Kuna habari zilizoko chini ya viunga vya watawala zinasema watu wa
‘’kitengo’’ wameamua kulifanyia kazi suala la Mchungaji Gwajima, Clouds
Media International na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kwa
sababu halitoi afya njema kisiasa.
Kwa kifupi, ‘’kitengo’’ ni neno ambalo kwa kiingereza ni ‘’The ruling
class/The Establishment’’. Hawa ni watu ambao moja ya kazi zao ni
kutathmini kwa kina hali ya kisiasa, kiuchumi na kiulinzi nchini halafu
baadaye hutoa mwelekeo kwa taasisi zinazohusika.
Kwa hiyo kuna uwezekano mkubwa hatutaweza kumsikia tena Mchungaji Gwajima akimzodoa Makonda katika mahubiri yake kanisani.
Ieleweke kuwa baada ya Uchaguzi Mkuu 2015 kumalizika, watu wa
‘’kitengo’’ walifanya tathmini na kubainisha watu ambayo wataweza
kufanikisha mikakati ya kisiasa kwa CCM na kiuchumi kwa serikali katika
mikoa ambayo inaonekana ni muhimu sana kisiasa na kiuchumi. Mikoa hiyo
muhimu sana ilipelekewa viongozi ambao watafanikisha mikakati hiyo na
mojawapo ni Mkoa wa Dar es Salaam.
Kwa wale wanadhani Makonda ataondolewa hivi karibuni katika Mkoa wa Dar
es Salaam, nadhani wataendelea kusubiri sana mpaka pale watu wa
‘’kitengo’’ watakapo jiridhisha kuwa kazi waliyomtuma ameshindwa
kuifanya au makosa anayofanya ni makubwa kiasi kwamba yanaondoa hata
madhumuni makuu ya uwepo wake kama Mkuu wa Mkoa.
Nimalizie kwa kusema, Mkuu wa taasisi ya watu wenye ‘’suti nyeusi’’
ametoa onyo kali kwa vijana wake kwa yaliyotokea Clouds Media
International na kwa Nape Nnauye kwa sababu kazi waliyopewa ni kumlinda
Mkuu wa Mkoa na sio yeye Mkuu wa Mkoa awape kazi za kufanya nje ya
misingi yao ya kazi. Ieleweke kuwa baada ya kufanyika uchunguzi wa kina
kiulinzi ilibainika Makonda anatakiwa kuboreshewa ulinzi.
Msishangae sana kwa nini Nape Nnauye ameamua kuwa kimya kuhusiana na
kadhia ya kutishiwa bastola. Ameelezwa ukweli wa hali halisi
iliyopelekea kitendo hicho kutokea.
Mjumbe hauwawi! Naiwakilisha jinsi ilivyo!
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment