Rais
John Pombe Magufuli amewapandisha vyeo maafisa sita wa Uhamiaji kuwa
Makamishna kuanzia februari 28, mwaka 2017 na kuwateua kushika nyadhifa
mbalimbali katika Jeshi hilo.
Wateule
hao ni Mrakibu wa Uhamiaji (SI) Edward Peter Chogero kuwa Kamishna wa
Divisheni ya Fedha na Utawala pamoja na Mrakibu Mwandamizi wa Uhamiaji
(SSI) Samwel Rhobby Magweiga kuwa Kamishna wa Divisheni ya Udhibiti na
Uongozi wa Mipaka.
Wengine
ni Mrakibu Mwandamizi (SSI) wa Uhamiaji Gerald John Kihinga kuwa
Kamishna wa Divisheni ya Pasipoti na Uraia, Mrakibu Mwandamizi wa
Uhamiaji (SSI) Musanga Mbusuro Etimba ambaye anakuwa Kamishna wa
Divisheni ya Hati za Ukaazi na Pasi.
Aidha Mrakibu Mwandamizi wa Uhamiaji (SSI) Hennerole Morgan Manyanga ameteuliwa kuwa Kamishna wa Divisheni ya Sheria.
Rais amemteua pia naibu Kamishna wa Uhamiaji Mourice David Kitinusa kuwa Kamishna Chuo cha Uhamiaji cha kikanda (TRITA)
Kwa
mujibu wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani, Meja Jenerali
Projest Rwegasira, amesema kuwa uteuzi huo unaanzia februari 28, mwaka
2017.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment