MZAZI mwenziye na Mwanamuziki Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’,
Siwema Hudson amesema kitendo cha serikali kumpa kashikashi kutokana na
wimbo wake wa Wapo hakikumshangaza kwani alitarajia hayo yatokee kwa
kuwa zilipendwa wake huyo ni mtu wa kukurupuka.
Akizungumza na gazeti hili juzi baada ya Nay kutoka polisi, Siwema
alisema yeye amekaa na Nay kwa muda mrefu na mara nyingi akiamua jambo
ndiyo hivyo wala hakuna mtu anayeweza kumshauri.
“Unajua Nay anapenda kukurupuka na wala hataki mtu apinge wazo lake,
kama ameamua kufanya kitu anafanya tu na nilifahamu kuwa ipo siku hilo
lingemtokea, sasa kama limepita anatakiwa kujitathmini upya,” alisema
Siwema
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment