Wakili
Peter Kibatala ameiandikia barua Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu,
akiomba kujitoa kumuwakilisha msanii wa filamu nchini, Wema Sepetu
katika kesi ya dawa za kulevya inayomkabili.
Hatua
hiyo imekuja leo Jumatano, baada ya shauri lililopita Desemba 12, mwaka
jana, mahakama hiyo kuelezwa kuwa wakili wa Wema hajafika na kushindwa
kuendelea kusikiliza kesi hiyo.
Mbali
na wakili Kibatala kuomba kujitoa katika kesi hiyo, mahakama hiyo
imepokea barua kutoka kwa Wakili Albert Msando kuomba kumuwakilisha Wema
katika kesi hiyo na kwamba aliomba apewe muda wa kupitia jalada hilo
kabla ya kuendelea na kesi.
Hakimu
Mkazi Mkuu, Thomas Simba anayesikiliza shauri hilo, amesema kuwa
amepokea barua hizo Januari 9, mwaka huu na kuahirisha kesi hiyo hadi
Februari 8, mwaka huu, itakaposikilizwa.
Washtakiwa wengine katika kesi hiyo ya kutumia dawa za kulevya ni Angelina Msigwa na Matrida Abbas.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment