Mwenyekiti
wa CUF anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama Siasa, Prof. Ibrahim
Lipumba amelalamikia kitendo cha Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim
Seif Sharrif Hamad kuzifunga akaunti zote za chama hicho za wilaya.
Ameyasema
hayo wakati wa kikao cha baraza la uongozi linaloongozwa na upande
wake. Profesa Lipumba amesema kutokana na uamuzi huo ruzuku ya chama
kutoka serikalini wameikosa.
“Wajumbe
nawashukuru kwa kuja ili kupata fursa ya kujenga chama. Chama chetu
kipo ndani ya mtihani ambao kwa kweli chanzo chake ni Katibu Mkuu wetu
kutoheshimu katiba yetu na kutoheshimu taratibu za kidemokrasia,” amesema Prof. Lipumba.
Aidha,
Prof. Lipumba amesema kuwa Maalim Seif alitakiwa kuhudhuria kikao hicho
na alipewa taarifa lakini hakuweza kufika, hali iliyosababisha majukumu
yake kusimamiwa na Naibu Katibu Mkuu wa CUF Tanzania Bara. Magdalena
Sakaaya.
Kwa
upande wake, Naibu Katibu Mkuu wa CUF (Zanzibar), Nassor Mazrui amesema
kuwa hatua ya kufunga akaunti za benki imelenga kulinda fedha ya chama
ili zisitumiwe vibaya na upande wa Profesa Lipumba.
Hata
hivyo, Msajili wa Vyama vya Siasa bado anamtambua Prof. Lipumba kuwa ni
Mwenyekiti wa chama hicho kwa kuwa hakuwa na taarifa kuhusu uamuzi wake
wa kujiuzulu.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment