Mhe.
 Pinda (kushoto) akisalimiana na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya 
Serikali katika Wizara ya Mambo ya Nje, Bi. Mindi Kasiga.
 Waziri
 Mkuu, Mhe. Mizengo Pinda (kulia) na Balozi wa Vietnam nchini, Mhe. 
Vothanh Nam (kushoto) wakiwa wamesimama kwa pamoja tayari kwa nyimbo za 
mataifa yao.
 Naibu
 Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi 
Yahya Simba (wa pili kutoka kulia) kwa pamoja na Mke wa Balozi wa 
Vietnam nchini na Kiongozi wa Mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa 
nchini ambaye pia ni Balozi wa Demokrasia ya Kongo nchini Balozi Juma 
Mpango (kushoto) wakiwa wamesimama wakati nyimbo za taifa la Tanzania na
 Vietnam zikiimbwa. 
 Huyu ni Mabalozi mbalimbali wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini nao wakiwa wamesimama tayari kwa kuimba  nyimbo za Taifa
 Hii ni Sehemu ya wageni waalikwa kwenye maadhimisho hayo.
 Kikundi cha Polisi cha Brass Band kikipiga nyimbo za Mataifa hayo mawili wakati wa Maadhimisho hayo
 Huyu ni Balozi wa Vietnam nchini, Mhe. Vothanh Nam naye akizungumza katika hafla hiyo.
 Afisa
 Mambo ya Nje Bw. Emmanuel Luangisa (katikati) akifuatilia hotuba kwenye
 kitabu iliyokuwa ikisomwa na Mhe. Waziri Mkuu (hayupo pichani) 
 Waziri
 Mkuu akitakiana afya njema na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya 
Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Balozi Yahya Simba (wa pili kutoka 
kulia). Mwenye nguo nyekundu  ni Mke wa Balozi wa Vietnam nchini  na 
kulia ni Afisa kutoka  Ubalozi wa Vietnam nchini. 
 Waziri
 Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  Mhe. Mizengo Pinda 
akizungumza katika hafla ya maadhimisho ya Miaka 50 ya Mahusiano ya 
Kidiplomasia kati ya Tanzania na Vietnam. Katika hotuba yake Mhe. Pinda 
alilishukuru Taifa la Vietnam kupitia Ubalozi wake nchini kwa kuendelea 
kuimarisha ushirikiano  na Tanzania katika nyanja mbalimbali zikiwemo za
 kiuchumi, biashara na kidiplomasia. Hafla hiyo ilifanyika katika Hotel 
ya Serena Jijini Dar es Salaam tarehe 02 Septemba 2015.
 Waziri
 Mkuu, Mhe. Pinda (kulia) na Balozi wa Vietnam nchini Mhe. Vothanh Nam 
(kushoto) wakitakiana afya njema  kwenye hafla hiyo. 
 Mhe.
 Pinda akikata Keki pamoja na Balozi Nam ikiwa ni ishara ya kuadhimisha 
miaka 50 ya ushirikiano wa Kidiplomasia kati ya Tanzania na Vietnam. 
Hawa ni Maafisa kutoka Wizara ya  Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa nao wakiwa na nyuso za furaha wakati wa maadhimisho hayo. 
Toa maoni yako hapa.
 








 




 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
0 comments:
Post a Comment