Ukiwa shujaa wenzetu wanakupa heshima na hiki ndicho kilichotokea kwa mshambuliaji nyota wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo.
Serikali
ya kisiwa cha mji wa Madeira nchini Ureno imeamua kubadili jina la
Uwanja wake wa Ndege kutoka “Madeira Airport” na kuwa Uwanja wa Ndege wa
Cristiano Ronaldo.
Tayari mabadiliko yameanza kufanyika na baada ya sikh chache zijazo utatangazwa wakati wa uzinduzi rasmi.
Ronaldo
ni Mreno aliyezaliwa kisiwani humo, kisiwa ambacho kilo karibu na kile
cha Hispania kinachomilikiwa na Hispania Cha Tenerife ambacho Mtanzania,
Farid Mussa anacheza soka hapo.
Ronaldo
amekuwa nahodha wa kwanza kuiwezesha Ureno kubeba ubingwa wa Ulaya,
mchezaji mwenye mafanikio akiwa England (Manchester United), Hispania na
Real Madrid pia amefanikiwa kubeba ubingwa wa Ulaya na kuwa mchezaji
bora wa dunia mara kadhaa.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment