Kocha
Mkuu wa Taifa Stars, Salum Mayanga, amefunguka kuwa, beki wa kati wa
timu hiyo, Erasto Nyoni kwa sasa ndiye beki bora kwake kuliko wengine
wanaocheza nafasi hiyo akiwemo Kelvin Yondani anayekipiga kwenye Klabu
ya Yanga.
Mayanga
ametoa kauli hiyo baada ya juzi Jumamosi kumpa nafasi Erasto
anayekipiga kwenye Klabu ya Azam kucheza mechi ya kirafiki ya kimataifa
dhidi ya Botswana kwenye Uwanja wa Taifa, Dar na Taifa Stars kuibuka na
ushindi wa mabao 2-0 yaliyofungwa na Mbwana Samatta dakika ya pili na
87.
Akizungumzia
umuhimu wa Erasto kwenye kikosi chake, Mayanga amesema: “Kiufundi
namwamini sana Erasto na ndiyo maana nimemwita kwenye kikosi changu,
lakini nafahamu nina idadi kubwa ya vijana wanaocheza kwenye safu ya
ulinzi anayocheza yeye na sijawaita kutokana na sababu zangu binafsi.
“Sababu
hasa iliyonifanya nimchukue Erasto, kwanza nilihitaji beki wa kati
mzoefu, mrefu na mwenye uwezo wa kucheza nafasi zaidi ya moja uwanjani,
ukiangalia sifa hizo zote yeye anazo, hivyo kiufundi kwangu Erasto ni
bora kwa sasa.
“Ninachowaomba
Watanzania tuwaunge mkono wachezaji wetu na si kuwakatisha tamaa kwa
sababu Tanzania ni ya wote na mwalimu anaangalia kwa wakati husika nani
anafaa katika kuipigania timu."
SOURCE: CHAMPIONI
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment