Mwanamuziki
Nay wa Mitego ameachiwa huru kutoka katika Kituo cha Polisi cha Kati
Dar es Salaam ikiwa ni saa chache tangu Rais Dkt Magufuli aliporuhusu
kuchezwa redioni kwa wimbo wake uliokuwa umefungiwa na BASATA.
Agizo
hilo la Rais Magufuli limetolewa leo na Waziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo Dkt Mwakyembe alipokuwa akizungumza na waandishi habari
mkoani Dodoma.
Waziri
Mwakyembe alisema kuwa Rais Magufuli amesema wimbo huo ni mzuri, na
kumshauri Nay wa Mitego aongezee mambo mengine kama kuwataja watu ambao
wanakwepa kodi, watumiaji wa dawa za kulevya.
Nay
wa Mitego alikamatwa usiku wa kuamkia jana ambapo alipelekwa katika
Kituo cha Polisi Mvomero na baadae alisafirishwa hadi Kituo cha Polisi
cha Kati jijini Dar es Salaam.
Baada
ya kutoka, Nay wa Mitego amezungumza na waandishi wa habari na
kuwashukuru wale wote waliojitokeza na kumsaidia kwa namna yoyote ile.
Amewashukuru
Watanzania wote lakini pia wasanii waliokwenda kumuona na kumtumia
jumbe za kumpa moyo, lakini pia mawakili wake waliopambana kwa muda wote
kuhakikisha kuwa haki yake inakuwepo na kulindwa.
"Asante kwa wote walioamka na kuwa upande wangu, upande wa haki, walioamini kile ambacho nimekifanya nawashukuru sana". Amesema Nay wa Mitego
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment