Thursday, 3 September 2015

#YALIYOJIRI>>>Karatasi za kupigia kura kuletwa kutoka Afrika Kusini.Fahamu zaidi hapa.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesema asilimia kubwa ya maandalizi ya uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 25, mwaka huu yamekamilika, huku karatasi za kupigia kura zikitokea Afrika Kusini.
Aidha, tume hiyo imesema gharama za awali kwa ajili ya ununuzi wa vifaa mbalimbali kama vile wino, fulana, kofia, karatasi za kura, vibanda vya kupigia kura na vifaa vya kufungashia katika uchaguzi huo hadi sasa zimefikia Sh. bilioni 31.25.

Imesema dola za Marekani 6, 145, 882.92 sawa na Sh. bilioni 13.1 zinatarajiwa kutumika kwa ajili ya ununuzi karatasi hizo za kura. Hayo yalisemwa na Mkurugenzi wa Manunuzi na Menejimenti ya Lojistiki wa Nec, Eliud Njaila, wakati akizungumza na Nipashe, jijini Dar es Salaam jana.

Alisema karatasi hizo zinatarajia kuanza kuwasili nchini Septemba 29 hadi Oktoba 15, mwaka huu.

Alisema gharama za vifaa hivyo ni tofauti na zile zilizotumiwa na tume hiyo kwa ajili ya kununulia mashine 8,000 za Biometric Voters Registration (BVR) na shughuli nzima ya uandikishaji kwenye Daftari la Wapigakura nchi nzima, ambazo kwa mujibu wa Nec ni Sh. bilioni 133.

Tume hiyo pia ilisema Sh. bilioni 85 zilitumika kulipa posho waandikishaji, wataalamu wa mashine hizo, kutengeneza kadi, karatasi, wino na vifaa muhimu wakati wa uandikishji kwenye daftari hilo nchini kote. Alitaja kampuni iliyoshinda zabuni ya wazi ya kutengeneza karatasi hizo kuwa ni Uniprint ya nchini Afrika Kusini ambayo alisema ina uzoefu mkubwa katika kazi hiyo kwani ndiyo iliyoshinda zabuni ya kutengeneza vifaa hivyo katika uchaguzi mkuu nchini humo wa Tanzania wa mwaka 2005.

Related Posts:

  • MAITI yaokotwa Bwawani. Mwili wa mtu ambaye hajafahamika umeokotwa katika bwawa la maji lililopo Mtaa wa Nkende Shuleni katika Halmashauri ya Mji wa Tarime. Hili ni tukio la tatu la watu kuuawa kisha miili yao kutupwa kwenye mabwawa ya maji kat… Read More
  • VIDEO: Magufuli Afungwe Breki- Halima Mdee. Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Chadema Halima Mdee kwa mwenendo anao kwenda nao Rais Magufuli analipeleka taifa pabaya na kwamba Watanzania wanapswa kumfunga breki kwa kuonesha kutofurahishwa na matendo yake. Mdee ameya… Read More
  • Minykano ya Kisiasa na vijembe ndani ya Bunge. MJADALA wa kujadili miswada ya rasilimali za madini ulianza jana Bungeni, huku ukigubikwa na minykano ya Kisiasa na vijembe ndani ya Bunge. Miongoni mwa vijembe hivyo ni Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema,… Read More
  • SERIKALI YATANGAZA NAFASI 400 ZA AJIRA MAMLAKA YA MAPATO TRA. SERIKALI YATANGAZA NAFASI 400 ZA AJIRA MAMLAKA YA MAPATO TRA, BONYEZA HAPA CHINI KU APPLY, SHARE NA MARAFIKI.  <<<<KU APPLY BOFYA HAPA>>> Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye S… Read More
  • MADUKA ya Supermarkets za Nakumatt Hali Tete. Mamia ya wafanyakazi huenda wakakosa ajira Afrika Mashariki baada ya maduka ya jumla ya Nakumatt kuonekana kuwa hatarini. Nakumatt iliyo na maduka nchini Kenya, Uganda, Tanzania na Rwanda inakabiliwa na changamoto za kuli… Read More

0 comments:

Post a Comment