Askari
wawili wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa kutoka Tanzania, wameuawa
kwenye mashambulizi makali yanayoendelea nchini Kongo.
Tukio
hilo limetokea katika eneo la Beni ambako Askari wa Umoja wa Mataifa wa
kulinda amani wanapigana na kikundi cha waasi cha Uganda (ADF),
kilichoanza vurugu na ukiukaji wa haki za binadamu kwa kuua raia.
Katibu
Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amethibitisha kuuawa kwa
wanajeshi hao kutoka Tanzania, huku akitoa tarifa kuwa askari wengine 18
kutoka nchi tofauti wamejeruhiwa.
Pamoja
na hayo Katibu Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa amehimiza mamlaka za Kongo
kuchunguza haraka tukio hilo na kuwachukulia hatua wahusika.
Hivi
karibuni nchini Kongo kumekuwa na machafuko baada ya vikundi vya uasi
kuanza tena vurugu na mauaji baada ya miaka kadhaa kupita kukiwa shwari,
huku serikali ya nchi hiyo na Umoja wa Mataifa wakiishtaki ADF kwa
ukiukaji wa hai za binadamu na mauaji ya watu zaidi ya 700 katika eneo
la Beni, tangu Oktoba 2014.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment