Thursday, 3 September 2015

#YALIYOJIRI>>>Karatasi za kupigia kura kuletwa kutoka Afrika Kusini.Fahamu zaidi hapa.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesema asilimia kubwa ya maandalizi ya uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 25, mwaka huu yamekamilika, huku karatasi za kupigia kura zikitokea Afrika Kusini.
Aidha, tume hiyo imesema gharama za awali kwa ajili ya ununuzi wa vifaa mbalimbali kama vile wino, fulana, kofia, karatasi za kura, vibanda vya kupigia kura na vifaa vya kufungashia katika uchaguzi huo hadi sasa zimefikia Sh. bilioni 31.25.

Imesema dola za Marekani 6, 145, 882.92 sawa na Sh. bilioni 13.1 zinatarajiwa kutumika kwa ajili ya ununuzi karatasi hizo za kura. Hayo yalisemwa na Mkurugenzi wa Manunuzi na Menejimenti ya Lojistiki wa Nec, Eliud Njaila, wakati akizungumza na Nipashe, jijini Dar es Salaam jana.

Alisema karatasi hizo zinatarajia kuanza kuwasili nchini Septemba 29 hadi Oktoba 15, mwaka huu.

Alisema gharama za vifaa hivyo ni tofauti na zile zilizotumiwa na tume hiyo kwa ajili ya kununulia mashine 8,000 za Biometric Voters Registration (BVR) na shughuli nzima ya uandikishaji kwenye Daftari la Wapigakura nchi nzima, ambazo kwa mujibu wa Nec ni Sh. bilioni 133.

Tume hiyo pia ilisema Sh. bilioni 85 zilitumika kulipa posho waandikishaji, wataalamu wa mashine hizo, kutengeneza kadi, karatasi, wino na vifaa muhimu wakati wa uandikishji kwenye daftari hilo nchini kote. Alitaja kampuni iliyoshinda zabuni ya wazi ya kutengeneza karatasi hizo kuwa ni Uniprint ya nchini Afrika Kusini ambayo alisema ina uzoefu mkubwa katika kazi hiyo kwani ndiyo iliyoshinda zabuni ya kutengeneza vifaa hivyo katika uchaguzi mkuu nchini humo wa Tanzania wa mwaka 2005.

#MICHEZO>>Kipa wa Nigeria Enyema aikosa mechi ya Taifa Start's iyo Jumamosi.Fahamu zaidi hapa.

Kipa wa Nigeria Vincent Enyema, amejiondoa kutoka kwa kikosi cha Nigeria, kitakachoshiriki katika mechi ya kufuzu kwa fainali ya kombe la Mataifa ya Afrika, mwaka wa 2017, dhidi ya Tanzania siku ya Jumamosi kufuatia kifo cha mamake.
Kocha wa Nigeria, Sunday Oliseh, amesema kwa sasa Enyema, amepata pigo kubwa na tumemruhusu kwenda nyumbani kwa misingi ya kibinadam.
Enyema alitarajiwa kusafiri Abuja siku ya Jumatatu, lakini alifutilia mbali safari hiyo.
Kipa wa timu ya Uingereza ya Wolves, Carl Ikeme, anatarajiwa kujaza pengo hilo katika mechi itakayokuwa ya kwanza katika timu hiyo ya Super Eagles.
Enyema, anayeichezea klabu ya Ufaransa ya Lille na mchezaji aliyecheza mechi nyingi zaidi katika kikosi cha Super Eagles, alikuwa kipa wa timu hiyo wakati ilipoicharaza Chad kwa magoli mawili kwa moja mjini Kaduna mwezi Juni mwaka huu.
Toa maoni yako hapa.

#YALIYOJIRI>>>WAZIRI WA ZAMANI MH.FREDERICK SUMAYE AMJIBU DR.SLAA.FAHAMU ZAIDI HAPA.

Meneja wa kampeni wa vyama vinavyounda umoja wa katiba(UKAWA) na waziri mkuu mstaafu wa serikali ya CCM ya awamu ya tatu BW FREDERICK TLUWAY SUMAYE amewataka watanzania kupuuza tuhuma za ufisadi zilizotolewa na aliyekuwa katibu mkuu wa CHADEMA Dr.Wilborad Slaa dhidi ya mgombea urais wa UKAWA Bw. Edward Lowassa pamoja na yeye na kueleza kwamba hawatapoteza muda wa kumjibu kwani hizo ni hila zilizopangwa kutaka kufifisha mabadiliko wanayohitaji kwa watanzania.

#MICHEZO>>Argentina yawa juu Viwango vya soka Duniani.Fahamu zaidi hapa.

Shirikisho la Soka duniani Fifa imetoa orodha ya Ubora Duniani kwa mwezi wa Nane ambapo Argentina inaongoza ikiwa nafasi ya kwanza.
Ubelgiji wao wako katika nafasi ya pili huku mabingwa wa dunia Ujerumani wakiwa katia nafasi ya tatu.
Kwa Afrika, Nchi za juu kabisa ni zile zile na zimeshika Nafasi hizo hizo za Mwezi uliopita na hizo ni Algeria ambao wako Nafasi ya 19 wakifuaťiwa na Ivory Coast ambao ni wa 21.
Kwa nchi za ukanda wa afrika mashariki Uganda wanaongoza wakiwa nafasi ya 71,Rwanda wako nafasi ya 78, kenya wao wanashika nafasi ya 116, Burundi wao wako nafasi 134 huku Tanzania wakiwa nafasi ya 140.
Orodha ya ubora duniani
1 Argentina
2 Belgium
3 Germany
4 Colombia
5 Brazil
6 Portugal
7 Romania
8 Chile
9 Wales
10 England
Poa maoni yako hapa.

#YALIYOJIRI>>>TANZANIA NA VIETNAM WASHEREHEKEA MIAKA 50 YA USHIRIKIANO WA KIDIPLOMASIA.Fahamu zaidi hapa.

 Mhe. Pinda (kushoto) akisalimiana na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali katika Wizara ya Mambo ya Nje, Bi. Mindi Kasiga.
 Waziri Mkuu, Mhe. Mizengo Pinda (kulia) na Balozi wa Vietnam nchini, Mhe. Vothanh Nam (kushoto) wakiwa wamesimama kwa pamoja tayari kwa nyimbo za mataifa yao.
 Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Yahya Simba (wa pili kutoka kulia) kwa pamoja na Mke wa Balozi wa Vietnam nchini na Kiongozi wa Mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini ambaye pia ni Balozi wa Demokrasia ya Kongo nchini Balozi Juma Mpango (kushoto) wakiwa wamesimama wakati nyimbo za taifa la Tanzania na Vietnam zikiimbwa.
 Huyu ni Mabalozi mbalimbali wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini nao wakiwa wamesimama tayari kwa kuimba  nyimbo za Taifa
 Hii ni Sehemu ya wageni waalikwa kwenye maadhimisho hayo.
 Kikundi cha Polisi cha Brass Band kikipiga nyimbo za Mataifa hayo mawili wakati wa Maadhimisho hayo
 Huyu ni Balozi wa Vietnam nchini, Mhe. Vothanh Nam naye akizungumza katika hafla hiyo.
 Afisa Mambo ya Nje Bw. Emmanuel Luangisa (katikati) akifuatilia hotuba kwenye kitabu iliyokuwa ikisomwa na Mhe. Waziri Mkuu (hayupo pichani)
 Waziri Mkuu akitakiana afya njema na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Balozi Yahya Simba (wa pili kutoka kulia). Mwenye nguo nyekundu  ni Mke wa Balozi wa Vietnam nchini  na kulia ni Afisa kutoka  Ubalozi wa Vietnam nchini.
 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  Mhe. Mizengo Pinda akizungumza katika hafla ya maadhimisho ya Miaka 50 ya Mahusiano ya Kidiplomasia kati ya Tanzania na Vietnam. Katika hotuba yake Mhe. Pinda alilishukuru Taifa la Vietnam kupitia Ubalozi wake nchini kwa kuendelea kuimarisha ushirikiano  na Tanzania katika nyanja mbalimbali zikiwemo za kiuchumi, biashara na kidiplomasia. Hafla hiyo ilifanyika katika Hotel ya Serena Jijini Dar es Salaam tarehe 02 Septemba 2015.
 Waziri Mkuu, Mhe. Pinda (kulia) na Balozi wa Vietnam nchini Mhe. Vothanh Nam (kushoto) wakitakiana afya njema  kwenye hafla hiyo.
 Mhe. Pinda akikata Keki pamoja na Balozi Nam ikiwa ni ishara ya kuadhimisha miaka 50 ya ushirikiano wa Kidiplomasia kati ya Tanzania na Vietnam.
Hawa ni Maafisa kutoka Wizara ya  Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa nao wakiwa na nyuso za furaha wakati wa maadhimisho hayo. 
Toa maoni yako hapa.

Nimewaekea Vikatuni watu wangu hapa.


Wednesday, 2 September 2015

Download nyimbo ya BouNako ft LordEyes - Bado Tunapeta.Ipo hapa.


#YALIYOJIRI>>UKAWA Kupitia Mh Mbatia amjibu Dr Slaa.Kiko hapa.


Download nyimbo mpya ya P-Square – OMG(Free Me) hapa.


#YALIYOJIRI>>Irene Uwoya akiwa Anapiga Kampeni ipo hapa.


#MICHEZO>>Fahamu Timu zilizotumia Pesa nyingi kwenye Usajili wa England hapa.

Unaambiwa kipindi hiki cha usajili ndio kimevunja rekodi ya kutumia pesa nyingi zaidi ukiacha miaka iliyopita. Ishu ni kwamba usajili mkubwa haumaanishi ndio ubingwa upo mezani, lakini kwa kiasi kikubwa inachangia.
Manchester city imefanya usajili wa nguvu sana na inaongoza kwenye hii list. Matunda ya usajili wao umeanza kuoneka mwanzo wa ligi na wamepata matokeo mazuri. Lakini ligi ya uingereza haiwezi kutabirika mapema tusubiri hadi hapo baadae.
Hii hapa ni list ya club za EPL kwa pesa walizozitumia kwenye usajili. Listi imepangwa kutokana na net spend ambayo ni tofauti kati ya pesa zilizotumiaka toa pesa zilizopokewa.

#MICHEZO>>>Fahamu orodha ya wachezaji ambao wamehama kwenye Timu zao Ligi mbali mbali.

 Hii ni orodha ya wachezaji ambao wamehama au kuhamia klabu nyingine ulimwenguni kote (ligi moja kwenda lingi nyingine).
Jason Denayer [Manchester City – Galatasaray] Loan
Julian Draxler [Schalke – Wolfsburg] Undisclosed
Emanuele Giaccherini [Sunderland – Bologna] Loan
Javi Guerra [Cardiff – Rayo Vallecano] Undisclosed
Javier Hernandez [Manchester United – Bayer Leverkusen] £7.3m
Hernanes [Inter Milan – Juventus] £9.5m
Brown Ideye [West Brom – Olympiakos] Undisclosed
Adnan Januzaj [Manchester United – Borussia Dortmund] Loan
Olivier Kemen [Newcastle – Lyon] £550,000
Mario Lemina [Marseille – Juventus] Loan
Modibo Maiga [West Ham – Al Nassr] Undisclosed
Emmanuel Mayuka [Southampton – Metz] Undisclosed
Felipe Melo [Galatasaray – Inter Milan] £8m
Loic Nego [Charlton – Videoton] Undisclosed
Stefan Scepovic [Celtic – Getafe] Loan
Ricky van Wolfswinkel [Norwich – Real Betis] Loan
Etien Velikonja [Cardiff – Lierse SK] Undisclosed
Jelle Vossen [Burnley – Club Brugge] Undisclosed
Chanzo: Mtando wa BBC SPORT

#YALIYOJIRI>>>Dk. John Magufuli akiwa anautubia huko Mtwara hii leo.

Mgombea Urais CCM Dk. John Magufuli ameahidi kujenga hospitali za rufaa kila mkoa iwapo atachaguliwa kuingia Ikulu

#YALIYOJIRI>>>Mgombea Urais CCM Dr.John akicheza music na Bendi ya Yamoto huko Mtwara hii leo.

 Mgombea Urais CCM Dr.John akiyarudi mangoma kutoka kwa wanamuziki wa bendi ya Yamoto mtwara leo
 Mgombea Urais CCM Dr.John akicheza muzic huko Mtwara.

Bendi ya Yamoto iwa inamiliki Jukwaa huko Mtwara hii leo.

Tuesday, 1 September 2015

#YALIYOJIRI>>>Edward Lowassa mgombea urais kupitia UKAWA apokelewa na Maeflu Huko Ruvuma Hii leo.Fahamu zaidi hapa.

 Mgombea Urais wa UKAWA, Mhe. Edward Lowassa akiwa na waziri mstaafu Fredick Sumaye, Mkoani Ruvuma
 Umati wa wakazi wa Mkoa wa Ruvuma wakiwa katika mkutano wa Mgombe Urais wa UKAWA, Mhe. Edward Lowassa
 Hawa ni WanaRuvuma wakiwa kwenye mkutano wa UKAWA hii leo.
 Hawa ni maelfu wa WanaRuvuma wakiwa wameshikilia mabango yenye ujumbe mbali mbali.
 Mgombe Urais wa UKAWA Mhe. Edward Lowassa akiwasalimia wakazi Mkoa wa Ruvuma.
 Umati wa watu wanaunga mkono UKAWA wakiwa katika mkutano, Kumsikiliza Mgombe Urais Mhe. Edward Lowassa.
 Wananchi wa Songea waliojitokeza katika viwanja vya Matalawe, kumsikiliza Edward lowassa.

  Hawa ni maelfu wa WanaRuvuma wakiwa wameshikilia mabango na Bendera yenye ujumbe mbali mbali.
Waziri wa zamani Sumaye akiwa anawautubia Wananchi wa Ruvuma hii leo.
Toa maoni yako hapa.

#MICHEZO>>David De Gea ni Lawama Tu.Fahamu zaidi hapa.

Klabu ya Real waliomkosa kipa waliyemtarajia, David De Gea kutoka Manchester United, wamesema bayana kwamba walifanya kila waliloweza kukamilisha usajili huo lakini Mashetani Wekundu ndio walikwamisha mchakato.
Katika taarifa yao, Madrid wanasema kwamba United walifungua mazungumzo juu ya kumtoa kipa huyo ili nao wamchukue wa Madrid, Keylor Navas lakini United wakachukua saa nane nzima kujibu masuala ya mikataba ya wawili hao.
Madrid waliomruhusu kipa wao namba moja, Iker Casillas aliyekuwa pia nahodha wao ajiunge na Porto wa Ureno, wanasema kwamba walifikia makubaliano haraka na United juu ya usajili, na kwamba saa 7:39 mchana wa Jumatatu waliwatumia Man U mikataba husika,lakini United wakakaa kimya hadi saa 3:43 usiku walipowatumia marekebisho kidogo.
 Toa maoni yako hapa.