchi hizo mbili, Wanasheria wa Serikali na kampuni washirika
wa mradi huo Lake Albert (CNOOC, TOTAL na TULLOW).
Pamoja
na mambo mengine, Mawaziri, Maafisa na Wataalam wa pande zote husika
walikaa na kukubaliana kwamba rasimu ya makubaliano rasmi ya kuanza kwa
mradi yawe yamekamilika na kuwa tayari katika kipindi cha wiki mbili
ili kuwezesha Marais wa Tanzania na Uganda kuweka jiwe la msingi
kuashiria kuanza ujenzi wa kihistoria wa mradi huo wa bomba la mafuta
kutoka Hoima nchini Uganda hadi Chongoleani mkoani Tanga, Tanzania.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment