1. Wakikosa attention yako. Wasichana hupenda pale wanapofahamu kuwa 
unawasikiliza na unafahamu nini wao wanahitaji. Kama kutakosekana 
mawasiliano mazuri na atagundua hilo atauona uhusiano huo haumtimilizii 
haja zake. Hata kama kila kitu kinaenda sawa. Msikilize anapoongea. Kama
 akiona hapati penzi analolihitaji atatafuta mwingine ambaye yupo tayari
 kumtimizia.
2. Kumuheshimu. Msichana huwa anajitoa sana awapo katika mahusiano hivyo
 anategemea mvulana uheshimu hata kwa chochote kidogo anachokufanyia. 
Mfanye agundue kuwa umeheshimu kile ambacho amekufanyia.
3. Usaliti. Unaposaliti inamaanisha kuna kitu hakipo sawa katika 
mahusiano yako hata kama una uwezo wa kushughulikia lakini wewe unaona 
njia sahihi ni kutoka nje kuwa na mahusiano na msichana mwingine 
ukidhani ndio unarekebisha. Pale msichana wako akikukamata unamsaliti 
fahamu hawezi kuvumilia naye atakuacha.
4. Ukosefu wa hisia za kimapenzi. Msichana hupenda kuona kuwa wanapendwa
 wanathaminwa na wapenzi wao wanawajali sasa wakiona kuwa hakuna 
conection ya hisia za kimapenzi kutoka kwa mvulana wake huona kuwa 
hakuna mapenzi ya kweli katika uhusiano aliopo
5. Hawapendi kusikia kuhusu mapenzi mara kwa mara wasichana hupenda 
kutumia muda mrefu na wapenzi wao bila kusikia neno la kuwataka wafanye 
mapenzi kama ukiwa nao na ukawataka kimapenzi mara kwa mara watakuwa 
wanakuavoid hata utakapokuwa ukiwagusa.
6. Unapomcontrol sana
msichana humpenda mvulana atakayemlinda na kujiona yupo sehemu salama sio kumdhibiti kufanya mambo yake mengine anapenda uhuru.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
 









 




 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
0 comments:
Post a Comment