Mbunge
wa Kigoma Mjini kwa tiketi ya ACT Wazalendo, Zitto Kabwe amefunguka na
kusema kuwa uchumi wa nchi unazidi kudidimia na thamani ya shilingi
inazidi kushuka huku mfumuko wa bei ukizidi kupaa.
Zitto
Kabwe anasema kupitia Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) ambayo jana
ametoa taarifa yake juu ya hali ya uchumi nchini ni kwamba hali si nzuri
kwani uchumi umeonyesha kusinyaa na kudidimia huku wananchi wa hali ya
chini wakiwa wahanga wakubwa zaidi.
"Taarifa
hiyo inaonyesha namna hali ya uchumi wetu inavyozidi kuwa mbaya zaidi
kwa wananchi wa hali ya chini , kwa mfumuko wa bei umepanda mno tangu
kuanza kwa utekelezaji wa bajeti ya 2017/18, ongezeko ambalo
limechangiwa zaidi na kupanda kwa bei ya bidhaa za chakula (bidhaa
ambazo wananchi wengi zaidi wanazitumia)" alisema Zitto Kabawe
Aidha
Zitto Kabwe amedai kushuka kwa thamani ya sarafu ya Tanzania kumezidi
kuongeza maumivu kwa wananchi na ili kusaidia kupunguza ukali na gharama
za maisha mishahara ilipaswa kupanda kwa asilimia 8 zaidi.
"Thamani
ya sarafu ya Tanzania imeshuka, uwezo wa Tsh. 100 kununua bidhaa
umeshuka hadi Tsh. 92.18. Maana yake ni kuwa mwaka 2016 shilingi 100,000
ilikupa bidhaa za shilingi 100,000. Mwaka huu 2017 shilingi 100,000
inakupa bidhaa za shilingi 92,000.
"Kwa
hiyo ili upate bidhaa za shilingi laki moja inakubidi uongeze shilingi
elfu 8 zaidi. Kiuchumi, ili kulinda hali za wananchi, mishahara ilipaswa
kupanda kwa asilimia 8 ili kuwapunguzia maumivu ya gharama za maisha.
"Lakini
hali hiyo inatokea katika wakati ambao mishahara haijapanda, na Rais wa
nchi yetu kasema Serikali anayoingoza haitapandisha kabisa mishahara.
Hali ni mbaya mno mtaani, mijini uzalishaji wa bidhaa za viwanda
umeshuka kwa zaidi ya nusu, kutoka trilioni 1.5 mpaka bilioni 700 tu"
alisisitiza Zitto Kabwe
Mbali
na hilo Zitto Kabwe ametoa ushauri wa nini serikali inapaswa kufanya
ili kukabiliana na hali hiyo na kupunguza ukali wa maisha kwa wananchi
Zitto
amedai Serikali inapaswa itazame namna inatekeleza mipango yake ya
Maendeleo, Serikali isikilize na kufanyia kazi mawazo ya sekta binafsi
katika kuweka sawa mazingira ya uwekezaji bila kupoka haki ya nchi
kufaidi na rasilimali zake na pia ameitaka serikali ifanyie kazi haswa
uchumi wa vijijini kwa kurekebisha mapungufu yote yanayoshusha
uzalishaji kwenye sekta ya kilimo.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment