Waziri
Mkuu wa Ethiopia, Hailemariam Dessalegn anatarajiwa kuwasili nchini
kesho, Machi 31 kwa ziara ya kitaifa ya siku mbili kufuatia mwaliko wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph
Magufuli.
Hayo
yalisemwa jana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano Afrika
Masharika, Dkt. Suzan Kolimba alipokuwa Akizungumza na waandishi wa
habari.
Alisema
kuwa ziara ya Waziri Mkuu wa Ethiopia, Dessalegn imetokana na mkutano
kati yake na Rais Dkt. Magufuli uliofanyika baada ya mkutano wa kawaida
wa 28 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika uliofanyika hivi
karibuni huko nchini Ethiopia.
Alisema
kuwa madhumuni ya ziara hiyo ni pamoja na kukuza mahusiano mazuri
yaliyopo baina ya Tanzania na Ethiopia pamoja na kujadili fursa zaidi
za ushirikiano katika maeneo mbalimbali ikiwemo uwekezaji na biashara.
“Mahusiano
ya Tanzania na Ethiopia ni mazuri, Ethiopia imeonesha nia ya kufungua
Ubalozi wake hapa nchini hivi karibuni. Kwa sasa Ethiopia inawakilishwa
nchini na Balozi wake aliyepo Nairobi nchini Kenya” alisema Naibu Waziri Kolimba.
Wakati
wa ziara hiyo,Waziri Mkuu wa Ethiopia, Dessalegn atakutana na Rais Dkt.
John Magufuli kwa mazungumzo, watashuhudia uwekwaji saini wa mikataba
ya ushirikiano kwenye maeneo mbalimbali kabla ya kuzungumza na Waandishi
wa Habari.
Aprili
01 mwaka huu, Waziri mkuu huyo wa Ethiopia atatembelea Mamlaka ya
Bandari Tanzania (TPA) na kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa
Bandarini hapo, Dessalegn na ujumbe wake wataondoka siku hiyo hiyo
kurejea Ethiopia.
Hata
hivyo, Mwaka 2015 Waziri Mkuu wa Ethiopia, Dessalegn alitembelea
Tanzania na kushiriki uzinduzi wa Kiwanda cha kutengeneza dawa za kuua
viluwi luwi vya mbu wanaoeneza Malaria kilichojengwa Kibaha, Pwani kwa
ufadhili wa Serikali ya Cuba.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment