Kocha wa Botswana, Peter Butler ameukubali uwezo wa mshambuliaji wa
Taifa Stars, Mbwana Samatta aliyepachika mabao mawili kwenye mchezo wa
kirafiki, ambao ulichezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Samatta aliwaadhibu Botswana kwa kufunga bao la kwanza dakika ya pili,
baadaye kufunga la pili kwa shuti la adhabu kiufundi dakika ya 87, pia
alionekana kuwa hatari kwenye lango la Botswana mara kadhaa.
Utofauti wa matokeo umetajwa kusababishwa na Mshambuliaji huyo wa KRC
Genk ya Ubelgiji kutokana na uwezo wake mzuri wa kucheka na nyavu
alionao, licha ya muda mwingi Botswana kuoneka kumiliki asilimia kubwa
ya mchezo.
"Ni ngumu kucheza ugenini kwa huku Afrika, lakini timu yangu imejitahidi
kucheza vizuri, muda mwingi tulikuwa tunamiliki mpira lakini
haikutusaidia pamoja na kuwa tulibadili mfumo kwa lengo la kutaka
tutengeneze nafasi.
"Nahodha wa Tanzania 'Samatta' alicheza vizuri na ndiye aliyekuwa
mchezaji hatari zaidi kwetu kipindi chote cha mchezo, amefunga mabao
mawili ambayo yameleta utofauti, kwa kipindi chote Tanzania walikuwa
bora kwenye eneo lao la ushambuliaji ukilinganisha na timu yangu.
"Tumepata ushindani wa kutosha kitu ambacho nilikuwa nakihitaji kwenye
timu yangu, ambayo imeundwa na vijana nadhani hata kwa Tanzania itakuwa
hivyo kwakuwa tumewapa upinzani, bila shaka kocha naye atakuwa
ameufurahia upinzani tulioutoa kwa timu yake," alisema Butler.
Kocha huyo wa Botswana aliwai kuzitumikia klabu ya West Bromwich Albion
mwaka 1992–1994 ambapo alicheza mechi 70 na kufunga mabao 3 akitumika
kama kiungo na baadaye alitua Notts County ambako hakudumu kwa misimu
mingi na mwishowe alisajiliwa West Ham United zote za nchini Uingereza.
Kipa wa Botwana, ambaye alitunguliwa mabao mawili na Samatta, Kabelo
Dambe anayekipiga kwenye klabu ya Platinum Stars nchini Afrika Kusini
alisema mshambuliaji huyo ni moja katiwashambuliaji bora Afrika, ambao
amekumbana nao.
"Amenifunga mabao ambayo si mepesi, lile la kwanza ilikuwa nilisogea
kidogo ili kulifanya goli kuwa dogo kwa mshambuliaji, lakini alinifunga
kwenye hali ile na hata bao la pili alitumia akili kwasababu niliwapanga
wachezaji wenzangu kwenye ukuta.
"Alichokifanya nahodha wa Tanzania ni kupiga mpira kwa haraka kabla ya
hata sijakaa sawa golini, lakini tulijitahidi kucheza vizuri ila
hatukuwa na bahati ya kufunga mabao kitu ambacho wenzetu waliweza,"
alisema Dambe.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment