Mahakama
ya Hakimu Mkazi Arusha leo imesikiliza malalamiko ya watuhumiwa 61
wanao kabiliwa na kosa la ugaidi, ambapo ni shauri lililofunguliwa mwaka
2014.
Wakizungumza
leo mahakamani hapo watuhumiwa hao wamesema kuwa leo ndiyo itakuwa
mwisho wao kufika kwenye viwanja vya mahakama hiyo mpaka upande wa
jamuhuri utakapo kamilisha upelelezi wao.
Wamesema
wamekuwa wakifika mahakamani kwa muda ambapo wengi wao familia
zinateseka na kusambaratika sababu ya kukaa mahabusu kwa miaka minne kwa
makosa ya kusingiziwa.
Aidha
wamesema wamekuwa wakipewa ahadi hewa na mkuu wa upelelezi kuwa
angeshughulikia shauri hilo ndani ya miezi mitatu na kwamba suala la
mahakama kushindwa kutekeleza wajibu wake wa kikatiba linaleta ukakasi
kwa wananchi.
Hakimu
Mfawidhi Nestory Baro wa mahakama hiyo amewataka watuhumiwa kuwa na
subira wakati wakishughulikia shauri lao ambapo kesi itatajwa April 11
mwaka huu na amewataka kufika mahakamani siku hiyo bila kukosa wakati
akifanya utaratibu wa kumtafuta mkuu wa upelelezi na kuzungumza naye
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment